Nape Aangukia Pua Bungeni

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
ILE kauli kwamba ‘muosha huoshwa’ imedhihiri bungeni baada ya wabunge kumkalia kooni Nape Nauye, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo, anaandika Faki Sosi

Jana wabunge hao wamesema kwamba, Nape ambaye kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana, alikuwa akinadi baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Tano kuwa mizigo na kwamba, kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya bunge kutazuia wananchi kumpima kama yeye ni mzigo ama rumbesa.

Miongoni mwa waliomng’ang’ania Nape ni Mwita Waitara, Mbunge wa Ukonga, Dar es Salaam (Chadema) ambapo wakati akichangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2016/17 amesema, matangazo hayo yangeonesha wazi kwamba Nape ni mzigo ama rumbesa.

Amesema, Serekali ya Rais John Magufuli inawasukuma wananchi kuomba stakabadi lakini haitaki wajue namna gani fedha wanazolipia kodi zinavyotumika.

“Nilipoona amepewa Wizara ya Habari nikajua ataruhusu mojadala ya wazi ili tumuone yeye kwamba hatokuwa mzigo lakini yeye amekuwa rumbesa,” amesema Waitara.

Kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana, Nape akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwa na Abdurahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM walitembea nchi nzima wakinadi baadhi ya mawaziri wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete jambo ambalo lilisababisha Nape kuitwa Vuvuzela.

Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini amelieleza bunge kwamba, wabunge wote wanaounga mkono bunge kutooneshwa moja kwa moja na hata kusababisha mtafaruku bungeni wanahojiwa na Kamati ya Maadili ya Bunge.

Nape amesema kuwa, wabunge kwa pamoja walisomama na kupinga hatua ya serikali kuzuia matangazo hayo lakini cha kushangaza wengine wamegeuka.
 
Andika habari inayoeleweka unakimbilia wapi
 
Nape sasa kaamua kuja kivingine anamchukua viti maalum mpaka Guest house wanakaa wee huko anamfundisha kukariri kuwa Bunge live ni sumu kwa ccm hivyo wakiingia ndani wakatae live kwa nguvu zote, mfano yule viti maalum wa jana katoka Guest kakimbilia bungeni kuropoka pasipo kutafakari kwanza, Yaani Akili za kuambiwa hakuchanganya na zake kabsa,
 
Mkweli mkuu ila kwa hili nape kachemka aisee
kufa kufaana sasa nape anatumia Neno live kuchepuka na wale ambao wanataka wafundishwe jinsi ya kupinga live hadi Watanzania wakubali, mfano ni yule Mbunge wa viti maalum wa jana.
 
Mmh ilikuwa inakuja vzr baadae umevuruga,ila nimeibeba baadhi ya mawazir wa JPM ni lumbesa sio mizigo tena.
 
Mtoa mada na wachangiaji siwaelewi, mliangalia bunge hiyo Jana wakati wabunge na nape wanatoa hoja hizo
 
Kwa mtizamo wango nilivyomuelewa mleta Mada ni kwamba alitaka kumwambia Nape juu ya kile alichokuwa akifanya pindi wakiwa na Kinana kwenye majukwaa kilikuwa ni sawa na yeye kwa sasa, Yaani walizunguka wakiwalaani mawaziri mizigo hadi wengine wakajiuzulu, sasa inaelekea na yeye ni Waziri mzigo kutokana na kutokwenda na kasi ya Magufuli kabakia kushinda Guest kuwafunda Viti maalum wakatae bunge kurushwa Live wakihofia kujulikana mapungufu yao kwenye kujenga Hoja kama mfano tulioshuhudia jana kutoka kwa viti maalum wa Musoma .
 
Mmh ilikuwa inakuja vzr baadae umevuruga,ila nimeibeba baadhi ya mawazir wa JPM ni lumbesa sio mizigo tena.
lumbesa tafasri yake ni mzigo uliopitiliza zaidi na zaidi kwa maana kwamba Nape ni Waziri mzigo kuliko wale wa awamu ya Kikwete.
 
Cyber crime
 
ila bajeti yake imepita sasa kuangukia pua vp
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…