Bushmaster
JF-Expert Member
- Jan 18, 2022
- 542
- 1,178
Kama hujamuoa bado ni mpenzi wa wote,kwahyo hapo inapigwa gombania goli ataemuwahi ndio huyo huyo,
kwa kifupi tuu kwa sisi wazoefu hizi ni dalili za kuachwa hivyo hapo unaandaliwa kisaikolojia taratibu hivyo ukiona hivyo tambua kuna siku haina saa wala dakika utaanza kuona mabadiliko ya tabia .Kama kijana wa 2001 unaweza kupangilia maandishi hivi basi ni imani yangu kubwa una uelewa mzuri na hiki nachotaka kukwambia utakishika na kukielewa. Kwa sasa hivi kinachokusumbua ni mindset yako ukiamini unapendwa lakini kiuhalisia huyo tayari ni mke wa mtu kilichobaki ni kuhalalishwa tu. Hata usipomwambia leo aolewe nakuhakikishia hautazidi mwaka utaanza kuziona rangi huzielewi.
Sasa unachotakiwa kufanya punguza mazoea ikiwezekana hata mbususu usiiguse kama utaweza mwambie akaolewe na Eng, nakuhakikishia baada ya kumwambia ivyo atakulilia machozi na kuja na zile kauli za wanaume ni mbwa usitetereke umefanya jambo zuri kwa ajili yenu wote. Sasa katika hiki kipindi hiki ndio utajua mwanamke ni mtu wa namna gani. Hakikisha haumgusi au kuwa karibu naye utajiepusha na mengi sana.
Naomba niishie hapo naamini umenielewa. Mke wa mtu sumu
We jamaa una chaiWakuu nipeni ushauri mdogo wenu.
Nipo kwenye mahusiano na huyu binti kimsingi tulianza mahusiano kipindi nipo mwaka wa kwanza chuoni (hivi sasa nipo mwaka wa pili), lakini yeye tayari hivi sasa kamaliza masomo na yupo nyumbani (amesoma Diploma ya clinical medicine).
Lengo la mahusiano yetu ni badae tuanzishe familia kwa pamoja (kufunga ndoa).
Umri wake ni mkubwa kwangu, ananizidi miaka miwili mimi ni wa 2001
Ni zaidi ya mara nne sasa huyu binti ananambia kuna wanaume ambao wana muapproach kwaajili ya kumuoa, hata rafiki zake wa kike mara nyingi huniambia kuwa huyu binti ana windwa na wanaume wengi tena ambao wapo seriously na wenye maisha yao.
Ofcourse hata mimi naweza ku confirm hicho kitu, maana she is beautiful pia ana akili na ufahamu mzuri, she is completely a wife material.
Jana usiku amenitumia screenshot za chating za jamaa ambae ni engineer, jamaa anamwambia kabisa anataka kumuoa mwakani na yupo serious.
Ugumu unakuja hapa, mimi bado nipo chuo tena maisha yangu ni kawaida sana, na nyumbani kwetu hali si nzuri hata kidogo, kiufupi bado nina safari ndefu sana ya kujitafuta kimaisha.
Naona kabisa huyu binti nitamchelesha kwenye maisha anayotaka, na yeye anajua hali yangu hiyo. Natamani kumwambia akubali hao wanaomchumbia lakini sijui atapokea vipi, mana tunapendana, na mimi ninapotazama safari ya maisha yangu bado naona ukungu na giza kubwa sana.
Sitaki kumzibia riziki huyu binti, najua ananipenda na mimi pia nampenda sana.
Hapa nipo njia panda, sijui nifanye maamuzi gani kwa manufaa ya kila upande.