Napoleon

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,746
Napoleon Bonaperte kwa jina linginge Napoleone di Boungartealizaliwa 15 August 1769 na alifariki 05 May, 1821. Alikuwa mwanajeshi wa Kifaransa na pia kiongozi wa kisiasa aliejipatia umaarufu wakati wa mapinduzi wa Kifaransa na aliendesha kampeni nyingi zilizoleta mafanikio wakati wa vita vya mapinduzi. Akiwa Napoleon I, alikuwa kiongozi wa Ufaransa tangia 1804 mpaka 1814 na baadae tena 1815. Napoleon alitawala Ulaya na dunia kwa mambo mengi kwa miaka mingi akiwa anaiongoza Ufaransa kutoka vita nyingi ziliohusishwa na Vita vya Napoleon. Alishinda nyingi ya vita hivi na alijijengea ufalme mkubwa uliotawala bara la Ulaya kabla ya kushindwa 1815. Napoleon ni mmoja wa makamanda wa kuaminika ambae mbinu zake za kivita mpaka hii leo zinafundishwa katika mafunzo ya kijeshi dunia nzima. Na mpaka leo ni mwanasiasa anaeheshimika zaidi yatika historia ya binadamu.
800px-Jacques-Louis_David_-_The_Emperor_Napoleon_in_His_Study_at_the_Tuileries_-_Google_Art_Project.jpg

Napoleon alikua na nguvu na ushawishi mkubwa kwenye dunia iliyokuwa inaendelea na alileta mabadiliko mengi katika tawala nyingi alizoziteka na kuzitawala nchi kama Switzerland, Italy na Ujerumani. Alileta sera za mageuzi Ufaransa na nchi zote za Magharibi. Mafanikio yake ya kisiasa ya mwisho yaliyoitwa Napoleon Code, yanaushawishi katika mitaala mingi ya sheria katika nchi zaidi ya 70 duniani. Mwanasheria wa Kiingereza alieitwa Anderw Roberts anasema "Mawazo ambayo yanaongoza katika dunia ya sasa juu ya usawa, utawala kutokana na uwezo (merits), sheria za umiliki wa nyumba, uhuru wa kuabudu, usawa wa elimu, maswala ya pesa na mengine mengi yamekuwa shinikizwa, kuwekwa sawa na kusambazwa ki jiografia na Napoleon". Huko kwiningine alisisitiza utawala unaojitegemea kwa sehemu moja (local administration). Napoleon aliona umuhimu wa sayansi na sanaa katika maendeleo na pia alipiga vita sana ukabaila kumiliki mashamba (feudalism), hii ilipelekea mvutano wa kimaslahi kati ya Utawala wa Roma (Roman Empire).

Napoleon alizaliwa Corsica na alisaidia mapinduzi ya Ufaransa akiwa mwanajeshiana alijatahidi sana kusambaza mawazo ya kuutoa utawala wa kifalme katika sehemu yake aliyozaliwa Corsica. Alipanda vyeo haraka katika na kufikia cheo cha kamanda wakati wa mapinduzi baada ya kuwashinda wanajeshi waliokuwa upande wa mfalme. Alipokuwa na miaka 26 alianza kampeni ya kijeshi dhidi ya Australia na marafiki zake kama Itali, alijipatia sifa za ushindi wa ushawishi na kuweza kujishindia Penisula ya Itali kwatika mwaka mmoja, alikuja kuwa shujaa wa nchi yake. 1798 aliongoza jeshi lake katika safari ya Egypt na ilifanya mageuzi katika nguvu za siasa. Alipanga mashambulizi ya kijeshi November 1799 na kuwa Kiongozi wa nchi inayoongozwa na Utawala wa watu (Republican). Ushindi wake ulimpa ari ya kufanya mengi zaidi, 1804 alikuwa mtawala wa kwanza wa Ufaransa. Ubishi huu wa kisiasa ulimaanisha Wafaransa walikabiliwa na serikali ya tatu ya mseto mwaka 1895, Napoleon aliifunga hii serikali ya mseto kwa ushindi wa Ulm Campaign na vita ya watawala watatu wa Ulaya iliyojulikana kama Battle of Auterlitz iliyopelekea kuanguka kwa Utawala Mtatakatifu wa Roma (Holy Roman Empire). Mnamo mwaka 1806 serikali ya mseto ilianza kupigana na Napoleon Prussia ilianza kuwa na wasiwasi juu ya kukua kwa nguvu ya Ufaransa katika bara la ulaya. Haikuchukua muda kwa Napoleon kuushinda utawala wa Prussia katika vita ya Jeana na Austerlitz, aliongoza Jeshi la Umoja (Grand Army) ndani ya Ulaya Mashariki na kuishambulia Urusi June 1807 kwenye vita ya Friedland, ushindi wa Napoleon ulipelekea kusainiwa kwa mkataba wa Treaties of Tilsit. Mkataba huu ulikwa alama kubwa ya ushindi kwa Ufaransa lakini haukuiwekea amani bara la ulaya. Miaka miwili baadae Autrians walianza kuwapiga Wafaransa. Napoleon aliongeza nguvu ya jeshi lake na kupelekea ushindi kwenye vita ya Wagram, vita hii Waingereza waliungana na Wautsria kupigana na Ufaransa.

images

Napoleon alihamasika kuendeleza mawazo yake katika bara lote la ulaya na hii alifikiria kukomesha bidhaa za Uingereza ulaya itasaidia kuwashawishi Waingereza waondokane na utawala wa kifalme. Alivamia Spain, Portugal na pamoja na visiwa vya Gibraltar na alimtangaza kaka yake Joseph kuwa Mfalme wa Spain mwaka 1808. Spain na Portugal ziliungana na Mwingereza na kuanza vita ya Peninsular iliyodumu kwa miaka sita, vita hii ilitawaliwa na mashambulizi ya msituni. Ushindi mkubwa uliopatikanana ulimaanisha Napoleon alikua na maamuzi juu ya Spain, Portugal na Uingereza.

Utawala wa ulaya (system) ulisababisha vita vya kidiplomasia kati ya Ufaransa na marafiki zake kama Urusi ambayo haikuwa tayari kupoteza biashara. Warusi walipinga utawala huo na kumchokoza Napoleon kuingia vitani. Wafaransa walihamasisha shambulizi kwa Warusi kiangazi cha 1812. Vita hii ilipelekea kuanguka kwa jeshi la wananchi na machafuko makubwa yalitokea katika miji ya Urusi. Maadui wa Napoleon waliungana.

Maadui wa Napoleon walikuwa pamoja na Austria, Portugal, Spain, Russia na jeshi lao lilimshinda Napoleon katika viat ya Leipzing October 1813. Jeshi la adui liliingia Ufaransa na kuteka Paris April 1814, hii ilipelekea Napoleon kusalim amri mwezi April mwaka huo. Alikimbilia katika kisiwa cha Elba karibu na Rome na utawala wa kifalme wa Bourbon ulirudishwa madarakani. Napoleon alitoka katika kisiwa cha Elba mwaka 1815 na kuchukua tena madaraka ya Ufaransa, alianza mashambulizi mapya na wakati huu maadui wake waliungana na Waingereza na kumshambulia Napoleon katika shambulio la vita ya saba ya mseto. Vita hii pia iliitwa siku 100 za Napoleon ambazo alishindwa katika Vita ya Waterloo. Mpaka leo waingereza wanamsemo "this is my Waterloo" wakimaanisha anguko langu

Maisha ya mwanzo ya Napoleon.
Napoleon alizaliwa 15/08/1769, wazazi wake wakiwa Carlo Maria di Buonaparte na Maria Letizia Ramolino, katika kijiji cha asili yao cha Casa Buonapartein Ajaccio, mji mkuu wa kisiwa cha Corsica, akiwa mtoto wa nne kuzaliwa na watatu wa kiume. Mwaka aliozaliwa Napoleon ulikuwa mwaka mmoja tangu Corsica iwe chini ya utawala wa Ufaransa kutoka Jamhuri ya Genoa. Alibatizwa kama Napoleone di Buonaparte, alipewa jina la baba mkubwa ambae alikufa akiwa mtoto nae aliitwa Napoleon.
Ukoo wa Corsican Buonapartes ulitokea katika jamii ndogo ya Itali yenye heshima ambayo asili yake ilikuwa Tuscan, walikwenda Corsica wakitokea Liguria mnamo karne ya 16.

Baba yake Mheshimiwa Carlo Bounaparte alikua mwanasheria na yeye ndie alikuwa mwakilishi wa mfalme Louis XVI katika mahakama za Corsica mwaka 1777. Mtu aliekuwa na ushawishi mkubwa katika maisha ya utoto ya Napoleon alikuwa mama yake, Letizia Ramolino, ambae alimwadhibu na kuweka nidhamu kwa mtoto mkorofi Napoleon. Bibi mzaa mama wa Napoleon aliolewa tena Switzelarnd kwenye ndoa yake ya pili na mjomba wa Napoleon ambae alikua baadae cardinali Joseph Fesch, alikuwa ndie mwangalizi wa familia ya Bonaparte baadae.

Kutokana na familia aliyotoka Napoleon alikua na nafasi nzuri ya kusoma kuliko uwezo wa kawaida wa watu wa Corsican kwa wakati huo. January 1779 aliandikishwa kwenye shule ya dini ya Autun. May mwaka huo aliandikishwa kwenye shule ya maafisa wa kijeshi cha Brienne-le-Chateau. Lugha yake ya kwanza ikiwa Corscan, Kifaransa chake kilikua na laufidh ya Corsca na hakuweza kuandika neno French vizuri. Wanafunzi wenzake walimcheka kwa laufidh yake. Kutokana na hali hiyo aliamua kusoma sana na kuwa na muda mchache wa kuongea na wenzake. Siku ya mtihani mtahini wake aligundua uwezo wake mkubwa katika hesabu pia alielewa vyema historia na jografia na mtahini alisema "huyu kijana atakua baharia mzuri".

Alipomaliza masomo yake Brienne mwaka 1784, Napoleon alijiunga na chuo cha maafisa wa jeshi cha Ecole Militire mjini Paris. Alifundishwa kuwa ofisa wa mashambulizi ya silaha, baada ya kifocha baba yake ambacho kilipunguza uwezo wa kifedha na ilibidi amalize shule katika mwaka mmoja badaya ya miaka miwili. Alikua na mtu wa kwanza kutoka Corsican kumaliza Ecole Militaire na mtahini wake alikua mwanasayansi Pierre-Simon Laplace.

Maisha ya awali kama mwanajeshi.
Baada ya kuhitimu September 1785 alipangiwa kazi ya second lieutenant katika kikosi cha mashambulizi ya silaha na alifanya kazi mjini Valence na Auzonne mpaka wakati wa mapinduzi mwaka 1789, alichukua likizo ya karibia miaka miwili kati ya miji ya Corsica na Paris katika kipindi hicho. Kipindi hicho alikua raia mashuhuri wa Corsica na alimwandikia kiongozi wa wa Pasquale Paoli May 1789 kua "kama taifa nililozaliwa linateketea na wanajeshi wetu 30,000 wametapikwa kwenye pwani za bahari wakizika uhuru kwenye mawimbi ya damu. Hii hali yakusikitisha imenistua sana.

Alitumia miaka ya mwanzo ya mapinduzi kupigana na watu wa aina tatu, wanamapinduzi, waliompenda mfalme na watu wa Corsica. Alimuunga mkono Jacobin ambae aliamini utawala wa wengi (republican), waliratibu vilabu kwa wananchi wa Corsica na aliwapa amri askari wa kujitolea wa silaha. Alipandishwa cheo kuwa Kaptain katika jeshi la kawaida japokuwa hakuwepo jeshini na hali hiyo ilileta ubishi na watu walipinga sana kwa vurugu dhidi ya jeshi la Ufaransa mjini Corsica.

Alirudi Corsica ambako alitofautiana na Paoli, ambae aliamua kujitenga na Ufaransa na kuharibu mashambulizi ya Ufaransa ya kisiwa cha Sardini katika La Maddalena. Familia ya Bonaparte ilikimbilia Ufaransa June 1793 kwasababu ya kutofautiana na Paoli.

800px-Napoleon_-_2.jpg

Napoleon akiwa Second Lieutenant wa Corsica, mwenye umri wa miaka 23.

Shambuli ka kuteka Toulon.
Mnamo July 1793, Bonaparte alichapisha kipeperushi (pamphlet) kilichoitwa Le souper de Beucaire (Supper at Beucaire), kipeperushi hiki kilisaidia kuungwa mkono na Augustin Robespierre ambae alikua mdogo wa mwanamapinduzi Maximillien Robespierre. Kwa msaada wa mtu mwingine wa Corsica Antoine Christophe Saliceti, Bonaparte alipewa cheo cha kamanda wa askari wenye silaha wa jeshi la wananchi katika kuteka Toulon.

Alijipatia mbinu ya kuteka kilima ambapo wanajeshi wa jeshi la wananchi wenye bunduki walizunguka bandari ya mji na hii ilipelekea majeshi ya Waingereza kukimbia. Pigano hili lilipelekea kuchukua mji na Bonaparte alijeruhiwa pajani. Alipandishwa cheo kuwa brigadia generali akiwa na miaka 24 na hii ilipelekea macho ya Kikao cha Kamati ya Usalama kumteua kuwa Kiongozi wa jeshi la silaha la Ufaransa katika jeshi la Italia.

Napoleon alitumia muda kama inspekta wa pwani ya Mediterranea karibu na Marseille ambapo alisubiri kwa kuhakikishwa kwa post yake ya Jeshi la Italy. Alibuni mbinu ya kushambulia Ufalme wa Sardinia kama mpango wa Ufaransa dhidi ya vita ya kwanza ya majeshi ya falme za ulaya kuzuia mapinduzi ya Ufaransa. Augustin Robespierre na Saliceti walikua tayari wanasubiri amri ya kiongozi wa silaha.

Jeshi la Ufaransa liliendelea na mashambulizi ya Vita ya Saorgio Aprili 1704 kwa mipango ya Bonaparte na waliendelea kuteka Ormea katika milima. Kutoka Ormea walielekea magharibi na walilizunguka jeshi la Austro-Sardinian katika Saorge. Baada ya kampeni hii, Augustin Robespierre alimpeleka Bonaparte katika Jamhuri ya Genoa kuangalia nini nia ya serikali kuhusu Ufaransa.

Napoleon_%C3%A0_Toulon_par_Edouard_Detaille.jpg

Napoleon katika shambulizi la kuteka Toulon akiwa na umri wa miaka 24

Vita ya wanamapinduzi na wapenda ufalme mjini Paris (13 Vendemiaire)
Kuna mazungumzo yanayoendelea yasemayo Bonaparte alipewa kifungo cha ndani ya nyumba kwa uhusiano wake na wakina Robespierres kufuatia kushindwa kwao kwenye shambulio la Thermidorian July 1794, lakini katibu wa Napoleion aitwae Bourrienne, anasema maneno ya wivu yaliyohusu jeshi la Alps na jeshi la Italy ambalo Napoleon alilifanyia kazi wakati huo. Bonaparte aliandika barua yenye maelezo ya kutoa machozi katika kujitetea kwake kwa afisa mkuu wa serikali na hii ilipelekea kufutiwa makosa yake.
Aliachiliwa katika wiki mbili na kutokana na ufundi wake wa kivita, aliombwa aanze mipango ya mashambulizi ya Italia kama moja ya mashambulizi ya Ufaransa kwa Austria. Pia alishiriki katika safari ya kurudisha majeshi Corsica kutoka Uingereza, lakini Wafaransa walishambuliwa na Jeshi la Mfalme la Uingereza.

Mwaka 1795, Bonaparte alikuwa engaged kwa Desiree Clary, binti wa Francois Clary. Dada wa Desiree aitwae Julie Clary alishaolewa na kaka yake Napoleon aitwae Joseph. April 1795, alipewa cheo cha Ofisa wa Magharibi, ambacho kilihusisha vita ya Vendee hii ilikuwa vita ya wenyewe kwa wenyewe na wapenda ufalme. Post hii ilikua ya chini kulilo ofisa wa silaha na Napoleon alidai afya yake si nzuri.

Queen_desideria_by_locati-2.jpeg

Desiree Clary

Alihamishwa kwenye idara ya kusoma ramani na Kamati ya Usalama wa Taifa na alifikiriwa kwenda kufanya kazi kwa Sultan wa Constantinople (Turkey). Katika kipindi hiki aliandika kitabu cha mapenzi kilichoitwa Clisson et Eugenie, kilihusu askari na mpenzi wake, kwa uhalisia kilihusu mahusiano yake binafsi na Desiree. Mnamo September 15, Bonaparte aliondolewa katika orodha ya magenerali kutokana na kukaidi kwake kupigana vita ya Vendee, nguvu zake za kijeshi zilipunguzwa pia na uwezo wake wa kifedha.

Mnamo tarehe 03/10/1795 majeshi ya mfalme yalitangaza kukaidi maamuzi ya National Convention hili lilikua baraza la muda la kuongoza serikali baada ya mapinduzi na kiongozi wake alikua Paul Barras. Kiongozi wa Thermidorian alijua uwezo wa Bonaparte na alimpa amri ya kuvamia jumba la kifalme la Tuileries kulinda mapinduzi. Mauaji makubwa ya askari wa mfalme wa jeshi la Swiss pale na miaka mitatu baadae alitoa maelezo kwamba silaha ndio ilikua ulinzi.
]
Alitoa amri wa afisa wa kikosi cha farasi alieitwa Joachim Murat kutwaa silaha kubwa za kijeshi na kuzitumia kwenye mashambulizi 05/10/1795-13/10/1795 katika kalenda ya Ufaransa. Askari 1,400 wa mfalme waliuwawa katika mashambulizi haya na wengine waliobakia walikimbia. Alitangaza mji kwa cannon (a whiff of grapeshot) kutokana na maelezo ya wanahistoria wa karne ya 19 kama Thomas Carlyle katika maelezo yake HISTORIA YA MAPINDUZI YA UFARANSA.

Ushindi dhidi ya majeshi ya mfalme ulizima mawazo ya kubadilika kwa utawala na ulimpatia Bonaparte umaarufu wa ghafla pamoja na utajiri pia uongozi katika serikali mpya. Murat alimuoa mmoja wa dada wa Napoleon na akawa shemeji yake; pia alitumikia chini ya Napoleon kama mmoja wa majenerali. Bonaparte alipandishwa cheo kuwa kamanda wa majeshi ndani ya jeshi la Itali. Wiki chache baada ya hapo alikuwa kwenye mapenzi na Josephine de Beauharnais, aliekuwa mpenzi wa Barras kabla. Walioana 09 March 1796 kwa sherehe za kiserikali.

13Vend%C3%A9miaire.jpg

Mashambulizi ya silaha kwenye kanisa la Saint Roche Paris wakati wa 13 Venemiaire

Marie Josèphe Rose Tascher de La Pagerie alishaolewa ndoa ya kwanza na Francois Beauhanais na kujaliwa kupata watoto wawili kabla hajakutana na Napoleon. Beauhanais alikua tajiri sana lakini ndoa yao na Marie Josephe haikua na mapenzi, na hii ilipelekea kuachana. Marie Josephe alikuwa mkubwa kwa Napoleon kwa miaka sita.

Ridpath-Josephine_de_Beauharnais.jpg

Siku mbili baada ya ndoa, Bonaparte aliondoka Paris kwenda kwenye kazi yake kama kamanda wa jeshi la Iltali. Alikwenda kwa ari zote za kulipiga jeshi la Piedmont kabla ya rafiki zao Austria hawajaingia. Katika mfululizo wa mafanikio wakati wa shambulio la Montenotte, alipiga jeshi la Piedmont nje ya vita katika wiki mbili. Wafaransa baadae walianza kuwapiga Austria kwa muda uliobakia, ushindi huu ulijulikana kama mateko ya Mantua.
Austria walipiga mashambulizi mengi kwa Wafaransa lakini chini ya uongozi wa Napoleon washinda kwa mfululizo wa mapigano kutoka Castiglione, Bassano, Arcole na Rivoli na hii ilipelekea kuanguka kwa nafasi ya Austria nchini Itali. Askari 14,000 wa Australia walikufa na wafaransa walipoteza askari 5,000.

Kilichofuatia Wafaransa walivamia nyumba ya Habsburg, hii ilikua nyumba ya kifalme iliyosifika katika bara lote la ulaya. Majeshi ya Ufaransa yalianza Kusini mwa Ujerumani wakati huo walishindwa na Archduke Charles katika mwaka 1796, Archduke alisogeza majeshi kulinda mji wa Vienna baada ya kujua habari za Napoleon na aliyoyafanya Paris. Mkutano wa makamanda hawa wawili, Napoleon alirudisha majeshi ya Archduke nyuma na kuendelea mpaka katikati ya nchi ya Austria baada ya kushinda vita ya Tarvis mnamo March 1797. Waustria walipewa onyo na Wafaransa kuwa kutoka Leoben mpaka Vienna umbali wa takriban km 100 na waliamua kutafuta suluhu kwa njia ya amani. Ushindi wa Leoben ulifuatiwa na ushindi kamili Treaty of Campo Formio na hii iliipa Ufaransa nguvu ya kumiliki sehemu kubwa ya Kaskazini mwa Itali na nchi nyingine za chini. Ufaransa ilichukua uhuru wa nchi hizo uliodumu kwa miaka karibu 1,100. Pia aliruhusu farasi wake kuharibu farasi wanne ambao walikua mapambo ya fahari yaliyoitwa Horses of Saint Mark, farasi hao wa mapambo walitengenezwa kwa shaba.

Uwezo wake wa kijeshi kukabiliana na uhalisia wa dunia ilivyoendelea ulimwezesha kupata ushindi, kama vile jeshi la silaha kutembea kama msaada wa jeshi la miguu. Baadae kwenye wakati wa uhai wake alisikika akisema "Nimepigana vita sitini na sijajifunza kitu ambacho sikijui kuanzia mwanzo. Angalia Caesar; alipigana vita ya kwanza kama ya mwisho".
Bonaarte alipigana vita kwa kuzungusha majeshi yake kwenye kiungo cha majeshi ya adui na hii ilimaliza nguvu za maadui zake. Kama hakutumia njia yake maarufu ya kuwazunguka maadui zake na kuwashambulia katika pande zote mbili, aliingia kati kati ya aadui na kushamshambulia katika pande zote au aliharibu kiungo cha jeshi la aadui na kulinguka kupigana mpaka adui akimbie. Katika kampeni ya jeshi la Bonaparte alikamata wafungwa 150,000 wa kivita, silaha 540 na bendera 170 kama ishara ya ushindi. Jeshi la Ufaransa lilipigana na kushinda mapigano ya makubaliano kupitia njia za silaha, ufundi na ubunifu wa Bonaparte.

Wakati wa kampeni, Bonaparte alikuja kuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za Ufaransa. Alianzisha magazeti mawili: moja kwa wanajeshi na lingine lilisambazwa Ufaransa. Waliopenda utawala wa kifalme walimshambulia Bonaparte kwa kuishambulia Itali na walitahadharisha kuwa atakuja kuwa dikteta. Inasemekana Jeshi la Napoleon liliondoka na pesa zinazofikiriwa $45 million zikiwa pesa za Itali wakati wa kampeni kule pia $12 million katika vito vya thamani, juu ya hayo majeshi yake yaliondoka na picha za kuchora na sanamu(paintings na sculptures). Bonaparte alimtuma Generali Pierre Augereau kwenda Paris kuongoza nguvu za kijeshi za kupindua madaraka na kumrudisha mfalme hii ilitokea 04 September hii iliitwa Jaribio la 18 Fructidor. Ilibidi Barras na watu wengine wa Jamhuri waongoze tena lakini kwa kumtegemea Bonaparte ambae alifanikisha suluhisho la amani na Austria. Katika makubaliano hayo walimpata mwakilishi wa kifalme wa Austria kuwa mwakilishi katika Jamhuri ya Ufaransa na makubaliano hayo yaliitwa. Napolion alirudi Paris kwa mapokezi ya kishujaa na alikutana na waziri Talleyrand aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na alikuwa na nguvu serikalini kama Emperor Napoleon na wawili hao walianza mipango ya kuishambuila Uingereza.

Safari ya kuelekea Egypt.
Mpango wa Ufaransa juu ya Egypt na Syria.

Baada ya mipango ya miezi miwili, Bonaparte aliamua kuwa Jeshi la Ufaransa halikua na nguvu ya kutosha kupigana na Jeshi la maji la Falme ya Uingereza. Aliamua safari ya kijeshi kuiteka Egypt na kupunguza nguvu za Uingereza kuelekea India ambako walikua na biashara. Bonaparte alikua na nia ya kuianzishia Ufaransa mahuhisano na Mashariki ya kati na ikiwezekana kujiunga na Sultan wa Tipu ambae alikuwa adui wa Kiislam wa Uingereza. Napoleon alimhakikishia Mkurugenzi kuwa wakishateka Egypt tu, ataanzisha mahusiano na watoto wa mfalme wa India na kwa pamoja waishambulie Uingereza katika ardhi yenye thamani kwao.
May 1798, Bonaparte alichaguliwa kuwa mjubme wa Taaluma ya Sayansi Ufaransa. Safari yake ya Egypty ilijumlisha kundi la wanasayansi 167 na wataalamu wa hesabu, wataalamu wa mambo ya asili, chemistrym na geodesissts pamoja nae. Uvumbuzi wao ulikua pamoja na Rossetta Stone ambalo ni jiwe lililloandikwa Imani ya pili katika Imani tatu Hellenic Ptolemaic dynasty. Uvumbuzi huu ulichapishwa katika gazeti la Description de I'Egypte mnamo mwaka 1809.

Msafara wa Bonaparte ulifika Malta mnamo 09 June 1798, wakati huo ikimilikiwa na Knights Hospitaller hili lilikuwa jeshi la Wakatoliki. Kiongozi wao Ferndinand vo Hompesch zu Bolheim ambae alikuwa Mjerumani alijisalimisha kwa Bonaparte baada ya shambulio baada ya ubishi wa sitaki nina taka. Bonaparte alijichukulia kambi muhimu sana ya kijeshi akiwa amepoteza askari watatu tu.

Generali Bonaparte na msafara wake walikwepa Jeshi la Kifalme na kuzungukia Alexandria mnamo 01, July. Alipigana Vita ya Shubra Khit na Mamluks ambao ndio lilikuwa jeshi la Utawala wa Egypt. Hii iliwasaidia Wafaransa kufanya mazoezi yao ya kujihami kabla ya vita ya Piramid. Vita hii ilipiganiwa 21 July kwa umbali wa km 24 (mile 15) kutoka kwenye piramids. Jeshi la Generali Bonaparte lililokuwa na askari karibia 25,000 walilizingira jeshi la Mamluk ambalo lilipigana kisasa kwa wakati huo na farasi. Wafaransa 29 na inasadikiwa Waegypt 2,000 waliuwawa. Ushindi huu uliongeza ari kwa Wafaransa.

01 August, Waingereza walifanya shambulizi la kushtukiza chini ya Horatio Nelson walikamata au kuharibu meli karibu zote za Wafaransa , walibakisa mbili tu katika Vita ya Nile. Walilizima lengo la Bonaparte la kuiimarisha dola ya Ufaransa Mediteranaia. Jeshi lake lilishinda kwa muda kuimarisha nguvu ya Ufaransa Egypt, ingawa lilipata mashambulizi mengi. Mapema mwaka 1799, alihamisha majeshi yake katika wilayah ya Ottoman moja ya tawala za Damascus (Syria na Galilaya). Bonaparte aliongoza wanajeshi wake 13,000 katika kuteka miji ya pwani ikiwemo Arish, Gaza, Jaffa na Haifa. Mapigano ya Jaffa yalikuwa makali na ya kikatili. Bonaparte aligundua wengi wa washambuliaji wake walikuwa mateka wa kivita, aliamuru kuhifadhi risasi wauwawe kwa kutumbukizwa baharini au kunyongwa, wanaume, wanawake na watoto waliuwawa kwa muda wa siku tatu mfululizo.

Bonapart alianza na jeshi la askari 13,000; 1.500 kati yao waripotiwa kupotea, 1,200 walikufa na maelfu wengine walikufa kwa magonjwa hasa ugonjwa wa tauni. Alishindwa jaribio la kuiteka Acre ambayo sikuhizi inajulikana kama Akko nchini Israel, alitembeza jeshi lake mpaka Egypt mnamo Mwezi May, kwa kuhimiza kuondoka kwake eneo hilo, Bonaparte aliamuru wanajeshi walioshambuliwa na maradhi wauwawe na opium; idadi ya waliokufa mpaka leo ni fumbo, hakuna anaefahamu kati ya 30 au 580. Aliondoka na wanajeshi 1,000 walioumia. Aliporudi Egypy Bonarapart alimshinda vita ya Abukir ambayo iliongozwa na Saed Mutafa Pasha na jeshi la Ottoman.

Mtawala wa Ufaransa.
Wakati akiwa Egypt, Bonaparte alikuwa anapata habari za Ulaya na yanayoendelea huko. Aliambiwa kuwa Ufaransa imepata pigo kubwa katika vita iliyoongozwa na Uingereza, Austria na Urusi katika. 24 August 1799, alichukua upenyo wa Waingereza kuondaka kwa muda na yeye alipanda meli kuelekea Ufaransa, pamoja na kuwa hakupata dharura yeyote kutoka Paris na jeshi aliliacha chini ya uongozi wa Jean Baptiste Kleber.

Bila Bonaparte kufahamu kuwa Director alishamtuia ujumbe arudi haraka iwezekanavyo katika ardhi ya Ufaransa, mawasiliano mabovu yalisababisha ujumbe huo usimfikie. Wakati anafika Paris ilikuwa October, hali ya Ufaransa ilikuwa imetulia kwa ushindi wa mfululizo. Hata hivyo serikali ya Jamhuri haikuwa na pesa kabisa na Director hakuwa akipendwa na wengi kwa utendaji kazi wake. Director alimueleza Bonaparte jinsi
alivyokimbia mashambulizi lakini Bonaparte alikuw mdhoofu sana na hakuwa na nguvu za kumuadhibu.
Kaveli
Pamoja na kushindwa kwa safari ya Egypt, Napoleon alipokelewa kama shujaa. Alijiunga pamoja na director Emmanuel Joseph Sieyes, kaka yake Lucien ambae alikua speaker wa Baraza la Watu Miatano la Roger Ducos, director Joseph Fouche, na Talleyrand na waliweza kumtora Director kwa nguvu za kijeshi 09 November 1799 (siku hii iliitwa 18 za
Brumaire kwenye kalenda ya mapinduzi), kufunga baraza la watu mia tano Napoleon alikuja kuwa kiongozi wa kwanza wa serikali (consul) kwa miaka kumi pamoja na wasaidizi wengine wawili aliowachagua yeye. Nguvu za Napoleon serikalini ziliidhinishwa kwenye "Bunge la VIII", hili liliundwa na Sieyes ili kumpa Napoleon nguvu ndogo lakini baadae Napoleon alirekebisha makubaliano hayo na yalikubalika kwa kura (3,000,000 za ndiyo na kura 1,567 za hapana). Serikali ilionekana ni ya Kidemokrasia lakini ki uhalisia Napoleon aliingiza utawala wa kidiktekta.

Consulate wa Ufaransa.
Napoleon alitengeneza mfumo wa siasa ambao mwana historia Martyn Lyons aliuita "wa kidiktekta wenye kura ya ndio au hapana". Alikua na wasiwasi kuwa na demokrasia pamoja na mapinduzi yaliyokuwa yanaendelea lakini hakutaka kuyafumbia macho kabisa, Napoleon alibadilisha mfumo wa kupiga kura na wasimamizi wa kura katika safari yake ya kupata nguvu ya makoloni. Aliandika katiba ya Bunge la Mwaka wa VIII na alijiweka mwenyewe kuwa Kiongozi wa Kwanza na aliweka makazi yake Tuileries. Bunge liliungwa mkono kwa kura za kupindishwa katika uchaguzu uliofanyika Janurary iliyofuatia. Kura zilionyesha asilimia 99.4 walipiga kura ya "ndiyo", kaka wa Napoleon, Lucien alidanganya katika matokeo ya kura na kuonyesha kuwa watu million 3 walipiga kura katika kura za ndio au hapana; ki uhalisia walikuwa watu million 1.5. Waangalizi wa uchaguzi wa wakati huo wanadai namba ya wapiga kura ilionyesha watu million 5. Kwahiyo serikali iliongeza idadi ya namba ya wapiga kura kuonyesha kuwa watu waliomchagua Napoleon kwa mapenzi mema kuwa Consulate. Katika miezi yake ya kwanza kama Consulate, pamoja na vita vya Ulaya bado vikiwa vinaendelea, hali ya ndani ya nchi haikuwa imetulia. Napoleon kushikilia madaraka kulitia watu wengi hasira.

Miezi ya mwanzo wa 1800 Napoleon na jeshi lake walikatisha Swiss Alps kuelekea Italy ambako majeshi ya Austria yalichukua tena eneo la penisula wakati Napoleon yuko Egypt. Baada ya kuvuka kwa shida, majeshi ya Ufaransa yaliingia Kaskazini mwa Italy bila kupingwa, wakati jeshi la Ufaransa linaingia upande wa kaskazini, Waaustria walikuwa katika kituo cha Genoa ambacho kilikua kituo kidogo. Majeshi ya Ufaransa yaliwazunguka na baada ya siku chache za kutafutana hatimae majeshi ya Ufaransa yalikutana na kumpiga vita ya Marengo mnamo 14 June.

Ushindi wa Marengo ulimletea Napoleon sifa kubwa nyumbani na kurudisha heshima yake kisiasa lakini haukuleta amani. Kaka yake Bonaparte, Joseph aliongoza makubaliano magumu ya Luneveville ambao ni mji wa Loarraine na aliwaeleza Waingereza kuwa Austria ni sehemu ya Ufaransa sasa, Waingereza walikataa kabisa maelezo hayo na maongezi hayo yalikuwa magumu. Bonaparte alitoa amri kwa Generali Moreau kushambulia tena Austria na waliweza kushambulia Bavaria na kujichukulia ushindi mkubwa huko Hohenlinden December 1800. Matokeo ya kutekwa kwa Austria kulipelekea kusainiwa wa mkataba wa Luneville mnamo February 1801. Kufikia kipindi hicho ni Uingereza tu ndio nchi iliyobaki ikiwa na vita na Ufaransa.

Ushawishi wa Napoleon nje ya Ufaransa.
Napolieon ndiye alieeneza kanuni za Mapinduzi ya Ufaransa katika nchi nyingine, hasa kisheria akipinga sera za ubinafsi. Baada ya kuanguka kwa Napoleon, Napoleon Code iliendelea kuiletea ushindi Ufaransa hata kufanikiwa kuiteka Nertherlands, Belgium, na sehemu za Italy na Ujerumani, lakini pia imetumika kama msingi wa sheria katika nchi nyingi za Ulaya pia Jamhuri ya Dominica, Marekani, Canada hasa katika jimbo la Quebec. Kumbukumbu za Napoleon nchini Poland inasifa sana kwa msaada wake wa kuikomboa isimezwe na Urusi. Code ya Napoleon ilifutilia mbali utawala wa kifalme wa kumiliki kila kitu na kuleta watu wa kati wenye haki ya umiliki wa vyanzo vya uchumi.

Napoleon anaweza kuitwa mwanzilishi wa Ujerumani ya leo. Baada ya kuumalizika utawala wa Dola Takatifu ya Roma, alipunguza namba ya majimbo ya Ujerumani kutoka 300 mpaka kufikia 50, hii ilisaidia kuleta umoja wa Ujerumani. Kutokana na utawala wa Ufaransa nchini Ujerumani, ilileta nguvu ya umoja na mshikamano kati ya raia wa Kijerumani. Napoleon pia alisaidia sana Marekani alipokubali kuiuzia jimbo la Louisiana kwa dolla million 15 wakati wa uraisi wa Thomas Jefferson. Jimbo hilo ndio limeongeza ukubwa wa Marekani mara mbili na kuifanya iwe na state 13 katika umoja wake.

Kaveli
 
Napoleon Bonaperte kwa jina linginge Napoleone di Boungartealizaliwa 15 August 1769 na alifariki 05 May, 1821. Alikuwa mwanajeshi wa Kifaransa na pia kiongozi wa kisiasa aliejipatia umaarufu wakati wa mapinduzi wa Kifaransa na aliendesha kampeni nyingi zilizoleta mafanikio wakati wa vita vya mapinduzi. Akiwa Napoleon I, alikuwa kiongozi wa Ufaransa tangia 1804 mpaka 1814 na baadae tena 1815. Napoleon alitawala Ulaya na dunia kwa mambo mengi kwa miaka mingi akiwa anaiongoza Ufaransa kutoka vita nyingi ziliohusishwa na Vita vya Napoleon. Alishinda nyingi ya vita hivi na alijijengea ufalme mkubwa uliotawala bara la Ulaya kabla ya kushindwa 1815. Napoleon ni mmoja wa makamanda wa kuaminika ambae mbinu zake za kivita mpaka hii leo zinafundishwa katika mafunzo ya kijeshi dunia nzima. Na mpaka leo ni mwanasiasa anaeheshimika zaidi yatika historia ya binadamu.
800px-Jacques-Louis_David_-_The_Emperor_Napoleon_in_His_Study_at_the_Tuileries_-_Google_Art_Project.jpg

Napoleon alikua na nguvu na ushawishi mkubwa kwenye dunia iliyokuwa inaendelea na alileta mabadiliko mengi katika tawala nyingi alizoziteka na kuzitawala nchi kama Switzerland, Italy na Ujerumani. Alileta sera za mageuzi Ufaransa na nchi zote za Magharibi. Mafanikio yake ya kisiasa ya mwisho yaliyoitwa Napoleon Code, yanaushawishi katika mitaala mingi ya sheria katika nchi zaidi ya 70 duniani. Mwanasheria wa Kiingereza alieitwa Anderw Roberts anasema "Mawazo ambayo yanaongoza katika dunia ya sasa juu ya usawa, utawala kutokana na uwezo (merits), sheria za umiliki wa nyumba, uhuru wa kuabudu, usawa wa elimu, maswala ya pesa na mengine mengi yamekuwa shinikizwa, kuwekwa sawa na kusambazwa ki jiografia na Napoleon". Huko kwiningine alisisitiza utawala unaojitegemea kwa sehemu moja (local administration). Napoleon aliona umuhimu wa sayansi na sanaa katika maendeleo na pia alipiga vita sana ukabaila kumiliki mashamba (feudalism), hii ilipelekea mvutano wa kimaslahi kati ya Utawala wa Roma (Roman Empire).

Napoleon alizaliwa Corsica na alisaidia mapinduzi ya Ufaransa akiwa mwanajeshiana alijatahidi sana kusambaza mawazo ya kuutoa utawala wa kifalme katika sehemu yake aliyozaliwa Corsica. Alipanda vyeo haraka katika na kufikia cheo cha kamanda wakati wa mapinduzi baada ya kuwashinda wanajeshi waliokuwa upande wa mfalme. Alipokuwa na miaka 26 alianza kampeni ya kijeshi dhidi ya Australia na marafiki zake kama Itali, alijipatia sifa za ushindi wa ushawishi na kuweza kujishindia Penisula ya Itali kwatika mwaka mmoja, alikuja kuwa shujaa wa nchi yake. 1798 aliongoza jeshi lake katika safari ya Egypt na ilifanya mageuzi katika nguvu za siasa. Alipanga mashambulizi ya kijeshi November 1799 na kuwa Kiongozi wa nchi inayoongozwa na Utawala wa watu (Republican). Ushindi wake ulimpa ari ya kufanya mengi zaidi, 1804 alikuwa mtawala wa kwanza wa Ufaransa. Ubishi huu wa kisiasa ulimaanisha Wafaransa walikabiliwa na serikali ya tatu ya mseto mwaka 1895, Napoleon aliifunga hii serikali ya mseto kwa ushindi wa Ulm Campaign na vita ya watawala watatu wa Ulaya iliyojulikana kama Battle of Auterlitz iliyopelekea kuanguka kwa Utawala Mtatakatifu wa Roma (Holy Roman Empire). Mnamo mwaka 1806 serikali ya mseto ilianza kupigana na Napoleon Prussia ilianza kuwa na wasiwasi juu ya kukua kwa nguvu ya Ufaransa katika bara la ulaya. Haikuchukua muda kwa Napoleon kuushinda utawala wa Prussia katika vita ya Jeana na Austerlitz, aliongoza Jeshi la Umoja (Grand Army) ndani ya Ulaya Mashariki na kuishambulia Urusi June 1807 kwenye vita ya Friedland, ushindi wa Napoleon ulipelekea kusainiwa kwa mkataba wa Treaties of Tilsit. Mkataba huu ulikwa alama kubwa ya ushindi kwa Ufaransa lakini haukuiwekea amani bara la ulaya. Miaka miwili baadae Autrians walianza kuwapiga Wafaransa. Napoleon aliongeza nguvu ya jeshi lake na kupelekea ushindi kwenye vita ya Wagram, vita hii Waingereza waliungana na Wautsria kupigana na Ufaransa.

images

Napoleon alihamasika kuendeleza mawazo yake katika bara lote la ulaya na hii alifikiria kukomesha bidhaa za Uingereza ulaya itasaidia kuwashawishi Waingereza waondokane na utawala wa kifalme. Alivamia Spain, Portugal na pamoja na visiwa vya Gibraltar na alimtangaza kaka yake Joseph kuwa Mfalme wa Spain mwaka 1808. Spain na Portugal ziliungana na Mwingereza na kuanza vita ya Peninsular iliyodumu kwa miaka sita, vita hii ilitawaliwa na mashambulizi ya msituni. Ushindi mkubwa uliopatikanana ulimaanisha Napoleon alikua na maamuzi juu ya Spain, Portugal na Uingereza.

Utawala wa ulaya (system) ulisababisha vita vya kidiplomasia kati ya Ufaransa na marafiki zake kama Urusi ambayo haikuwa tayari kupoteza biashara. Warusi walipinga utawala huo na kumchokoza Napoleon kuingia vitani. Wafaransa walihamasisha shambulizi kwa Warusi kiangazi cha 1812. Vita hii ilipelekea kuanguka kwa jeshi la wananchi na machafuko makubwa yalitokea katika miji ya Urusi. Maadui wa Napoleon waliungana.

Maadui wa Napoleon walikuwa pamoja na Austria, Portugal, Spain, Russia na jeshi lao lilimshinda Napoleon katika viat ya Leipzing October 1813. Jeshi la adui liliingia Ufaransa na kuteka Paris April 1814, hii ilipelekea Napoleon kusalim amri mwezi April mwaka huo. Alikimbilia katika kisiwa cha Elba karibu na Rome na utawala wa kifalme wa Bourbon ulirudishwa madarakani. Napoleon alitoka katika kisiwa cha Elba mwaka 1815 na kuchukua tena madaraka ya Ufaransa, alianza mashambulizi mapya na wakati huu maadui wake waliungana na Waingereza na kumshambulia Napoleon katika shambulio la vita ya saba ya mseto. Vita hii pia iliitwa siku 100 za Napoleon ambazo alishindwa katika Vita ya Waterloo. Mpaka leo waingereza wanamsemo "this is my Waterloo" wakimaanisha anguko langu

Maisha ya mwanzo ya Napoleon.
Napoleon alizaliwa 15/08/1769, wazazi wake wakiwa Carlo Maria di Buonaparte na Maria Letizia Ramolino, katika kijiji cha asili yao cha Casa Buonapartein Ajaccio, mji mkuu wa kisiwa cha Corsica, akiwa mtoto wa nne kuzaliwa na watatu wa kiume. Mwaka aliozaliwa Napoleon ulikuwa mwaka mmoja tangu Corsica iwe chini ya utawala wa Ufaransa kutoka Jamhuri ya Genoa. Alibatizwa kama Napoleone di Buonaparte, alipewa jina la baba mkubwa ambae alikufa akiwa mtoto nae aliitwa Napoleon.
Ukoo wa Corsican Buonapartes ulitokea katika jamii ndogo ya Itali yenye heshima ambayo asili yake ilikuwa Tuscan, walikwenda Corsica wakitokea Liguria mnamo karne ya 16.

Baba yake Mheshimiwa Carlo Bounaparte alikua mwanasheria na yeye ndie alikuwa mwakilishi wa mfalme Louis XVI katika mahakama za Corsica mwaka 1777. Mtu aliekuwa na ushawishi mkubwa katika maisha ya utoto ya Napoleon alikuwa mama yake, Letizia Ramolino, ambae alimwadhibu na kuweka nidhamu kwa mtoto mkorofi Napoleon. Bibi mzaa mama wa Napoleon aliolewa tena Switzelarnd kwenye ndoa yake ya pili na mjomba wa Napoleon ambae alikua baadae cardinali Joseph Fesch, alikuwa ndie mwangalizi wa familia ya Bonaparte baadae.

Kutokana na familia aliyotoka Napoleon alikua na nafasi nzuri ya kusoma kuliko uwezo wa kawaida wa watu wa Corsican kwa wakati huo. January 1779 aliandikishwa kwenye shule ya dini ya Autun. May mwaka huo aliandikishwa kwenye shule ya maafisa wa kijeshi cha Brienne-le-Chateau. Lugha yake ya kwanza ikiwa Corscan, Kifaransa chake kilikua na laufidh ya Corsca na hakuweza kuandika neno French vizuri. Wanafunzi wenzake walimcheka kwa laufidh yake. Kutokana na hali hiyo aliamua kusoma sana na kuwa na muda mchache wa kuongea na wenzake. Siku ya mtihani mtahini wake aligundua uwezo wake mkubwa katika hesabu pia alielewa vyema historia na jografia na mtahini alisema "huyu kijana atakua baharia mzuri".

Alipomaliza masomo yake Brienne mwaka 1784, Napoleon alijiunga na chuo cha maafisa wa jeshi cha Ecole Militire mjini Paris. Alifundishwa kuwa ofisa wa mashambulizi ya silaha, baada ya kifocha baba yake ambacho kilipunguza uwezo wa kifedha na ilibidi amalize shule katika mwaka mmoja badaya ya miaka miwili. Alikua na mtu wa kwanza kutoka Corsican kumaliza Ecole Militaire na mtahini wake alikua mwanasayansi Pierre-Simon Laplace.

Maisha ya awali kama mwanajeshi.
Baada ya kuhitimu September 1785 alipangiwa kazi ya second lieutenant katika kikosi cha mashambulizi ya silaha na alifanya kazi mjini Valence na Auzonne mpaka wakati wa mapinduzi mwaka 1789, alichukua likizo ya karibia miaka miwili kati ya miji ya Corsica na Paris katika kipindi hicho. Kipindi hicho alikua raia mashuhuri wa Corsica na alimwandikia kiongozi wa wa Pasquale Paoli May 1789 kua "kama taifa nililozaliwa linateketea na wanajeshi wetu 30,000 wametapikwa kwenye pwani za bahari wakizika uhuru kwenye mawimbi ya damu. Hii hali yakusikitisha imenistua sana.

Alitumia miaka ya mwanzo ya mapinduzi kupigana na watu wa aina tatu, wanamapinduzi, waliompenda mfalme na watu wa Corsica. Alimuunga mkono Jacobin ambae aliamini utawala wa wengi (republican), waliratibu vilabu kwa wananchi wa Corsica na aliwapa amri askari wa kujitolea wa silaha. Alipandishwa cheo kuwa Kaptain katika jeshi la kawaida japokuwa hakuwepo jeshini na hali hiyo ilileta ubishi na watu walipinga sana kwa vurugu dhidi ya jeshi la Ufaransa mjini Corsica.

Alirudi Corsica ambako alitofautiana na Paoli, ambae aliamua kujitenga na Ufaransa na kuharibu mashambulizi ya Ufaransa ya kisiwa cha Sardini katika La Maddalena. Familia ya Bonaparte ilikimbilia Ufaransa June 1793 kwasababu ya kutofautiana na Paoli.

800px-Napoleon_-_2.jpg

Napoleon akiwa Second Lieutenant wa Corsica, mwenye umri wa miaka 23.

Shambuli ka kuteka Toulon.
Mnamo July 1793, Bonaparte alichapisha kipeperushi (pamphlet) kilichoitwa Le souper de Beucaire (Supper at Beucaire), kipeperushi hiki kilisaidia kuungwa mkono na Augustin Robespierre ambae alikua mdogo wa mwanamapinduzi Maximillien Robespierre. Kwa msaada wa mtu mwingine wa Corsica Antoine Christophe Saliceti, Bonaparte alipewa cheo cha kamanda wa askari wenye silaha wa jeshi la wananchi katika kuteka Toulon.

Alijipatia mbinu ya kuteka kilima ambapo wanajeshi wa jeshi la wananchi wenye bunduki walizunguka bandari ya mji na hii ilipelekea majeshi ya Waingereza kukimbia. Pigano hili lilipelekea kuchukua mji na Bonaparte alijeruhiwa pajani. Alipandishwa cheo kuwa brigadia generali akiwa na miaka 24 na hii ilipelekea macho ya Kikao cha Kamati ya Usalama kumteua kuwa Kiongozi wa jeshi la silaha la Ufaransa katika jeshi la Italia.

Napoleon alitumia muda kama inspekta wa pwani ya Mediterranea karibu na Marseille ambapo alisubiri kwa kuhakikishwa kwa post yake ya Jeshi la Italy. Alibuni mbinu ya kushambulia Ufalme wa Sardinia kama mpango wa Ufaransa dhidi ya vita ya kwanza ya majeshi ya falme za ulaya kuzuia mapinduzi ya Ufaransa. Augustin Robespierre na Saliceti walikua tayari wanasubiri amri ya kiongozi wa silaha.

Jeshi la Ufaransa liliendelea na mashambulizi ya Vita ya Saorgio Aprili 1704 kwa mipango ya Bonaparte na waliendelea kuteka Ormea katika milima. Kutoka Ormea walielekea magharibi na walilizunguka jeshi la Austro-Sardinian katika Saorge. Baada ya kampeni hii, Augustin Robespierre alimpeleka Bonaparte katika Jamhuri ya Genoa kuangalia nini nia ya serikali kuhusu Ufaransa.

Napoleon_%C3%A0_Toulon_par_Edouard_Detaille.jpg

Napoleon katika shambulizi la kuteka Toulon akiwa na umri wa miaka 24

Vita ya wanamapinduzi na wapenda ufalme mjini Paris (13 Vendemiaire)
Kuna mazungumzo yanayoendelea yasemayo Bonaparte alipewa kifungo cha ndani ya nyumba kwa uhusiano wake na wakina Robespierres kufuatia kushindwa kwao kwenye shambulio la Thermidorian July 1794, lakini katibu wa Napoleion aitwae Bourrienne, anasema maneno ya wivu yaliyohusu jeshi la Alps na jeshi la Italy ambalo Napoleon alilifanyia kazi wakati huo. Bonaparte aliandika barua yenye maelezo ya kutoa machozi katika kujitetea kwake kwa afisa mkuu wa serikali na hii ilipelekea kufutiwa makosa yake.
Aliachiliwa katika wiki mbili na kutokana na ufundi wake wa kivita, aliombwa aanze mipango ya mashambulizi ya Italia kama moja ya mashambulizi ya Ufaransa kwa Austria. Pia alishiriki katika safari ya kurudisha majeshi Corsica kutoka Uingereza, lakini Wafaransa walishambuliwa na Jeshi la Mfalme la Uingereza.

Mwaka 1795, Bonaparte alikuwa engaged kwa Desiree Clary, binti wa Francois Clary. Dada wa Desiree aitwae Julie Clary alishaolewa na kaka yake Napoleon aitwae Joseph. April 1795, alipewa cheo cha Ofisa wa Magharibi, ambacho kilihusisha vita ya Vendee hii ilikuwa vita ya wenyewe kwa wenyewe na wapenda ufalme. Post hii ilikua ya chini kulilo ofisa wa silaha na Napoleon alidai afya yake si nzuri.

Queen_desideria_by_locati-2.jpeg

Desiree Clary

Alihamishwa kwenye idara ya kusoma ramani na Kamati ya Usalama wa Taifa na alifikiriwa kwenda kufanya kazi kwa Sultan wa Constantinople (Turkey). Katika kipindi hiki aliandika kitabu cha mapenzi kilichoitwa Clisson et Eugenie, kilihusu askari na mpenzi wake, kwa uhalisia kilihusu mahusiano yake binafsi na Desiree. Mnamo September 15, Bonaparte aliondolewa katika orodha ya magenerali kutokana na kukaidi kwake kupigana vita ya Vendee, nguvu zake za kijeshi zilipunguzwa pia na uwezo wake wa kifedha.

Mnamo tarehe 03/10/1795 majeshi ya mfalme yalitangaza kukaidi maamuzi ya National Convention hili lilikua baraza la muda la kuongoza serikali baada ya mapinduzi na kiongozi wake alikua Paul Barras. Kiongozi wa Thermidorian alijua uwezo wa Bonaparte na alimpa amri ya kuvamia jumba la kifalme la Tuileries kulinda mapinduzi. Mauaji makubwa ya askari wa mfalme wa jeshi la Swiss pale na miaka mitatu baadae alitoa maelezo kwamba silaha ndio ilikua ulinzi.
]
Alitoa amri wa afisa wa kikosi cha farasi alieitwa Joachim Murat kutwaa silaha kubwa za kijeshi na kuzitumia kwenye mashambulizi 05/10/1795-13/10/1795 katika kalenda ya Ufaransa. Askari 1,400 wa mfalme waliuwawa katika mashambulizi haya na wengine waliobakia walikimbia. Alitangaza mji kwa cannon (a whiff of grapeshot) kutokana na maelezo ya wanahistoria wa karne ya 19 kama Thomas Carlyle katika maelezo yake HISTORIA YA MAPINDUZI YA UFARANSA.

Ushindi dhidi ya majeshi ya mfalme ulizima mawazo ya kubadilika kwa utawala na ulimpatia Bonaparte umaarufu wa ghafla pamoja na utajiri pia uongozi katika serikali mpya. Murat alimuoa mmoja wa dada wa Napoleon na akawa shemeji yake; pia alitumikia chini ya Napoleon kama mmoja wa majenerali. Bonaparte alipandishwa cheo kuwa kamanda wa majeshi ndani ya jeshi la Itali. Wiki chache baada ya hapo alikuwa kwenye mapenzi na Josephine de Beauharnais, aliekuwa mpenzi wa Barras kabla. Walioana 09 March 1796 kwa sherehe za kiserikali.

13Vend%C3%A9miaire.jpg

Mashambulizi ya silaha kwenye kanisa la Saint Roche Paris wakati wa 13 Venemiaire

Marie Josèphe Rose Tascher de La Pagerie alishaolewa ndoa ya kwanza na Francois Beauhanais na kujaliwa kupata watoto wawili kabla hajakutana na Napoleon. Beauhanais alikua tajiri sana lakini ndoa yao na Marie Josephe haikua na mapenzi, na hii ilipelekea kuachana. Marie Josephe alikuwa mkubwa kwa Napoleon kwa miaka sita.

Ridpath-Josephine_de_Beauharnais.jpg

Siku mbili baada ya ndoa, Bonaparte aliondoka Paris kwenda kwenye kazi yake kama kamanda wa jeshi la Iltali. Alikwenda kwa ari zote za kulipiga jeshi la Piedmont kabla ya rafiki zao Austria hawajaingia. Katika mfululizo wa mafanikio wakati wa shambulio la Montenotte, alipiga jeshi la Piedmont nje ya vita katika wiki mbili. Wafaransa baadae walianza kuwapiga Austria kwa muda uliobakia, ushindi huu ulijulikana kama mateko ya Mantua.
Austria walipiga mashambulizi mengi kwa Wafaransa lakini chini ya uongozi wa Napoleon washinda kwa mfululizo wa mapigano kutoka Castiglione, Bassano, Arcole na Rivoli na hii ilipelekea kuanguka kwa nafasi ya Austria nchini Itali. Askari 14,000 wa Australia walikufa na wafaransa walipoteza askari 5,000.

Kilichofuatia Wafaransa walivamia nyumba ya Habsburg, hii ilikua nyumba ya kifalme iliyosifika katika bara lote la ulaya. Majeshi ya Ufaransa yalianza Kusini mwa Ujerumani wakati huo walishindwa na Archduke Charles katika mwaka 1796, Archduke alisogeza majeshi kulinda mji wa Vienna baada ya kujua habari za Napoleon na aliyoyafanya Paris. Mkutano wa makamanda hawa wawili, Napoleon alirudisha majeshi ya Archduke nyuma na kuendelea mpaka katikati ya nchi ya Austria baada ya kushinda vita ya Tarvis mnamo March 1797. Waustria walipewa onyo na Wafaransa kuwa kutoka Leoben mpaka Vienna umbali wa takriban km 100 na waliamua kutafuta suluhu kwa njia ya amani. Ushindi wa Leoben ulifuatiwa na ushindi kamili Treaty of Campo Formio na hii iliipa Ufaransa nguvu ya kumiliki sehemu kubwa ya Kaskazini mwa Itali na nchi nyingine za chini. Ufaransa ilichukua uhuru wa nchi hizo uliodumu kwa miaka karibu 1,100. Pia aliruhusu farasi wake kuharibu farasi wanne ambao walikua mapambo ya fahari yaliyoitwa Horses of Saint Mark, farasi hao wa mapambo walitengenezwa kwa shaba.
Asante sAana! NaombA ya Alexander the great!
 
Back
Top Bottom