Naomba msaada wenu wakuu.

Choo bora hicho wenzio wanakunya ziwani kama huamini waulize Wakurya
Ni kweli mkuu lakini nikipiga picha namna mazingira yanakuwa kipindi cha masika ni hali mbaya
 
Sasa choo tu unaomba msaada nyumba utaweza kujenga kweli wewe, hebu ondoa hiyo mentality ya kuomba omba.

Hicho choo kikawe chachu ya wewe kupambana na kupata maokoto ya kuweza kuboresha mazingira ya hapo kwa bi mdashi
 
Sijui nitaonekana namna gani lakini ki ukweli.....kuomba omba ni mlango wa udhalili......kuwa mwepesi wa kuomba omba kunaondoa utu wa mtu.....juu ya mgongo wa ardhi changamoto ni nyingi na kila mmoja anapitia za kwake mpaka mwisho wa dunia....lakini pia neema ni nyingi na kila mtu ana za kwake kulingana na anavyoziona na kuzithamini neema zake........

Na kamwe hauwezi kuziona Neema na utukufu wa Mungu maishani mwako kwa kuzitazama Neema za wengine bali neema zako kwa wakati huo......

Lakini pia kwenye safari ya maisha mambo huenda hatua kwa hatua ikiwa jitihada zinafanyika za kutoka hatua moja kwenda nyingine.......

Kwa hali ya choo chako na makazi yako sio mazuri sana lakini pia sio mabaya sana.....hivyo basi kwa mtazamo wangu ungetakiwa utie bidii kwenye kutafuta kazi ili taratibu uboreshe hali ya maisha hapo kwenu

Sote tunatambua kuwa mambo ni tight lakini kuomba msaada iwe mambo ya dharula yale kibinadamu
 
Habari za muda huu, natumaini mpo salama wote. Nina shida ya kiasi Cha fedha kwa ajili kujenga choo bora hapa nyumbani. Ni miaka mitatu sasa najitahidi kufanikisha jambo hili lakini naishia kushindwa. Sababu kubwa ni kwamba kiasi cha pesa ninachokipata katika kazi ndogo ndogo za kila siku kinaishia kufanya marejesho ya mikopo ambayo namsaidia mama yangu kuilipa. Ni mikopo ya muda mrefu na imekuwa ikinichanganya sana hasa kila mgambo wakitumwa kumchukua mama kwenda naye ofisi za kata kila mara. Hiking kitu kimefanya niendelee kulipa marejesho kila siku ili kupunguza ukali wa hayo madeni.

Mimi ni kijana wa miaka 26 na ni miaka mitatu sasa tangu nimalize chuo kikuu. Naishi nyumbani na mama yangu na wadogo zangu wawili na ninatamani sana kuondoka hapa nyumbani kabla ya mwaka huu kuisha.

Naomba sana msaada wenu wakuu wa pesa niweze kujenga choo hapa nyumbani kabla ya kuondoka, maana kipindi Cha masika huwa mateso sana kutumia hiki choo. Ni ndoto yangu kuondoka hapa nyumbani angalau nikiwa nimeacha mazingira mazuri kwa upande wa choo.

Picha za choo tunachotumia Kwa sasa
View attachment 3106287View attachment 3106288View attachment 3106291

Namba yangu ni 0672569461 TIGO PESA
Jina YONA.

MUNGU AWABARIKI.
Pole sana , madeni unayolipa kama yalikopa Kwa ajili ya elimu yako hauna budi kuyalipa , ila kuhusu choo kipindi Cha masika ni kinajaa maji au vipi .
Kama ni kujaa maji inulia udongo kutoruhusu maji kuingia kwenye shimo na uezeke hata bati 4 . Mengine yatakuja huko mbeleni maana choo ujenzi wake kuanzia kuchimba choo adi umalize unaweza Kuta m 3+ zinapotea.
 
Habari za muda huu, natumaini mpo salama wote. Nina shida ya kiasi Cha fedha kwa ajili kujenga choo bora hapa nyumbani. Ni miaka mitatu sasa najitahidi kufanikisha jambo hili lakini naishia kushindwa. Sababu kubwa ni kwamba kiasi cha pesa ninachokipata katika kazi ndogo ndogo za kila siku kinaishia kufanya marejesho ya mikopo ambayo namsaidia mama yangu kuilipa. Ni mikopo ya muda mrefu na imekuwa ikinichanganya sana hasa kila mgambo wakitumwa kumchukua mama kwenda naye ofisi za kata kila mara. Hiking kitu kimefanya niendelee kulipa marejesho kila siku ili kupunguza ukali wa hayo madeni.

Mimi ni kijana wa miaka 26 na ni miaka mitatu sasa tangu nimalize chuo kikuu. Naishi nyumbani na mama yangu na wadogo zangu wawili na ninatamani sana kuondoka hapa nyumbani kabla ya mwaka huu kuisha.

Naomba sana msaada wenu wakuu wa pesa niweze kujenga choo hapa nyumbani kabla ya kuondoka, maana kipindi Cha masika huwa mateso sana kutumia hiki choo. Ni ndoto yangu kuondoka hapa nyumbani angalau nikiwa nimeacha mazingira mazuri kwa upande wa choo.

Picha za choo tunachotumia Kwa sasa
View attachment 3106287View attachment 3106288View attachment 3106291

Namba yangu ni 0672569461 TIGO PESA
Jina YONA.

MUNGU AWABARIKI.
Unataka pesa tu au tukija na matofali na simenti angalau tukujengee cha pasipoti saizi utatupokea? Au tukianzisha mnada humu wa kuiuza simu yako tupate kiasi chapesa huenda na ziada utakuwa tayari.
 
Msaada utapata wala hilo usijali,

Mtu akiomba msaada anapondwa na kusakamwa! akiiba utasikia ''Si bora hata angeomba''

We make a living by what we get,but we make a life by what we give.
 
Umemaliza kila kitu. Kuomba msaada iwe ni kwa mambo ya dharura kama ugonjwa, ukosefu wa chakula; na mengine yenye uharaka sana. Vinginevyo mtu unaweza kujikuta kila kitu unaomba omba tu.

Halafu katika dunia hii kila mtu ana matatizo yake; sema tu wengi wetu tunapambana nayo kimya kimya. Tusipende kuomba omba sana hasa kama shida yenyewe si ya dharura kivile maana tunaweza kuishia kujitwezea utu wetu!
Mkuu,hicho choo anasema kinajaa maji wakati wa masika,hivyo kinakua ni hatari kwa wakazi wa hapo home kwao,
Huoni kua Choo cha hivyo kinaweza kusababisha wakazi wake kupata maradhi?

Mleta mada ameamua kuomba msaada wa kurekebisha choo kabla hakijawaletea maradhi ambayo wewe unataka akipata maradhi ndio aombe msaada!
 
Unataka pesa tu au tukija na matofali na simenti angalau tukujengee cha pasipoti saizi utatupokea? Au tukianzisha mnada humu wa kuiuza simu yako tupate kiasi chapesa huenda na ziada utakuwa tayari.
Hapana sio pesa tu mkuu hata msaada tofauti na pesa unaoweza kusaidia ujenzi huu.
 
Yaani unaomba msaada wa choo ee.. yaani unajali sana kunya kuliko maisha
 
Hiyo mentality itakuumiza sana mkuu. Sehemu kama JF suka uzi ukiomba kazi au fursa ya kukuingizia kipato au elezea kile unachoweza kufanya ili watu wakupe nafasi ufanye upate pesa.

Hauna uwezo wa kutatua changamoto za nyumbani omba njia ya kukusaidia kujenga uwezo wa kutatua changamoto hizo.

Changamoto zote ulizoelezea SULUHISO lake ni PESA.

Na wewe tatizo lako siyo pesa bali ni uwezo wa kutengeneza pesa.

Focus hapo upate suluhisho.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom