Naomba Mungu Watu wema wasiuawe Kwa Kusingiziwa Ujambazi au Majibizano ya Risasi

Kwa vyovyote vile ! Naunga mkono hoja ya Rais na ujumbe alio utoa siku ile ! Lakini pia naunga mkono andiko la mtoa mada !

Kama una mtoto wako ni askali , ukisikia ameenda kupambana na jambazi , presha unayopata ni wewe pekee unaweza kuielezea ! Katika muhtadha huo , utaomba tu wam - ny'ang'anye haraka !

Lakini kwa upande wa pili , ukiwa na mtoto ambae unajua sio jambazi , na ukasikia kazungukwa na polisi , ungependa usiwe na shaka kuwa atanyang'anywa haraka ' siraha ' ambayo HANA !

Nategemea GT waelewe naposema nawaunga mkono Mheshimiwa Magu na mtoa mada
 
Wewe ni jambazi hofu ya nini?
Wale wafanyabiashara wamadini kutoka ulanga waliouwawa na zombe akasema walikuwa majambazi jee ni kweli walikuwa majambazi?labda ikutokee kwa ndugu au rafiki yako ndipo utakapomuelewa mleta uzi
 
We piga kelele, lakini polisi hawaendi bila full information. Kama ni kundi lako jipange.
Umeongea point kaka me cjui hata anacholalamika coz Police sio wajinga na kama ni jambazi na unamiliki siraha kinyume cha sheria kwa nn wasikukamate kwa tahadhari!!
 
Hii Tabia ya Polisi Kwenda Majumbani kwa Watau wakidai kwenda Kuwakamata bila hata watu wenyewe kuwa na Taarifa, na Pia Bila Polisi wenyewe Kuwa na Uniform, Nembo, pamoja na Gari za Jeshi la Polisi huku wakiwa na Silaha nzito. Na Kauli ya Kunyang'anganya Majambazi silaha haraka haraka.

Naomba Mungu isitumike kuuwa watu kuwasingizia ujambazi au majibizano ya Silaha Kama ilivyowahi Kutokea huko nyuma. Mauaji Mengine ambayo yalikuwa na Sura za Kisiasa.

Mimi Nashauri Hii Tabia ya Polisi, Kuzingira Nyumba za Watu mathalan wanasiasa nk watu ambao unaweza kuwapigia simu na wakaja kituoni, hii Tabia itakuja Kutoa Mwanya wa Watu kudhulumiwa Uhai wao Kinyume na Matakwa ya Serikali, Na Baadaye Serikali na Watanzania tutaletewa habari za Kupikwa. Najua asilimia kubwa ya Askari Polisi wana Utu, Nidhamu na Uaminifu, lakini hilo lisitupe imani ya Kutengeneza mianya ya hujuma.

Kama Mtu Sio Jambazi, Hajamdhuru yeyote Kimwii, Sio Gaidi, Mnajua jinsi ya Kuwasiliana naye, ACHENI KUZINGIRA NYUMBA, NA OFISI ZA WATU, AU KUFUKUZA GARI LA MTU AMBAYE HATA HAJUI KUWA ANAHITAJIKA NA POLISI, HUKU WANAOMFUKUZA HAMNA HATA UNIFORM, HUKU NI KUJENGA MAZINGIRA YA MAUAJI NA BAADAYE TUTALETEWA HADITHI ZA AJABU, "LILIKUWA JAMBAZI, AU KAMA NI MTU ANAJULIKANA, TULIENDA NYUMBANI KWAKE, WALINZI WAKE WAKATUSHAMBULIA KWA RISASI, LAKINI KWA BAHATI MBAYA RISASI MOJA IKAMPATA YEYE, NA TUNAWASHIKILIA WATUHUMIWA WAWILI WANAOSADIKIWA KUWA WALINZI WAKE, PICHA ZAO HIZI HAPA"

bushmen.hunters.558x842.jpg


Nilihisi Kabla ya Uchaguzi kuwa Tabia na Kauli za Ukiua Jambazi, Hakuna hatia wala Uchunguzi ni za Hatari. Kwamba Nataka Jambazi akivamia mahali na silaha asikabiliwe hapana, Nia yangu Sitaki hii iwe nii Kauli Mbiu au Operesheni kama ya "Tokomeza" Ambayo itatumiwa kwa Kisingizio. Au na Watu wenye Nia mbaya ya Kuangamiza Maisha ya watu fulani. Sijakurupuka na Kusema haya yameshatokea Mara Nyingi.

sasa kama wamepata taarifa za kiitelejensia kua ww ni jambaz na una siraha unataka waje kukukamata kwa kukupigia magoti?? mkuu maoni yako yanatia shaka inawezekana na ww ni m1 wao!!
 
Back
Top Bottom