Natafuta namna nzuri ya kuachana na mpenzi wangu aliyenifungulia kesi ya ubakaji

Requal

JF-Expert Member
Jun 5, 2020
1,025
1,914
Nina mpenzi wangu ambae tunaishi nae toka mda tuko chuo, Huyu mpenzi tayari ana mtoto ambae alimpata akiwa Olevel.

Nilianza kukaa nae rasmi toka Niko chuo akiwa yeye na huyo mtoto wake, nikiwa na mishe zangu za kupambana mtaani. Baada ya kumaliza chuo nikawa na bajaji zangu mbili, Moja nikampa mtu, nyingine nikawa naendesha Mimi.

Mwaka jana mwanzoni TAESA wakanipa taasisi ya kwenda kufanya kazi kama Intern kwa mkoa huu huu nilipo, hivyo nikawa naenda baada ya mda wa kazi saa 11 naingia barabarani kutafuta ridhiki.

Mambo yakawa magumu kidogo kama mnavyojua utafutaji ulivyo, siku Moja huyu mpenzi aliniaga anaenda sehemu ila kufatilia hiyo sehemu hakuenda na kibaya zaidi ikatumwa meseji kutoka kwa mtu ambaye inaonekana kabisa ni mwanaume akionesha kuridhishwa na namna walivyokutana.

Baada ya kumuuliza akawa na majibu ya dharau sana, kwamba alifikia kipindi anaona siwezi kumbabaisha kwa namna yoyote ile, nilitoka nikaenda kijiweni kwangu ninapopaki bajaji baada ya kufikiria sana nikaona ninayo fanya ni ujinga, kwanza kwetu wanasikia sikia tu naishi na mwanamke ila hatujawahi kwenda Wala kwao, nalea mtoto ambae sio wangu, nimejipa gharama ya kukodi nyumba ya 150k wakati Bado sijasimama kiuchumi na Bado mtu ananisaliti na dharau juu kuliko kuendelea kukaa na kuanza kuuana, Nikaamua kuchukua begi langu na kwenda kuanza maisha mapya.

Nilikaa kama mwezi tukiwa hatuko pamoja, Kuna siku asubuhi nikiwa kijiweni kwangu nasubiri abiria akaja mke wangu na gari la Polisi, nikatiwa pingu nikasekwa kwenye gari, pamoja na kwamba nilijitahidi Ili kujua kosa Nini niliambulia kipigo.

Nafika Polisi, waliokuwa pale kituoni wakauliza, yule jamaa aliyebaka ndio huyu. Maafande walionibeba wakajibu, Ndio yeye. Nikiwa Bado nimepigwa na butwaa sijui kinachoendelea. Zikaja faili zinaonesha nilikuwa namuingilia "kumbaka" yule mtoto wa mpenzi wangu niliyekuwa nakaa nae.

Nilihamaki sana, kipindi chote huyu mpenzi wangu alikuwa analia tu. Nilikaa mahabusu siku mbili, siku ya tatu mzee wangu akawa amepata taarifa akaja, akamtafuta huyu mpenzi wangu wakawa wote. Lakini kabla ya hapo nilipata nafasi ya kuongea na mzee akiwa na afande mmoja ambao wote kwa pamoja walionesha kwamba hii kesi ni ngumu kuliko binafsi ninavyoichukulia haijalishi nimeonewa au la! Kwa namna yoyote Ile mtoto akipimwa na akathibisha basi inabidi nikatumikie serikali.

Mzee akanieleza inabidi niwe mpole kwa mpenzi wangu tuweke mambo sawa, tuondoe tofauti zetu halafu tukishakuwa sawa hii kesi itakuwa rahisi, walikaa na huyu mpenzi wangu walipokuja kwangu ilibidi niwe mpole nimuombe msamaha kama Kuna sehemu nilimkosea, dhamana ikafosiwa kikahitajika kiasi Cha pesa, walitaka pesa nyingi kidogo mzee alinieleza ila sikumbuki maana akili ilishavurugwa, ilipopatikana nikatoka nikapangiwa siku ya kuwa naripoti

Baada ya kutoka pale tukaenda nyumbani kwa mzee, akatukaliza, kwa vile alishanipa maelekezo nikawa mpole na mnyeyekevu sana, mambo yakawa sawa, kimbembe kikawa ni kufuta kesi jamaa wakakomaa, wakawa wananikomalia na yeye wakamgeuka At the end wakataka 3.5 m Ili waifute, sikuwa na pesa ikabidi niuze bajaji yangu Moja kwa hasara na baadhi ya asset zangu nikawapa na kweli wakaifuta.

Sasa hapa Niko naishi na huyu mwanamke japo kaomba msamaha sana na kuonesha kujutia kosa lake lakini akili yangu Bado inagoma, kama alidhamiria kunipa kifungo Cha Miaka 30 Sidhani kama ananitakia mema, wazazi wangu Bado hawajaniambia chochote tangu tutoke siku ya kesi Ila naona kabisa hapa natakiwa kutoka mapema

Sasa ndugu zangu natokaje hapa Ili yasijirudie yale ya kesi ya ubakaji?

Wanaume tuna mitihani sana kama sio mvumilivu unaweza ukaua
 
Nina mpenzi wangu ambae tunaishi nae toka mda tuko chuo, Huyu mpenzi tayari ana mtoto ambae alimpata akiwa Olevel.

Nilianza kukaa nae rasmi toka Niko chuo akiwa yeye na huyo mtoto wake, nikiwa na mishe zangu za kupambana mtaani. Baada ya kumaliza chuo nikawa na bajaji zangu mbili, Moja nikampa mtu, nyingine nikawa naendesha Mimi.
Dah! Hawa viumbe ilitupasa tuwaepuke ila utelezi huu unatugharimu!
 
Mkuu, unaendelea kuishi na mwanamke aliyekufanyia hayo? Aysee, kweli binadamu tumetofautiana sana! Na huna mtoto naye!! Aysee, nenda serikali za mitaa, tafuta mwanasheria, tafuta viongozi wa dini! Kote huko uende na barua kuwa UMEMUACHA HUYO MWANAMKE uache na nakala kama ushahidi!! Ukiendelea kukaza fuvu atakuua!! Acha ujinga wewe
 
Mkuu, unaendelea kuishi na mwanamke aliyekufanyia hayo? Aysee, kweli binadamu tumetofautiana sana! Na huna mtoto naye!! Aysee, nenda serikali za mitaa, tafuta mwanasheria, tafuta viongozi wa dini! Kote huko uende na barua kuwa UMEMUACHA HUYO MWANAMKE uache na nakala kama ushahidi!! Ukiendelea kukaza fuvu atakuua!! Acha ujinga wewe
Kaka umesoma vizuri! Hapa naumiza kichwa namna gani naweza kumuacha nisije kupotezwa tena kwa kesi ya ubakaji
 
Hana wazazi huyo binti?? Mpeleke kwao mwambie unataka ukapaone mpange harusi huku kabla panga na nduguzo wakufungashie virago vyako vyote virudishwe kwenu kisha ukifika ukweni ongea nia yako ila utamwambia mwenzio hutaweza lala ukweni ukiweza kuwapa tu kisogo break ya kwanza ni mkoa mwengine kwanduguzo badili na namba ya sim sajili hata kwa kitambulisho cha mama yako anza upya.
 
hana wazazi huyo binti?? mpeleke kwao mwambie unataka ukapaone mpange harusi huku kabla panga na nduguzo wakufungashie virago vyako vyote virudishwe kwenu kisha ukifika ukweni ongea nia yako ila utamwambia mwenzio hutaweza lala ukweni ukiweza kuwapa tu kisogo break ya kwanza ni mkoa mwengine kwanduguzo badili na namba ya sim sajili hata kwa kitambulisho cha mama yako anza upya.
Ikiwa hivi hawezi tena kwenda kufungua kesi kama ya mwanzo? Changamoto unaweza kupigwa Miaka bila kuangalia ushahidi wa kutosha
 
duh, kuna wanawake wana roho ngumu mno.

Mchezee mchezo wake yeye mwenyewe. Jaribu kuanzisha topic ya yeye kukufungulia kesi ya uongo lakini hakikisha unarekodi kila analosema akiwa anakiri kuwa alikubambikia kesi.

Ukimaliza sasa mwambie wewe na yeye basi na akithubutu kurudia tena mchezo wake wa mwanzo una kila ushahidi na utamshitaki yeye.

Hama hapo mnapokaa na hakikisha hapajui utakapahamia, anza maisha mapya.
 
Ikiwa hivi hawezi tena kwenda kufungua kesi kama ya mwanzo? Changamoto unapiga Miaka bila kuangalia ushahidi wa kutosha
hata akikufungulia atakupatia wapi?? anyway hujaamua kumuacha huyo nenda serikali ya mtaa andaa nakala kwa nduguze nakala kwanduguzo na rafiki zenu og baki nayo itoe kopi tembea nayo mfukoni kwamba hauna mahusiano naye na kitakachokupata yeye ndie mshtakiwa namba moja
 
We kaka, hadi nimetoa machozi, Mungu akusaidie pole sana... Kwanza, unahitaji ushahidi kuwa ile kesi ya kwanza alikusingizia.

Nenda polepole, unaweza kuwa unamtumia sms ukiwa kazini kumuelezea namna gani unampenda na ulivyoumia aliyokufanyia. Si unasema anaomba msamaha sana? Hii inamaanisha ataendelea kujieleza kwa sms, na wewe uwe unamdodosa kwa sms, ilikuaje akakupangia njama hizo, na maswali ambayo yatakupa majibu ambayo utayatumia kama ushahidi.

Pili, mchukue mtoto ukamfanyie vipimo bila yeye kujua kama alishawahi kuingiliwa kabisa. Halafu, hifadhi majibu.

Mwisho, Mungu akufariji. Na kama kuna watu wa kukusaidia humu, wakusaidie tu. Jamani, viatu vyako ni vigumu.
 
Back
Top Bottom