Naomba msaada wenu, nahisi kuchukua maamuzi magumu

sam green

Senior Member
Feb 21, 2020
183
269
Habari zenu, naombeni ushauri hata kunichangia hata mawazo niondokane na hili, jambo.

Nilikuwa na mpenzi wngu tumedumu kwenye mahusiano miaka mitatu, hatimae mwaka huu mwezi wa 2 kaniacha kisa kupishana kidogo tu.

Nahisi kufa na kuchukua maamuzi magumu, mapenzi yananiumiza sanaaa, mipango mingi tulipanga mengi tumeyafanya, mengi mno.

Nikikumbuka tu kidogo naishia kulia haijalishi niko wapi. Hata kazini tuu nikimuwaza kidogo tu naliaa, kubwa zaidi kinachoniuma ktk mahusiano yetu, mpenzi aliwah kuwa na mahusiano ya Siri na mtu flan nikagundua, akaomba msamaha yakaishaa.

Hivi sasa nimeona ndio wamerudiana tenaa kama walivyokua, naumiaa sana, usingizi sipati. Nimekuwa mtu wa hvyoo muda wote hasa muda tukiokaaa, mambo tuliyopanga, vitu tulvyofanyaa, na huyo mwanamke nilimpangia Chumba sehem, lakini yaliyonisibu nahisi nimebaki peke yangu. Dunia yotee.
😭😭😭😭😭
 
Post yako iliyopita ulitudanganya. Nanukuu

"NB: Baada ya kugombana nae, nilimwomba anipe kitu kimoja kati ya tv na sabufa yeye alinipa tv, ni vitu vingi nimenunua nimemuachiaa nikaamua kukaa kimya.

Lakini mpaka sasa najiona nimejipunguzia mzigo, maan sasa hivi sitoi tena hela za matumizi, kodi silipi, yaani pesa nayopata haina matumizi makubwa.

Naombeni ushauri wenu! Mawazo yenu, ila mimi nina imani tuu ipo siku atarudi kuomba msamahaa!"

Ushauri wangu ni huu.
Kijana ushajaa kwenye mfumo na inaonekana dhahiri bado wewe ni mgeni kwenye mapenzi. Unapotaka ushauri kuwa muwazi na mkweli ili upate ushauri kutokana na uhalisia wa mambo.
Ukilipita ilo salama rasmi utatakaswa kuwa mwanaume. Pole sana jitahidi ukubali uhalisia na umove on maana ukijifanya unajua kupenda sana utakufa kabla ya siku zako.
 
Asante kwa ushauri! .
 
Wa hivi huwa wana ongozwa na hisia kuliko akili.
Muacheni ajiue
 
Tangazo Tangazo ...nauza sum ya panya,mende,viroboto .

NB -: Na sum ya mapenzi ipo Ni ya kulamba lamba
 
Pole sana kila mwanaume amepitia hicho kipindi, kuna ambao walimuachia mwanamke kila kitu wakatoka na nguo zao tu wakaanza upya, na mengine mengi kila mmoja ameumizwa nina mengi ya kukuambia na natambua situation yako ila fanya hivi

1. Hama mtaa au nyumba unayokaa ambayo mpenzi wako alikuwa anakuja
2. Tafuta kitu kitakachokupa furaha tofauti na mapenzi
3. Futa picha zake zote, futa namba ya simu ya kwake ma marafiki zake na mu unfollow kwenye social network zote
4. Jitenge na watu wote wanaoweza kukupa habari zake
5. Ondoa kila kitu kinachomuhusu kwako kama mlikuwa mnaangali tv pamoja acha kuangalia vipindi mlivyokuwa mnaangalia wote, acha kusikiliza nyimbo azipendazo

6. Usipende kukaa peke ako tafuta marafiki nenda bar kunywa hata juice au soda rudi hm ukiwa ma usingizi jikeep busy bro

7. Kama ni mtu wa dini funga na kuomba naamanisha omba upate faraja ya moyo
Mungi ni pendo na anakupenda shetani anatumia mapenzi kuumiza vijana wengi sana soma zaburi ya 142 usiku huu

Not
Usiogope unachokifikiria kichwan kwako si uhalisia wewe ni wa thamani sana na kunawasichana wengine wazuri wanakupenda na kukungojea

Mungu akikuondoa mahali using'ang'anie anajua mawazo na amesikia maongezi yao mabaya ambayo wewe huyajui
 
πŸ’―
 
Kwanza mwanaume ukiwa na mwanamke inabidi mnaliana Timing kama kukata kichwa cha kobe, ukiona anaonesha dalili tu za kuzingua unawahi kumpiga chini wewe mapeema kabla ya yeye hajatamka,

Sasa dalili unaziona kabisa bado ulifumbia macho,

Enjoy Show Show sasa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…