Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 75,016
- 156,385
Kuna mdau kauliza swali kuhusu Vimondo kikiwemo na kile kinachopatikana Jijini Mbeya katika wilaya ya Mbozi. Nitajibu kwa ufupi tu, ili na wengine wapate kuelewa kuhusu Vimondo na chimbuko lake.
Ipo hivii.........kijiografia chimbuko la vimondo vingi vilivyopo huko angani (outer space) vimetoka kwenye jua. Yaani lile joto kali lililopo kwenye jua ndio husababisha mawe kutoka kwenye mzingo wake kuelekea kwenye baadhi ya Sayari.
Na mengi ya mawe hayo hukutana na ukanda wa baridi kali na kuganda na mwisho wa siku kuyeyuka bila kuleta madhara kwenye sayari zinazolizunguka jua ikiwemo dunia yetu. Bila ukanda huo wenye baridi kali sana (coldest layer) basi mawe hayo ya moto yangeleta athari kubwa sana huku Duniani.
Tambua kwamba, vimondo vingi yaani (asteroids) vipo katika ya Sayari ya Jupita na Mars. Na hapo ndipo vilipotengeneza mkanda ambao kijiografia unaitwa ' main asteroids belt'. Na vingine hupenya zaidi kusogea kwenye ukanda wa ndani kwenye usawa wa Sayari tatu za mwanzo kwenye mfumo wa jua kwa maana ya Mercury , Venus pamoja na Dunia yetu hii.
Ikumbukwe pia hata hicho kimondo kilichopo Mbozi katika mkoa wa Mbeya ni kwamba, mnamo mwaka 1930 wanasayansi walikigundua Kimondo chenye ukubwa wa tani 16 ( metric tons ) Kimondo kile ni moja ya vimondo maarufu sana duniani kwa ukubwa na uzito vilivyowahi kuanguka na kugusa uso wa dunia yetu hii. Lakini pia kwa asilimia zaidi 99% ya Vimondo vilivyowahi kufika kwenye ardhi ya Dunia yetu hii ni Chuma.
NB: Kimondo kilichopo Mbeya hakikuanguka mwaka 1930, bali kiliangua miaka mingi tu huko nyuma. isipokuwa mnamo mwaka 1930 wanasayansi ndipo walipoanza kukichunguza. Asante!
Nawasilisha.