Hyrax
JF-Expert Member
- May 20, 2023
- 860
- 2,305
Wakuu salaam, Naomba ushauri wenu aisee maana ni wiki sasa najaribu kudadavua kipi ninunue kati ya Bajari au Gari aina ya IST kwaajili ya biashara ya huduma ya usafiri hapa mjini kupitia Bolt na Uber, mbali na hilo ntakuwa nafanya mishe zingine kupitia chombo nitakachonunua sasa naomba wenye uzoefu wa hizi mishe kipi nianze nacho na kitakachonipa faida endelevu, uzuri nitakuwa naendesha mwenyewe maana sina mishe nyingine hapa town kwasasa. ushauri wenu ntaupokea na kuwashukuru. asanteni