Naomba kujuzwa faida za kuwa na GREEN CARD ya Marekani

Filip

Member
Dec 30, 2023
18
30
Wana familia wa JF,

Humu ndani naamini wapo Watanzania ambao wanaishi Marekani kwa nguvu ya GREEN CARD.

Kwa faida ya wengi, naomba yeyote anayejua au amefanikiwa kuwa na Green Card ya Marekani ni kwa namna gani imemsaidia kuishi huko USA na kwa namna gani imemsaidia kupata kazi nzuri na kuweza ku-make enough cash na kutimiza ndoto zake.

Pia naomba kufahamu changamoto ambayo mtu aliyeshinda Green Card anaweza kukutana nayo mara tu anaingia Marekani for the first time au nini afanye ili mambo yaende sawa.

Mwisho naomba kujua kama mtu akiacha mshahahara wa 3M Bongo akienda Marekani anaweza ku-make fedha ndefu zaidi na hasa akiwa na hayo makaratasi kwa maana ya Green Card au ndio inaweza kuwa anapotea kimaisha?

Natanguliza shukrani kwa wajuzi wa haya mambo na naamini mchango wenu utasaidia Watanzania wengi kufahamu kuhusu faida za kuwa na Green Card ya Marekani.

ASANTENI SANA 🙏🙏
 
Kwa haraka Green card means permanent residence au kwa kiswahili ni ukaazi wa kudumu.

Ambao kuna njia mbali mbali za kuupata kama kupitia.

Ndoa, Diversity visa lottery, kuishi USA kihalali kwa miaka zaidi ya mi5 nk.

Green card holders wana haki sawa au kuzidiwa kidogo na raia kamili wa marekani.

Ukipata Green card maana yake ushakua nusu raia wa Marekani kama ukitaka uraia kamili utapata after 5years baada ya kuwa na Green card, kama utakidhi vigezo na masharti yake.

Kufanikiwa baada ya Green card ni wewe mwenyewe sio guaranteed, ni wewe na kichwa chako na nini unataka ufanye huku US.

Anyway ni somo refu na pana pitia website ya migration ya US usome zaidi.
 
Green card kwanza ni Kibali kinakufanya uwe mkazi wa kudumu wa Marekani au kukuwezesha kuishi na kufanya kazi sehemu yoyote ndani ya Marekani kwa muda na wakati wowote kama raia wa nchi hiyo.
Hiyo faida yake kwanza.

Changamoto kwa mara ya kwanza utapewa ya miaka miwili then wataangalia utulivu wako then wakupe 10 years.

Kwa wale wanaotamani kupata kibali hiki, kuna njia ya kuwekeza walau pesa kwenye biashara biashara kule. Ufike hata m900 in a year.

Au ukalipa, pesa kadhaa ukiwa na mwanasheria.
Wengine through muajiliwa wako.

Going about work.

Kazi yako ya m3. Bongo hapa. Kama umenyooka kule kazi utapata pesa nzuri. Nenda kajipange then vuta familia.
 
Unapata Mshahara 3 M Kwa Mwezi, tena ukiwa homeLand..!

Sasa Kwenda Marekani Kufanya Nini tena? Au nimesikia Vibaya?

Chance Yako ya Kupata mtaji kupitia huo Mshahara ni Kubwa na Kuanzisha biashara saizi ya Kati au Kubwa unayo.

Hapa kunahitajika Ukombozi Wa Fikra tu...!
Asikudanganye mtu,hata Diaspora Wanatamani sana kufanyia maokoto wakiwa homeLand...! ndo kilio Chao Cha Kila Siku Serikali ilegeze Masharti waje Wafanye uwekezaji home..!
 
Ukiwa nayo, huna tofauti na mwenye uraia, ila hutaweza kupiga kura tu.

Mambo ya elimu, ada utalipa ya bei nafuu, tofauti na ile ya mwanafunzi anayetoka nje ya Marekani (international) ambayo ni aghali sana.

Nafasi ya uwekezaji, kununua nyumba, kuanzisha biashara unapata bila ya shaka.

Utaingia na kutoka marekani bila visa, yaani huna haja ya kwenda ubalozini, ni kama unatoka Dar kwenda Tanga.
Green card si sawa na uraia, hivyo hata Tz na uTz hutaupoteza.

Kwa Marekani uwezekano wa kutengeneza zaidi ya milioni 3 kwa mwezi ni mkubwa, na kadiri ya taaluma yako na kujiendeleza kielimu, ujuzi na uzoefu, ndio kipato kinaongezeka zaidi.

Unapokuja kwa mara ya kwanza ni lazima ufikie kwa mwenyeji, nafikiri hilo unatakiwa ueleze ukijaza maombi kama una mtu utakaye fikia kwake. Baada ya hapo hua haichukui muda kwa mgeni kupata kazi na kuanza kujitegemea mwenyewe.
 
Mkuu hakuna nchi nzuri duniani kama Tanzania blv or not...Tanzania ni nchi pekee ambayo kuna watu hawalali ili wananchi wake walale...sio kawaida kila siku unaamka unafanya shughuli zako salama..unarudi kwako salama tena kwa muda unaotaka...katika nchi ina uungwana Africa ni Tanzania.

Kwa Asia ni ni nchi nyingi wamejengewa ustarabu..:na heshima...South korea da best...America kama ukienda nenda kajifunze(exposure) then uje bongo ufanye investments...hii yanga mnayo iona sa hiv si bahat mbaya...yule Rais aisee IQ yake si ya kawaida nenden chuo flan hapo posta mkaulize taarifa zake.

He is not normal guy ever..,,na ametokea chin kabisaa..,njaa anaifaham, imagine b4 hajui kama atakuwa Rais...but kila mimba ya mtoto wake lazima wife akajifungulie America...very geniouz guy. Wewe unalipwa mil3 unataka ukimbilie USA usalama wako ni mdogo bna..
 
3 M kwa mwezi.

Yaani Laki moja moja siwe 30...

Au tuseme Msimbazi msimbazi ziwe 300.

Nikifanya Kazi miezi 60 nitakuwa nimeingiza Shing' 180,000,000.

Basi tuseme nimejibana bana nikatumia Milioni themanini ndani ya miezi 60.

Hapo nitakuwa na Millioni Mia moja net.

Huo mbona mtaji mkubwa sana..! Hata Mabenki Watakutamani Wakuongezee mtaji..! Tuliza akili, Fikiri Vizuri
 
Mkuu hakuna nchi nzuri duniani kama Tanzania blv or not...Tanzania ni nchi pekee ambayo kuna watu hawalali ili wananchi wake walale...sio kawaida kila siku unaamka unafanya shughuli zako salama..unarudi kwako salama tena kwa muda unaotaka...katika nchi ina uungwana Africa ni Tanzania...
Duh subiri nim google Eng
 
Wana familia wa JF,

Humu ndani naamini wapo Watanzania ambao wanaishi Marekani kwa nguvu ya GREEN CARD.

Kwa faida ya wengi, naomba yeyote anayejua au amefanikiwa kuwa na Green Card ya Marekani ni kwa namna gani imemsaidia kuishi huko USA na kwa namna gani imemsaidia kupata kazi nzuri na kuweza ku-make enough cash na kutimiza ndoto zake.

Pia naomba kufahamu changamoto ambayo mtu aliyeshinda Green Card anaweza kukutana nayo mara tu anaingia Marekani for the first time au nini afanye ili mambo yaende sawa.

Mwisho naomba kujua kama mtu akiacha mshahahara wa 3M Bongo akienda Marekani anaweza ku-make fedha ndefu zaidi na hasa akiwa na hayo makaratasi kwa maana ya Green Card au ndio inaweza kuwa anapotea kimaisha?

Natanguliza shukrani kwa wajuzi wa haya mambo na naamini mchango wenu utasaidia Watanzania wengi kufahamu kuhusu faida za kuwa na Green Card ya Marekani.

ASANTENI SANA 🙏🙏
Hakuna faida yoyote; unaruhusiwa kuishi na kufanya kazi bila kubugudhiwa tu lakini haina maana kuwa hiyo ni faida kwani inategemea na vigezo vingine vingi hadi uweze kuiita kuwa ni faida. Unaweza kuwa na green card, ukaishia kuishi kwenye trailer na kufanya kazi ya bora mkono wende kinywani tu.

Ukipata green card usijisahau ukadhani umepata faida sana
 
Back
Top Bottom