Natafuta shule kwa Mtoto wa Miaka 3 (Boarding)

Sijui mazingira yako au umekumbwa na nini lakini hii bado kwangu haipo sawa.

Labda kama unapelekwa gerazani na huna ndugu mwingine yoyote wa kumwangalia mwanao.
 
Mkuu nimeshafikilia mara kufikilia nimefikia uamuzo huo kama unazijua shule naomba nitajie!
Sidhani kama ulifikiria kweli ilo wazo lako,nahisi lilikujia gafla tu...Mtoto wa Miaka mi3+ unampeleka boarding? Nope unaenda Kumuumiza tu.
 
Hivi wazazi wengine mnafahamu maana ya mtoto? Kwenu nyie Tv au simu zina thamani kuliko mtoto wenu na damu zenu, nasema hivyo kwa sababu kama ningekwambia niazime simu yako au Tv yako kwa mwaka mmoja husingekubali. Hv unathubutuje kumchukua mtoto mwenye miaka 3 au 4 kumkabidhi kwa mtu husiyemfahamu?

Unachokifanya ni unyama, hebu muangalie mtoto wako usoni fikiri huyu mtoto unampeleka kwa mtu ambaye hajawahi kumuona, na unamuacha kwa huyu mtu wiki au miezi hv hii shule ya mtoto wenye miaka 3 ni muhimu kiasi hicho? Hiv huna mama umpeleke mtoto wako kwa hicho kipindi mpka mambo yako yakae sawa?
Watu wengi sana hapa duniani ni majipu au mabusha
 
Kama mzazi unaweza kufikiri kumpeleka mtoto mwenye umri mdogo utakuwa umetatua matatizo yako fulani. Ki uhalisia binafsi naona au nafananisha tendo la mzazi kumpeleka mtoto wa umri tajwa kama kosa la jinai. Tuwe wazazi responsible jamani!!!
 
We mzazi timiza wajibu wako. Naomba nisimulie visa viwili tofauti usome uelewe ndipo utoe uamuzi.

Kuna Mtoto wa kike alizaliwa nje ya ndoa. Baba wa Mtoto kwa kumuogopa mke wa ndoa aliogopa kumpeleka nyumbani baada ya mama wa Mtoto kufariki badala yake akamuingiza Shule moja ya Academy hapa Dar, baada ya wiki mbili alipigiwa simu anaitwa Shule kuna tatizo alipofika akakuta kesi watoto wa kindergarten wamemkeketa mwanaye wakati wana cheza. Sasa wote ni watoto wadogo utawafanya nini?

Kisa cha pili ni watoto wa kiume walikuwa wanamtia vidole mwenzao wakiingia chooni.
Watoto wamemkeketa mwenzao?!!!!!!!
 
Nilisoma boarding secondary school na niliipenda sana shule yangu ila moja ya vitu ambavyo sitakuja kufanya ni kumpeleka mwanangu shule ya bweni iwe primary au secondary. Huwa najiuliza inakuwaje mtu anampeleka mwanae boarding ni kwamba hawawapendi watoto wao au naona kama siwezi.

Kwa Mtoto wa miaka3 sio sahihi kabisa kumpeleka boarding labda kama humpendi, hii trend ya kupeleka watoto wadogo boarding itakuja watokea puani
 
Mtoto bado mdogo haifai kumpelekal boarding. Hadi 4 years
Hata miaka4 haifai kwa ujumla boarding school haifai kabisa kwa level yeyote, ni kuigana kusiko na faida kupeleka watoto boarding school, naona imekua ni kama sifa kusema mwanangu anasoma boarding, au kama inakuongezea status fulani kusomesha mtoto boarding ila ni mateso kwa mtoto na hupati kumjua na kumlea mwanao vile utakavyo. Huwa nahisi wapeleka watoto shule za bweni hawawapendi watoto wao enough maana binafsi siwezi
 
Ngoja nikuambie possible effects atakazopata mwanao.

Physically:
a) afya yake itadorora sababu kuu vyakula vya boarding mostly si balanced diet. Na huwapa watoto junk foods zinazowafanya mabonge. b) atakuwa mzembe na lege lege sababu boarding wanaishi kwa ratiba ambazo zinawaweka na masomo tuuu badala watoto wacheze ili misuli yao ikue.
c) Huduma za afya boarding piga ua haziko bora kama nyumbani sababu care taker 1 anahudumia watoto wengi attention si kama ya mzazi nyumbani.
d) Pia 3 years... clinic nani atampeleka akiwa boarding?
e) Vyoo vile umevifikiria!?
Socio-emotionally.
a) atapoteza mapenzi na wewe (attachment loss) atakuja kuwa mtu wa masela huko mbeleni maana ndo watakuwa wanaijenga dunia yake.
b) akishakuwa wa masela, tegemea kuwa na mtoto asiyetii.
c) ataiga kufanya au kufanywa ujinga mwingi kama wasemavyo wadau. Na hivi watoto wanaona kila kitu siku hizi. Akifika boarding anapewa "kaka".
Self-help skills.
a) hataweza kufanya mengi maana wanafanyiwa na wahudumu.

Yako mengi sana.. But ngoja niishie hapa.
 
Anyway kama umeamua huna njia.. Ngoja nikupe hints za kuchunguza hiyo sehemu unampeleka mwanao.

1.wachunguze wafanyakazi.
-Je watoto wanawaogopa au wanawafurahia!?
- Tone yao ya sauti wanayotumia kuongea ikoje?
-maneno wanayotamka say in case watoto wakiwaudhi ni sahihi na si matusi!?
Hayo ni kwa kulinda self-esteem na self concept ya mwanao.
Pia
-Uliza qualifications zao kielimu na tazama mavazi yao.
-Aina ya adhabu wanazotoa watoto wakifanya makosa.
-Uliza falsafa ya jumla ya hiyo boarding school.

2. Kuhusu mazingira
-je wana space salama na ya kutosha kucheza!?
-wana vifaa vya kuchezea
-Ratiba ya siku iko vipi, watoto wanapewa muda mwingi kucheza!?
-Vyoo viko salama!? Viko saizi ya watoto na Idadi it inatosha? Je watoto na wafanyakazi wanashea Vyoo!? (mbaya sana hii)
-Maji yapo masafi na salama? Uliza source ya maji.
-cheki ratiba ya chakula weekly. Aina ya vyakula iwe salama na balanced. Uliza chakula chao wanakitoa wapi!? (isiwe mboga from bonde la msimbazi)
-Ratiba ioneshe watoto wanalala mapema.
-Huko vyumbani wanalalaje na wangapi kwenye kitanda? (Muhimu sana hii), usafi wa bweni, mwanga na hewa ya kutosha.
-location ya shule pia inamatter sana. Isiwe imezungukwa na sehemu hatari zenye makelele weee mchana kutwa.

Anzia hapo.
Kuna mengi siwezi yaandika yote hapa.
NB: Mi nafanya mwaka wa mwisho EARLY CHILDHOOD EDUCATION Udsm. So nakushauri kwa uzoefu na matokeo ya tafiti. Tafadhali Fuatilia yote haya kwa usalama na ukuaji bora wa mwanao.
 
Kuna mada ya watoto naomba hizi post mbili uziweke pale tafadhali kama hutajali
 
Nina binamu yangu shoga. Anasema alivyokuwa na miaka sita binamu yake alitaka kumbusu. Akamkatalia. Basi toka siku hiyo anapenda wanaume.

Sasa subiri mtoto wake mleta Mada aonyeshwe kupendwa na kujaliwa huko shule ndo aelewe.
Anadhani ana solve mambo yake ila anatengeneza matatizo tu, kina watoto nawajua walikua 3 years ila wanainamishana, eeh Mungu anijalie uzima mtoto wangu want kiume hatokaa asome boarding school daima na milele
 
I hope we've provoked him / her enough abadilishe mawazo. Kama bado yuko na msimamo basi tena, kweli binadamu tuko tofauti.
 
Huyo Mtoto bado mdogo but Km upo busy sana unashindwa kukaa na mtoto mpeleke,mpleke maps iko juu sana kitaluma!
 
Habarini Wana JF

Nina mwanangu nataka nimpeleke shule akawe anakaa huko huko ana miaka 3 anaenda mwaka wa nne

Naomba kuzijua shule zinazokuwa zinamfundisha mtoto kingereza kizuri kwa watoto wa umri huo na watoto wanakuwa wanalelewa huko huko i mean bording

Shule iwe Dar Es Salaam na ada isiwe inazidi Milioni Moja na Nusu! Naombeni msaaada
Hiyo ada kwa boarding hupati ,nenda st Anne Marie kwa msuguri ila ada itazid bajet yko kdogo
 
Back
Top Bottom