Natafuta namna nzuri ya kuachana na mpenzi wangu aliyenifungulia kesi ya ubakaji

Aisee kwa mpare Mimi kiburi na ujeuri nilio nao nicngeweza hata kumwangalia usoni huyo kahaba
 
siwezi kusema ni wanawake but kuna binadamu wakatili sana (wengine wanaomba msamaha ukifa)
BORA UKUTANE NA SIMBA KULIKO BINADAMU MWENYE ROHO MBAYA
 
We kaka, hadi nimetoa machozi, Mungu akusaidie pole sana... Kwanza, unahitaji ushahidi kuwa ile kesi ya kwanza alikusingizia.

Nenda polepole, unaweza kuwa unamtumia sms ukiwa kazini kumuelezea namna gani unampenda na ulivyoumia aliyokufanyia. Si unasema anaomba msamaha sana? Hii inamaanisha ataendelea kujieleza kwa sms, na wewe uwe unamdodosa kwa sms, ilikuaje akakupangia njama hizo, na maswali ambayo yatakupa majibu ambayo utayatumia kama ushahidi.

Pili, mchukue mtoto ukamfanyie vipimo bila yeye kujua kama alishawahi kuingiliwa kabisa. Halafu, hifadhi majibu.

Mwisho, Mungu akufariji. Na kama kuna watu wa kukusaidia humu, wakusaidie tu. Jamani, viatu vyako ni vigumu.
Drama queen jina linatisha lkn una akili mwaya
 
Kwakuwa hamna hata mtoto na mtoto aliyenae sio wako means hata huyo sio mpenzi wako naona uamuzi ulokuwa umeuchukua mwanzoni ubaki uleule labda fuata taratb kdg washirikishe hata ndugu ikiwezkana na viongozi wa mtaa hata wa dini umuache iwe wazi maana itafka muda baba wa mtoto atarudi aendeleze goma na angali we uko na huyo kama mkeo kwakuwa alikuwa ashaanza kuonesha dharau bas tambua tabia haifi inaweza fichika tu kwa muda ila itaendelea badae
 
Nina mpenzi wangu ambae tunaishi nae toka mda tuko chuo, Huyu mpenzi tayari ana mtoto ambae alimpata akiwa Olevel.

Nilianza kukaa nae rasmi toka Niko chuo akiwa yeye na huyo mtoto wake, nikiwa na mishe zangu za kupambana mtaani. Baada ya kumaliza chuo nikawa na bajaji zangu mbili, Moja nikampa mtu, nyingine nikawa naendesha Mimi.

Mwaka jana mwanzoni TAESA wakanipa taasisi ya kwenda kufanya kazi kama Intern kwa mkoa huu huu nilipo, hivyo nikawa naenda baada ya mda wa kazi saa 11 naingia barabarani kutafuta ridhiki.

Mambo yakawa magumu kidogo kama mnavyojua utafutaji ulivyo, siku Moja huyu mpenzi aliniaga anaenda sehemu ila kufatilia hiyo sehemu hakuenda na kibaya zaidi ikatumwa meseji kutoka kwa mtu ambaye inaonekana kabisa ni mwanaume akionesha kuridhishwa na namna walivyokutana.

Baada ya kumuuliza akawa na majibu ya dharau sana, kwamba alifikia kipindi anaona siwezi kumbabaisha kwa namna yoyote ile, nilitoka nikaenda kijiweni kwangu ninapopaki bajaji baada ya kufikiria sana nikaona ninayo fanya ni ujinga, kwanza kwetu wanasikia sikia tu naishi na mwanamke ila hatujawahi kwenda Wala kwao, nalea mtoto ambae sio wangu, nimejipa gharama ya kukodi nyumba ya 150k wakati Bado sijasimama kiuchumi na Bado mtu ananisaliti na dharau juu kuliko kuendelea kukaa na kuanza kuuana, Nikaamua kuchukua begi langu na kwenda kuanza maisha mapya.

Nilikaa kama mwezi tukiwa hatuko pamoja, Kuna siku asubuhi nikiwa kijiweni kwangu nasubiri abiria akaja mke wangu na gari la Polisi, nikatiwa pingu nikasekwa kwenye gari, pamoja na kwamba nilijitahidi Ili kujua kosa Nini niliambulia kipigo.

Nafika Polisi, waliokuwa pale kituoni wakauliza, yule jamaa aliyebaka ndio huyu. Maafande walionibeba wakajibu, Ndio yeye. Nikiwa Bado nimepigwa na butwaa sijui kinachoendelea. Zikaja faili zinaonesha nilikuwa namuingilia "kumbaka" yule mtoto wa mpenzi wangu niliyekuwa nakaa nae.

Nilihamaki sana, kipindi chote huyu mpenzi wangu alikuwa analia tu. Nilikaa mahabusu siku mbili, siku ya tatu mzee wangu akawa amepata taarifa akaja, akamtafuta huyu mpenzi wangu wakawa wote. Lakini kabla ya hapo nilipata nafasi ya kuongea na mzee akiwa na afande mmoja ambao wote kwa pamoja walionesha kwamba hii kesi ni ngumu kuliko binafsi ninavyoichukulia haijalishi nimeonewa au la! Kwa namna yoyote Ile mtoto akipimwa na akathibisha basi inabidi nikatumikie serikali.

Mzee akanieleza inabidi niwe mpole kwa mpenzi wangu tuweke mambo sawa, tuondoe tofauti zetu halafu tukishakuwa sawa hii kesi itakuwa rahisi, walikaa na huyu mpenzi wangu walipokuja kwangu ilibidi niwe mpole nimuombe msamaha kama Kuna sehemu nilimkosea, dhamana ikafosiwa kikahitajika kiasi Cha pesa, walitaka pesa nyingi kidogo mzee alinieleza ila sikumbuki maana akili ilishavurugwa, ilipopatikana nikatoka nikapangiwa siku ya kuwa naripoti

Baada ya kutoka pale tukaenda nyumbani kwa mzee, akatukaliza, kwa vile alishanipa maelekezo nikawa mpole na mnyeyekevu sana, mambo yakawa sawa, kimbembe kikawa ni kufuta kesi jamaa wakakomaa, wakawa wananikomalia na yeye wakamgeuka At the end wakataka 3.5 m Ili waifute, sikuwa na pesa ikabidi niuze bajaji yangu Moja kwa hasara na baadhi ya asset zangu nikawapa na kweli wakaifuta.

Sasa hapa Niko naishi na huyu mwanamke japo kaomba msamaha sana na kuonesha kujutia kosa lake lakini akili yangu Bado inagoma, kama alidhamiria kunipa kifungo Cha Miaka 30 Sidhani kama ananitakia mema, wazazi wangu Bado hawajaniambia chochote tangu tutoke siku ya kesi Ila naona kabisa hapa natakiwa kutoka mapema

Sasa ndugu zangu natokaje hapa Ili yasijirudie yale ya kesi ya ubakaji?

Wanaume tuna mitihani sana kama sio mvumilivu unaweza ukaua
Kama hii sio chai basi itoshe kusema wewe jamaa ni mwanaume mjinga sijawahi ona Toka nizaliwe, yaani mtu ameliwa na mwanaume mwingine na ushahidi umeupata hapo hapo anakubambikia kesi ya ubakaji na bado unarudi kuishi naye? Aisee!!!
 
Back
Top Bottom