The Khoisan
JF-Expert Member
- Jun 5, 2007
- 16,398
- 14,497
![]()
Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye akizungumzia kitendo cha baadhi ya wabunge wa upinzani bungeni kususia vikao vya bunge kwa madai ya kutokuwa na imani na Naibu spika Dk. Tulia Ackson.
Waziri Nape amesema ’Wingereza wanasema mtu mwenye akili ndogo anajadili watu, wenzetu wana mgogoro na naibu spika lakini zipo njia za kibunge za kutatua huu mgogoro lakini wao hawataki kuzifuata, hii ni ishara kuwa wanaongozwa na akili ndogo‘
‘Lakini la pili kubwa linalosikitisha ni kuwa anayewaongoza kutoka na kuingia Freeman Mbowe haji, havai makaratasi kama wenzake na huwenda yupo tuu nyumbani amelala nyumbani kwake. Ushauri wangu wajaribu kuwa na akili kubwa kidogo ya kushughulika na mfumo‘ –Waziri Nape
Kumbe watu wakipata madaraka wanafikiri wana akili kubwa kuliko wanaowaongoza!!?
No wonder ..............!!!?