Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 594
- 1,165
Wenzetu hawalali kila siku wanapenda kujua siri za Sayari zilizopo karibu na Dunia yetu, Chombo kinachohusika na masuala ya masafa marefu ya Angani Nasa wanafanikiwa kuweka rekodi ya Dunia kuwa chombo cha kwanza kufika kwenye sayari ya jua.
Kupitia chombo chao cha Uchunguzi kinaitwa Parker Solar Probe ambapo kimefanya safari ya kwenda kwenye sayari ya jua kufanya uchunguzi chenye uwezo wa kuhimili | kuvumilia Joto kali la jua pamoja na mionzi mikali inayotoka kwenye sayari hiyo ya jua.
Chombo icho kiliruka umbali wa maili milioni 3.8 sawa na kilomita milioni 6.1 kutoka usawa wa jua, wataalamu hao toka Nasa wanasema chombo kwa sasa kimepoteza Mawasiliano kwa kuwa kiko karibu na jua sehemu ambayo ina joto kali sana hivyo wanasubiri ishara zozote toka kwenye chombo hicho mpaka kufikia Desemba 27 kujua kama kimenusurika kuteketea na mionzi ya jua.
Lengo lao ni kuunda chombo Ambacho kitakua na uwezo wa kufika kwenye jua na kuweza kusaidia kwenye kufanya tafiti mbalimbali la jinsi ya kujua Jua linavyofanya kazi Je wanafanikiwa ngoja tuone ?