Nape: Wanahabari wahamasishe wananchi kugombea nafasi mbalimbali uchaguzi wa Serikali za Mitaa bila kujali vyama vyao

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,828
13,585
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (World Press Freedom Day) kwa Mwaka 2024 yanaendelea Jijini Dodoma, leo Mei 2, 2024.

Spika wa Bunge la Tanzania - Tulia Ackson ndiye mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo yanayofanyika kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, ikiwa ni siku ya pili kati ya tatu

Kauli Mbiu ni Uandishi wa Habari na Changamoto za Mabadiliko ya Tabia Nchi

Viongozi wengine wanaoshiriki ni
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari - Nape Moses Nnauye,
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma - Rose Senyamule Staki,
Mratibu Mkazi wa UN - Zlatan Milisic,
Rais wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) - Deogratius Nsokolo,
Mwakilishi wa UNESCO - Michel Toto,
Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC - Kenneth Simbaya

Hotuba:
Rais wa UTPC - Deogratius Nsokolo,

Tupo hapa Dodoma kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani ambapo tunatarajia kuwepo na waziri mkuu katika siku ya kilele, Mei 3, 2024. Tunaishukuru serikali kupitia bunge la JMT kupitia sheria ya huduma ya habari tanzania ambapo ilirekebisha vifungu tisa. Vifungu hivyo vilikuwa vinatukwaza kwa hiyo tunashukuru sana.

Ni matarajio yangu kwamba katika siku za usoni, vifungu 12 vilivyobaki serikali itafanya haraka kuvifanyia marekebisho ikiwa tutakubaliana katika maeneo yanayotarajiwa kufanyiwa marekebisho. Sisi ni chache, hivyo tuna matumaini makubwa na serikali na Bunge, hivyo tunaomba sana muendelee kutusikiliza ili muzifanyie kazi sheria zote zinazotukwaza.

Naomba nikukaribishe katika ukumbi huu na nakushukuru sana kwa kuja.

Alichozungumza Waziri Nape Nnauye
Nimshukuru Rais kwa kuwa tangu mwaka jana ni mambo mengi katika habari amefanya yameboreshwa. Kwa lugha rahisi, inawezekana hatujafika tulipopataka lakini hatupo tulipokuwa jana. Kuna juhudi zimefanyika kuhakikisha uhuru wa habari unazidi kuimarika siku hadi siku.

Nimeanza kuona wanahabari wanabeba ajenda kubwa za nchi yetu kama mazingira, gesi na kampeni mbalimbali. Uwezo wao na kalamu zao zina nguvu kubwa sana. Wanahabari wakiamua kukoroga mambo yanakorogeka. Niwashukuru sana, wanahabari mmetimiza majukumu yenu vizuri.

Baadhi ya vifungu vya sheria vya huduma ya habari vilivyobadilika vina mkono wa spika wa bunge kwa kuwa aliniuliza kwa baadhi ya vifungu ambavyo alivijua kutoka kwa waandishi waliomfikia spika moja kwa moja. Kuna wakati tunatunga kanuni ambazo hazieleweki eleweki, lakini tunajitahidi kuwashirikisha wadau na bunge ili kanuni zisipingane na sheria mama.

Tunataka kuunganisha sera za vyombo vya habari. Utangazaji na Print media ili twende kwa pamoja. Wakati ukifika tutaleta. Kwenye uhuru tunakwenda vizuri, fungia fungia haipo tena, changamoto kubwa ni uchumi wa vyombo vya habari. Kama tusipotatua uchumi wa vyombo tutafanya kazi bure.

Tuliunda tume ya uchunguzi kwa maagizo ya Rais. Tume imekuja na majibu tutayatoa hivi karibuni, kwa vyombo vinavyoidai serikali vitalipwa. Kuna vyombo vingi vimefungwa kwa kushindwa kujiendesha. Uhuru bila kuwa na uhuru wa uchumi hatutafika. Baadhi ya wanahabari wamekuwa wakimtegemea mtoa habari kuwalipa.

Nawaomba wanahabari wahamasishe watanzania wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Na vyombo vya habari vitoe nafasi sawa kwa wananchi wote bila kujali vyama vyao.

Freedom of the press is not just important to democracy, it is democracy. twendeni kuijenga nchi yetu.

Alichokisema Dkt. Tulia Ackson
Nitoe rai kwa waandishi wa habari na watangazaji kuihabarisha umma kuhusu mabadiliko ya tabia nchi. Sio kila jambo la kimazingira linahusika na mabadiliko ya tabia nchi. Tunategemea wanahabari kuhabarisha umma kuhusu nini mabadiliko ya tabia nchi haswa. Kuna vitu wananchi wanapelekewa wanachanganywa kuhusu kujua ipi ni mabadiliko ya tabia nchi na kipi ni mabadiliko ya kawaida ambayo yamekuwepo miaka yote.

Hivi karibuni tumepitia mafuriko, tunayasema sana kwenye mabadiliko ya tabia nchi. Haya ukiwaeleza wazee wanaweza kukwambia kuwa ni mambo ya kawaida kutokea. Hivyo tunawategemea waandishi kuwafikishia wananchi kuhusu uhalisia wa mabadiliko ya tabia nchi na mambo ambayo ni kawaida kujirudia.

Tunawategemea wanahabari kusaidia kwenye kuokoa mazingira. Inabidi wananchi kufahamu tabia ya kutupa taka hovyohasa za plastici kuna athari kubwa kwa mazingira, sio tu hapa nchini bali hata na nchi nyingine. Kwa hiyo waandishi inabidi mseme hilo.

Pia kuna jambo lingine la ukatili wa kijinsia. Mara nyingi mmekuwa mkiripoti ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake, lakini pia wanaume wamekuwa wakipitia ukatili wa kijinsia. Nyinyi kwa kutumia kalamu zenu mtusaidie kuwaweka salama watu wote salama kwenye jamii yetu.

Natambua mchango wa serikali, lakini serikali haiwezi kufanyakazi peke yake bali inahitaji kushirikiana na asasi za kiraia. Lakini tunatambua mchango wa vyombo vya habari katika kuzifikisha habari hizi, ambapo huwa mnatumia ujuzi wenu kuwasilisha mambo kwa jamii katika lugha inayoeleweka.

Mchango wa wanahabari katika maendeleo ni mkubwa sana. Maendeleo kwenye maji na sekta ya gesi. Maana mwanasiasa anaweza kutaja takwimu lakini kama takwimu hazijaandikwa kwa habari hazitawafikia watu hazitakuwa na maana.

Kwahiyo, hatutarajii kusikia habari za kusifia tu kwamba hospitali imejengwa bali pia hata kama mtu ameenda amekosa dawa pia ni muhimu kuiandiaka. AU kama kituo cha afya kiko mbali na jamii ni vizuri kuandika kwamba kituo hakina tija kwa kuwa hakitumiki. Hivyo msikae tu kutusifia.

Naiona changamoto kwenye kutoa fursa sawa ya kuhamasisha watu kushiriki uchaguzi kwa usawa bila kubagua vyama vyao. Kwa sababu vyombo havina fedha hivyo wanasiasa wenye fedha wanaweza kuwa wanawalipa watendaji wa vyombo hivyo ukakuta mtu mmoja anapata coverage.

Hapa itabidi kila taasisi ya serikali inayodaiwa ilipe kama hawalipi inabidi tuone mchakato waliojipanga watawezaje kulipa madeni hayo ili wawe vizuri kiuchumi na kufanya kazi zake kwa namna ambavyo wanategemewa wafanye.

Suala la malipo ya serikali kwa vyombo vya habari tutaishauri serikali ili iweze kulipa. Pia waandishi wa habari waweze kulipwa vizuri.

Jambo la waandishi ambao huwa wanatumwa kutoa taarifa za bunge. Tusaidiane kwenye kuwafanya waandishi hawa, wawe ni maalumu ili wawe wanatoa taarifa zenye weledi. Mtu anapokuwa muandishi wa bunge anakuwa anapata mafunzo, unapombadilisha maana yake unamleta yule ambaye hana mafunzo hii inakuwa changamoto. Kwa hiyo wahariri haya sio maelekezo bali ni ushauri kwenu kwamba msibadilishe badilishe waandishi. Kwa wenzetu wengine wanakuwa na waandishi wailiobobea.

Mwakilishi wa UNESCO: Michel Toto
Uhuru wa habari ni nguzo muhimu ya demokrasia. UNESCO inafurahi kuwa sehemu ya siku hii kwa kuwa tunathamini sana Uhuru wa Habari. Tunalishukuru bunge la Tanzania, hasa Neema Lugangira kwa kujizatiti kwake kwenye masuala mbalimbali.

Mratibu Mkazi wa UN - Zlatan Milisic
Nashukuru kupewa fursa ya kutoa neno la shukrani kwa mkutano huu wa uhuru wa habari. Akhsante Spika wa bunge kwa maneno yako kwa waandishi wa habari kwa kuwashauri waiwajibishe serikali nk. Uandishi wa habari wa masuala ya mazingira imekuwa ni suala linalopewa kipaumbele kwa sasa kutokana na namna yake ya kuokoa mazingira. Hata hivyo tunatambua changamoto ambazo waandishi wamekuwa wakizipata, kwa mfano waandishi walioawa Gaza nk. Kwa sababu hiyo umoja wa mataifa unajitahidi kuhakikisha kuwa waandishi wanakuwa salama wanapotekeleza majukumu yao
 
Back
Top Bottom