Naomba msaada wa kilimo cha Azolla

Nsema

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
275
479
Ndugu wana Jf hasa jukwaa hili LA ujasiriamali na biashara.nilikuwa nauliza je ?

Je kilimo cha Azolla mbegu zake hupatikana wapi,na ukilima Soko lake likovipi.

Vipi General management yake ikoje?
 
Azona ni aina ya magugu maji ambayo yanaonekana kuwa na kiasi kikubwa cha protein 20-30%. Azolla hutumiwa kulisha wanyama, kuku na Samaki.

Hili ni zao ambalo linaweza kuzalishwa kwa urahisi sana maana linaitaji jua, mbolea na maji pekeake. (Ila sio direct sunlight)

Mbegu ni raisi kupata kwenye madimbwi. Kwa mfano mwanza azolla ipo sana kwenye vitalu vya mchele au madibwi. Ni kiasi cha kukusanya utakayoweka pata na kuweka kwenye eneo unalotaka kupanda na zitamultply kwa hraka sana.

Unaweza kulima azolla kwenye containers au madimbwi. Waweza tumia mbolea ya hydroponic, mbolea za chemicali na za asili.
 
Soko la azolla kwa Tanzania bado halijawa kubwa na linaweza kuwa halipo kabisa maana ni watu wachache sana wanaotambua umuhimu wake kwenye mifugo. Katika nchi zilizoendelea Azolla wamefikia kiasi cha kuzalisha mafuta (ethanal) kutumia azolla. Na mafuta hya yanatumika kwenye magar na hta kuzalisha umeme. Miaka inayokuja na technologia inavyokuwa zitatengenezwa mashine na magar ambyo yatatumia azolla fuel.

Ila kama wewe ni mfugaji ni vizuri ukajizalishia azolla kama chakula cha mifugo yako. Kwa mfano research zinaonyesha kuwa uzalishaji wa maziwa kutoka kwenye ngombe huongezeka mara dufu endapo ngombe atalishwa azzola vilevile hta kwenye ukuaji wa kuku na samaki azzola imeprove kuwa reliable source ya protein.

Kwa soko la kimataifa azolla inasoko kubwa sana. Kwa mfano USA Zinalimwa kwenye hi tech green house ili kutilize space.
So kma wataka zalisha azolla kwa sasa Tanzania unabidi uzalishe kwa ajil ya export na kumbuka quality na quantity kwenye international maket ni factor kubwa.
 
Magugu ya azolla kwa sisi wakulima wa mpunga sitaki kuyasikia kabisa, labda yatumike kwa shughuli zinginge, yanatupa shida sana Kwenye mashamba ya mpunga huku Kyela, yaliletwa na mkulima mmoja ambaye alilenga kuwa kutokana na kukua kwa kasi magugu ya azolla, kunafunika majani mengine na kuacha mpunga ustawi bila magugu. Lakini Matokeo yake ni kwamba kasi ya kukua kwa azolla ni kubwa sana ukilinganisha na ukuaji wa mpunga na Matokeo yake ikawa inatupa usumbufu kuyazoa na kutupa nje ya shamba.

Ila sikuwa najua kama yana matumizi mengine kama ulivyoandika mleta maada
 
Ndugu wana Jf hasa jukwaa hili LA ujasiriamali na biashara.nilikuwa nauliza je ?

Je kilimo cha Azolla mbegu zake hupatikana wapi,na ukilima Soko lake likovipi.

Vipi General management yake ikoje?
Ngoja kwanza nika-google hiyo azolla alaf nitarudi
 
Soko lipo kubwa sana, tengeneza chakula cha kuku uuze kama chakula cha kuku. Ukiitntroduce bidhaa mpya kwenye soko ukafanikiwa kuimarket vizuri unamonopolize soko!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…