Nape: Hatutaki kudhibiti wanahabari

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,591
8,812
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema hawataki kuwadhibiti wanahabari bali kuwawekea mazingira bora ya kufanya kazi.

Kauli hiyo ameitoa wakati akifanya mahojiano na kipindi cha Dira ya Dunia kinachorushwa na kituo cha radio cha BBC ambapo amesema Serikali inafanya mchakato wa kuandaa sera na sheria za habari ili kumuwezesha mwandishi atimize majukumu yake kwa ufanisi zaidi.

Waziri Nape amesema serikali inataka kurejea kwenye mstari wa kuwa kinara wa kufanya vizuri katika sekta ya habari baada ya kuporomoka katika miaka ya hivi karibuni.

"Rais Samia Suluhu Hassan ni muumini wa haki na uhuru wa habari ndiyo maana kuna sheria zinazobana waandishi katuambia tusizifanyie kazi na tuzirekebisho baada ya kujadiliana na wadau".

Amesema kudhibitisha dhamira hiyo baadhi ya vyombo vya habari zinafanya kazi bila ya kupewa leseni kama sheria inavyotaka lakini kwa kuwa dhamira ni kujenga nchi zimeachwa hadi.

Waziri Nape amesema vyombo vya habari zimekuwa na mchango mkubwa kwa Taifa na hilo limeonekana katika kuhamasisha sensa ya watu atu na makazi inayoendelea hivi sasa.

"Uhusiano wa serikali na vyombo vya habari ni mzuri na ninaamini tukiendelea hivi tutafika mbali na sekta hii itakuwa ya kupigiwa mfano ndani na nje ya nchi" amesema

Waziri Nape amesema anaamini Bunge litapitisha mabadiliko ya sheria za habari zitakazopelekwa bungeni na serikali ili kanuni zitungwe na wanahabari waanze kujisimamia kupitia Baraza Huru ya Habari" amesema

Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile, amesema dhamira ya serikali ni njema hivyo wanahabari watimize wajibu wao kwa kuwa hakuna haki bila wajibu.

Amesema dhamira ya serikali haipaswi kutegemea utashi wa viongozi pekee bila uwepo wa sheria kwa kuwa anaweza kutokea kiongozi akazitumia sheria zilizopo ambazo zinakandamiza waandishi wa habari.

"Sisi tunaamini ni lazima tutumize wajibu wetu ikiwemo kuzuia uchapishaji na utangazaji wa taaluma yetu" amesema.
 
Mnapodhibiti uhuru wa mtu kutoa maoni yake hata asiye mwanahabari, maana yake kisaikolojia mnawadhibiti hata hao wanahabari wenyewe.
 
Wanahabari chonde chonde msije kumwamini huyu waziri na kujiachia.

Speaker Ndugai alitoa maoni yake tu leo hii hata kutoka nje ya nyumba yake ni shida.

Afumwisye wa TRC alitoa maoni yake kuhusu tozo, hivi tunwvyoongea kalala ndani.

Wanahabari akili mu kichwa!
 
Back
Top Bottom