Natafuta vijana wa kufyatua matofali

Kama kichwa Cha habari kinavyosema hapo juu natafuta vijana watatu nitaowaajiri waje wafyatue matofali malipo ni 5000 Kwa siku kula juu Yao Kwa waliotayari waje pm mda huu Kwa mnaohitaji nimeamua kutoa ajira Kwa vijana wenzangu Ili tuweze kusonga mbele


Kula juu yao tena kwa hiyo 5,000? Wewe kweli unaishi maisha magumu mno, binadamu gani huyo atakubali, kumbuka kibarua yeyote yule sasa hivi wa ujenzi ikiwa pamoja na kufyatua tofali ni tshs 10,000 hapo ndio chakula juu yake..!

Sasa utoe 5,000 kwanza hupati kibarua, kazi ya tofali utawaumiza, nakushauri tafuta mashine ya kufyatulia tofauli complete, itachanganya cement na mchanga na kumimina kwenye sehemu ya kupiga tofali alafu watu wanahamisha tu, ila sio kutumia mtu kama mashine kwa tshs 5,000 kwa siku
 
Back
Top Bottom