NAPE: Mbowe haji, havai makaratasi kama wenzake yupo nyumbani amelala

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,621
8,411



Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye akizungumzia kitendo cha baadhi ya wabunge wa upinzani bungeni kususia vikao vya bunge kwa madai ya kutokuwa na imani na Naibu spika Dk. Tulia Ackson.

Waziri Nape amesema ’Wingereza wanasema mtu mwenye akili ndogo anajadili watu, wenzetu wana mgogoro na naibu spika lakini zipo njia za kibunge za kutatua huu mgogoro lakini wao hawataki kuzifuata, hii ni ishara kuwa wanaongozwa na akili ndogo‘

‘Lakini la pili kubwa linalosikitisha ni kuwa anayewaongoza kutoka na kuingia Freeman Mbowe haji, havai makaratasi kama wenzake na huwenda yupo tuu nyumbani amelala nyumbani kwake. Ushauri wangu wajaribu kuwa na akili kubwa kidogo ya kushughulika na mfumo‘ –Waziri Nape

 
Nape, Nape, Nape rudia, wana akli ndogo? Kipimo chako ni kipi? Tuanzie hapo.
 

Nape bwana, nadhani anampenda sana Mbowe. Yaani haipiti wiki kabla hujamsikia Nape akisema Mbowe hivi, Mbowe vile.
 
Nape umeongea maneno ya hekima sana HASA HASA HAYO ULIYOMALIZIA

ni kweli kila mbuge arudi jimboni kwake ili akafanye maandamano na wananchi waliomchagua hadi kieleweke!

Sio kupeleka maandamano baadhi ya mikoa ilihali

Wananchi wa eneo husika wanapigwa na kuvunjwa vunjwa na polisi

Alafu baadhi ya wabunge majimbo yao yapo salama na shughuli za kimaendeleo zikiendelea
 
Safi Sanaaa!
 
Kwa hiyo anaejadili watu ni huyo Nape na wewe. Poleni sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…