kwanza nianze kwa kukupa pole, una mtihani na wakati mgumu kwelikweli! wengi wa wakwe hasa kina mama mara nyingi wanangalia mapungufu ya wake za watoto wao, na pengine kukuchongea kwa mumewe! nina mifano kadhaa ambayo mama mkwe amesababisha mifarakano, ugomvi hasa pale mke anapokuwa na misimamo ktk ukweli, wengine ndoa zimevunjika. sikutishi dada yangu, ila unatakiwa uishi kwa akili sana na mama mkwe, huku ukimsoma mumeo yupo upande gani maana damu ni nzito kuliko maji! ila umshauri mumeo amjengee mama yake mapema ili kuondoa mitafaruku hapo kwenu, kama atakuwa ana shd mtakuwa mnamsaidia akiwa kwake, au kumtembelea mara moja moja kuliko kuishi naye ni tatizo zaidi! hata kama hajiwezi bora kumpangishia rum akiwa na msaidizi kwa kweli! vinginevyo uvumilivu wako ndo kuishi kwako kwa amani