Mhh hawa waandishi wetu nao wana matatizo....sipingi maandishi yako hapa nakubaliana nayo.lakini Mheshimiwa ikitokea suala hili likapendekezwa chamani kwako hapo baadae uko tayari kugombea uraisi?Sijawahi kusema sina nia na wala sijawahi kusema nina nia. Huyu mwandishi kaandika maoni yake au hakuelewa hotuba yangu Kibondo.
zitto,
je una lolote la kusema kuhusiana na kauli yako uliposema kwamba 2010 hautogombea ubunge na utarudi shuleni ??
Nilisema sitagombea ubunge mwaka 2010. Bado ninasimamia maneno yangu mpaka sasa. Sijabadili msimamo huo. Nilisema pia katika mahojiano haya na mwandishi huyu
http://allafrica.com/stories/200803311770.html
Ninapata hisia kuwa kuna watu wanachuki zisizothimilika dhidi yangu na wapo tayari kupick chochote ilimradi kuonesha chuki zao. Sina cha kuwafanya..... ipo siku watagundua kuwa wananionea tu na wataacha chuki zao.
Mkuu Zitto,
Heshima kwako mheshimiwa sana, unajua nina ile video ya siku ya Lowassa na I am down na hotuba yako on it ambayo ni nzito sana, now naomba kusema hivi:-
1. Wewe ni politician, mwenye all credentials, kilichobaki sasa hivi wewe ni kusonga mbele tu na sio kurudi nyuma, a good politician ni yule ambaye ana priorities zake straight na hana tatizo kuzisema kwa wananchi, badala ya kuficha ficha kwani unaua mtu kwa kusema kuwa ungependa kuwania urais one day?
2. Nimekusikia mara nyingi sana ukipoteza muda wako na the so called maadui zako, kwa kweli sielewi why unapoteza hata muda kuwafikiria, I mean wanachi ni wananchi, kiongozi ni kiongozi ni vitu viwili ambavyo haviwezi kuchanganywa katika mawazo ya binafsi, sio kila zuri kwa the future ya taifa linaweza kueleweka kwa wananchi kwa urahisi ingawa linakuwa clear kwa kiongozi yule, sasa sio maaamuzi yote mazuri kwa taifa yataonekana mapema kama yalivyo na hili lako na urais sio rahisi kueleweka na wananchi wote kwa wakati huu, lakini as the time goes by litaeleweka wakati wewe ukiwa unasonga mbele na your dream!
3. It is about time sasa Tanzania tukawa na viongozi wenye angalau dream ya kuwa rais one day, kwa sababu tatizo la kuwa na marais kama Mwinyi na Mkapa, ambao hata siku moja hawakuota kuja kuwa, tayari tumeyaona lakini kwa sababu hakuna anyejali kuweka history chini accademically tunaishia kualumu tu na kulala, badala ya kutafuta means za kuzuia isije tokea in the future kwa kuandika vitabu na kusema ukweli kuwa urais sio lelemama, na kupata urais bila hata kutegemea inaweza ikawa tatizo sana kwa kiongozi.
4. Ni sisi tu wabongo na waaa-Afrika kwa ujumla ambao hatuwezi-predict nani anaweza kuwa rais in the future, lakini kule US kuna vitabu vya history ukiangalia utaona miaka 30 iliyopita kati ya wale waliokuwa predicted kuwa huenda one day watakuwa marais wa US, picha ya Bill Clinton imo, ukitembelea White House, kule West Wing kuna mahali kuna hizo picha za watu 50 na guess what? Bush senoir yumo pia, sasa kwa nini Tanzania iwe tatizo? Kugombea urais kwa nini iwe kitu cha kuficha?
Kwa kumaliza mkuu, ninasema hivi kuwa wewe endelea na your dream, hakuna kosa wala dhambi for that, wananchi ni wananchi ila kama kweli una hiyo dream, please achana na "maadui" ambao hawatakuja kunyamaza hata useme nini wewe ni ku-work on your dream mengine yatajiweka sawa yenyewe in the process, hapa Jf kuna watu wame-specialize na kushambulia tu tena ukiwasikiliza sana kuna wakati hata wanajishambulia wenyewe bila kujua jana walisema nini, na beside ndo hasa nia na madhumuni ya siasa za online,
ni wananchi wengi walio nje ya nchi, ambao hawaguswi na hata tatizo moja linaloendelea bongo, ndio maana wengine hata views zao on our nation huwezi elewa waliondoka lini bongo na watarudi lini pia, lakini ninakuhakikishia kuwa ukinaglia kwa makini hapa utaona tena vcery clear wanaoandika wakiwa bongo na wanaoandika wakiwa bongo, spirit ya lugha zetu hazifanani, wengi wetu walishakata tamaa hata ya kurudi nyumbani, na wengine hawajawahi hata kurudi nyumbani toka waondoke, wengine utaona wazi kuwa wamejifunzia siasa humu humu JF, sasa achana na watu, kuna ushauri wa maana kwako ambao unaweza kuuchota hapa, lakini negativity ziache hapa hapa mkuu!
Ninakutakia mafanikio mema mkuu huko mbele ya safari, na ninakuhakikishia kuwa tuko wengi ambao tuko njiani sio peke yako tu mwenye hizo dreams, nas hatuna hata uoga wowote kuzisema wazi hapa! Hao waandishi wanakutakia mema tu wewe ni kutowaogopa ni kusonga mbele tu na wakati ukifika ni kuugombea tu kwani tatizo ni nini?
Lakini kama hujasema inaeleweka, huenda kuna wananchi wanajaribu kukupa motisha mkuu!
Ahsante Mkuu!
Hizo siasa za zamani za kuogopa kuonesha ambition yako. Urais siyo ufalme ambao mtu anaogopa kusema anautaka. Alichofanya Zitto ni kujisababishia standard ya pekee na kuangaliwa na watu kwa ukaribu zaidi. Amejiweka ili achunguzwe na kupimwa. Haya mambo ya kudanganya ati watu hawautaki Urais lakini zikitolewa fomu wanakuwa wa kwanza kuchukua tena kwa mbwembwe yamepitwa na wakati.
Kama kuna mtu anafikiria kuwa Rais mwakani na ajulikane hivyo. Kinachonishangaza ni kuwa ilipoandikwa taarifa ya gazeti la Raia Mwema wiki chache zilizopita na watu waliojipanga Urais hakuna mtu aliyesema neno. Wao wenyewe hakuna aliyekanusha kuwa si kweli wanautaka Urais. Soma HAPA
Kama kuonesha nia ya kuutaka Urais ni kosa kubwa na vibaya watu kujua unautaka Urais mbona leo tuna Rais ambaye alijulikana ana utaka? Au kwa vile kasema Zitto kwa vile tunamjua na ni bwana mdogo na kama utani tunamuita "kijana" (kweli ni kijana lakini imetumika with contempt) basi hastahili kusema nia yake?
Urais ni nafasi ya kuwatumikia wananchi wenzako na Taifa lako na hakuna aibu wala kumfanya awe duni ati kwa sababu ametamka kuwa wakati ukifika angependa kufanya hivyo. Tuje na chuki nyingine lakini hizi za kwa vile Zitto kasema lililomoyoni mwake hazina msingi, kwani kuna baadhi ya watu hapa Zitto hawezi kusema lolote zuri, hawezi kufanya lolote jema, na hata kama ana mawazo yoyote basi asiyatoe kwa vile anaweza "kuchemsha" na kuwatibua wataalamu wa JF!
Kwa hili ni ninyi mmechemsha, leteni hoja nyingine, kijana ana haki zote kama Mtanzania yeyote na kama atakuwa na sifa zote za kuwa Rais basi hakuna kitakachomzuia..! and he'll have my full support if he wants to! Na hilo applies to anybody else who would dare to declare his intention na tutaangalia rekodi yake.
Binafsi nampongeza Mhe. Zitto kwa kusema alilonalo, na hivyo kutupa nafasi ya kumuangalia na kumsaidia asianze kufungwa fungwa na mafisadi, na hivyo amejiweka mwenyewe kwenye chekecheo la wakosoaji na tutampima na kumjaribu kama kwa moto na akipita salama itakuwa fahari kumuona akiapishwa kuwa Rais wa Jamhuri yetu! Yes I said it!
Zitto,
Msaidie kumuelimisha mshabiki wako huyu kwani nae ni miongoni mwa "walioamini" kuwa umesema na akaanza ku spin it to ur favor.... kibubusa as usual of course!
...sio kweli na hakuna kitu kama old and new politics!!! ish, politics ni politics tu........kuna wengine wanadhani wanakusaidia kumbe ndio kwanza wanakupotosha!! soma vizuri maelezo ya Kitila Mkumbo (nadhani mnafahamiana vizuri) jamaa ni real na ktk hili kasema ukweli bila spins!!!
asante.
Sikutamka kamwe kuwa nina nina ya kugombea Urais nilipokuwa Kibondo katika mkutano wa hadhara na wala sijafanya majadiliano yeyote na mwandishi wa PST pale Kibondo
...Masuala ya BIG POTATO sikuyasema na wala hiyo si lugha yangu. Sijawahi kutamka neno hilo Big Potato katika maisha yangu ya kisiasa. Kwanza ni neno ambalo ni kinyume na IDEOLOGY yangu. Eti Nataka kuwa Big Potato? Ujinga kabisa..... haya ni maneno ya vipetty bourgous ambao wanaona uongozi ni kama chanzo cha maisha ya kifahari.
Sijawahi kusema sina nia na wala sijawahi kusema nina nia. Huyu mwandishi kaandika maoni yake au hakuelewa hotuba yangu Kibondo.
Wana JF,
Sijawahi kusema sina nia na wala sijawahi kusema nina nia. Huyu mwandishi kaandika maoni yake au hakuelewa hotuba yangu Kibondo.
Wengi waliochangia hapa waliamini moja kwa moja kuwa maneno hayo niliyasema na kuweka hitimisho zao bila hata kunisikiliza ilhali mimi ni mwanaJF na huja hapa mara kwa mara. Ninapata hisia kuwa kuna watu wanachuki zisizothimilika dhidi yangu na wapo tayari kupick chochote ilimradi kuonesha chuki zao. Sina cha kuwafanya..... ipo siku watagundua kuwa wananionea tu na wataacha chuki zao.
.
...sio kweli na hakuna kitu kama old and new politics!!! ish, politics ni politics tu........kuna wengine wanadhani wanakusaidia kumbe ndio kwanza wanakupotosha!! soma vizuri maelezo ya Kitila Mkumbo (nadhani mnafahamiana vizuri) jamaa ni real na ktk hili kasema ukweli bila spins!!! asante.
... Hivyo mkuu iwe umesema au hukusema usione vibaya kwani wapo kina Steve Harper ambao leo ni waziri Mkuu wa Canada alikuwa na ndoto kama hizi toka zamani, na he made it iwe ilikuwa ambition ama vision iliyomsukuma bado matokeo yameweza kufikiwa. and he worked hard for it!..
...kama wewe!Hii mada ni ya siku nyingi.....
Nilisema sitagombea ubunge mwaka 2010. Bado ninasimamia maneno yangu mpaka sasa. Sijabadili msimamo huo. Nilisema pia katika mahojiano haya na mwandishi huyu
http://allafrica.com/stories/200803311770.html
nilijua tu utakuwa humugo zitto go