Naombeni ushauri nataka niwe nawahi kuamka

Kwa muda mrefu sana nina tatizo la kuwahi kuamka asubuhi, Kwa kawaida hua naamka saa nne na nikiwahi basi ni saa mbili, Nawekaga alarm saa 11 asubuhi lakini hua naishia kuipuuza, sina mwajiri wa kuniwekea mashart niingir kazini saa ngapi, Nimejiajiri so hususan sekta ya kulimia watu mashamba kwa trekta nililokodisha so mimi hua naendaga kucheki progress ya vijana niliowaajiri huko shambani weekend maana ni mbali na ninapoishi hapa town...Naombeni ushauri wenu nitumie mbinuz zipi niwahi kuamka
Huna kazi za kutosha mkuu
Hata nilale saa kumi asubuhi saa kumi na moja nshaamka
 
Ukiamua unaweza
Jiweke mazoea

Nilikuwa na mazoea ya kuamka saa 12 piga ua lazima mda huo ukifika nitakuwa macho

Ikafika kipindi mazoea ni kuamka saa 3 ,piga ua siwezi kuamka mapema mpaka saa 3

Niliweka mazoea nalala saa nane hili jambo lilinisumbua sana ,kila nikitaka kulala saa sita,saba au tano siwezi mpaka saa nane ndio usingizi huja

Kila jambo ni kuamua na mazoea ,ukiamua saa 11 uamke utaamka

Moyo ni kama mtoto mdogo ukimdekeza na kumzoesha ndivyo hivyo atakapodeka na kuzoea ,kama umeudekeza moyo na hujaamua haki ya mungu alarm utakuwa unazima kila siku

Konda analala saa 5/6 anaamka saa kumi

Amua ,jizoeshe ,ukishaamua kila siku mda huo utakuwa upo macho
Sio Moyo mkuu ni Ubongo/Akili.
Kiukwrli mm siwez kulala bila saa nane au tisa na kuamka ni saa2
 
Kwa muda mrefu sana nina tatizo la kuwahi kuamka asubuhi, Kwa kawaida hua naamka saa nne na nikiwahi basi ni saa mbili, Nawekaga alarm saa 11 asubuhi lakini hua naishia kuipuuza, sina mwajiri wa kuniwekea mashart niingir kazini saa ngapi, Nimejiajiri so hususan sekta ya kulimia watu mashamba kwa trekta nililokodisha so mimi hua naendaga kucheki progress ya vijana niliowaajiri huko shambani weekend maana ni mbali na ninapoishi hapa town...Naombeni ushauri wenu nitumie mbinuz zipi niwahi kuamka
Cha msingi uwe una make sure unalala mapema, pía tafuta shughuli nyingine ya kufanya siku za wiki, maana hata ukisema uwe unaamka Mapema alafu huna cha kufanya utatamani kuendelea kulala tu, cha msingi ongeza mradi mwingine
 
Ni vizuri kujifahamu, either you are a night or morning person.
Pengine ni mtu wa usiku zaidi kwa hiyo unachelewa kulala na kuchelewa kuamka. Na kama ni hivi basi inakuwa ngumu kwako kulala mapema hata kama unapenda.

akipewa appointment ya kula mzigo saa 1 asubui mbona 11 atakuwa macho

hajapata reason ya kuamka mapema
 
Back
Top Bottom