Nape Nnauye: Bajeti inatupeleka Tanzania ya Kidijitali. Hadi barua za watendaji mtaa kuhamia 'online'

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,507
8,136
Waziri Nape ametoa dondoo za bajeti yake anayotarajia kuisoma kesho ikiwemo Taifa kuhamia dijitali. Nape amesema kutakuwa na kitambulisho kimoja na kila kitu kitaunganishwa humo na watu wataacha kuhangaika kutafuta huduma kwani kila kitu kitaletwa 'Online'.

Waziri Nape Nnauye: Bajeti inaenda kutupeleka kwenye Tanzania ya kidijitali, kwa lugha rahisi ya mtaani tunataka huduma zote za Serikali kupatikana mtandaoni, ukitaka passport yako usilazimike kwenda ofisini, juzi tumefanya majaribio hata ya kuomba barua kwa watendaji wa mitaa yetu na vijiji.

Tunataka tuondoke kwenye utaratibu wa watanzania kutembea na vitambulisho vingi mfukoni, uwe na kitambulisho kimoja na kikupe huduma zote unazozihitaji.

Tunaendelea kukamilisha ujenzi wa Tanzania ya kidijitali ili tuondokane utaratibu wa kuhangaika kupata huduma, huduma zote ziweze kupatikana popote ulipo.

Nape pia ameongelea sekta ya afya ambapo amesema bajeti mpya mifumo itasomana na mgonjwa akifanyiwa CT Scan Dodoma hatalazimika kurudia kufanya tena akipelekwa Dar es Salaam. Nape amesema kitambulisho kitakuwa na taarifa za afya za mtu na zitasoma popote atapoenda duniani.

Serikali kuongeza kasi ya internet ili huduma ziwende kwenda ikiwemo kufundishana, kuendesha robot nk.

Kuhusu ajira, Nape amesema Tehama ina mapinduzi makubwa japokuwa wapo watakaopoteza kazi lakini amesema sayansi inasema unapoteza kazi mbili na kutengeneza kazi nne na hamna namna ya kuikwepa.

Pia, soma=> Nape Nnauye: Tanzania kuwa na Satelaiti yake kama backup ya internet, Mkongo uliokatika kuchukua siku 7 zaidi kutengemaa
 
Kwa Mtandao Huu ? Bado tuna safari ndefu na sio kwa Tanzania tu bali kwa Africa kwa ujumla hatuna Internet ya uhakika. Ni Muda wa kushirikiana nasisi tuweke Plan B, Mifumo ya wazungu ikikikataa.
 
Back
Top Bottom