Natafuta Fundi mwenye uwezo wa kufuta DPF kwenye Mazda

sasa mtusaidiaje tusiojua mambo ya magari embu twendeni sawa jamani hiyo DPF ndio kitu gani hicho hata kwa picha tu tuone.!
DPF ni Diesel Particulate Filter
Kwa lugha rahisi ni chujio la hewa gesi (zile za exhaust) ili kupunguza uchafuzi wa mazingira. Kwa Ulaya na Marekani ni requirement/ni lazima kwa sasa ili kulinda mazingira. Nchi za Afrika bado hatuna masharti hayo.
Kinachotokea yale masizi yakijaa kwenye chujio, hewa/gesi zenye joto zinakuwa hazipiti vizuri na gari haipumui vizuri. Joto linaweza kurudi kwenye engine likaharinu turbo hata cylinder head.
Kuzuia au kuchelewesha hilo ndio kitu kinaitwa DPF regeneration, kwa kifupi ni kuisafisha DPF kwa njia ya kuipasha joto gari ili iyeyushe zile taka/masizi/uchafu kwenye chujio. Gari za Diesel za miaka hii zinataka gari iwe inatembezwa umbali mrefu hata mara moja au mbili kwa mwezi ili kuchoma hizo ashes.
Kuna mifumo mingine kwa ajili hiyo pia kama vile EGR, ADBLUE ila kwenye mazda ni dpf na egr tu
 
Umeelezea vizuri sana mkuu
 
Back
Top Bottom