Naomba kujulishwa kwa sababu za kitaalam; Ipi nyumba bora kati ya tofali za kuchoma na cement?

Kuandaa tofali za kuchoma kunahitaji kuchimba udongo ufyatue tofali, ukate miti upate kuni za kuchoma tofali, mazingira machache sana yanaruhusu hiyo kazi ukilinganisha na za cement ambazo unanunua tu na kutafuta mchanga.
ni hela yako tu,
mwaka 2003 wakati mkapa ametoa hela za kujenga shule za msingi, ndani ya mkoa shinyanga nilipata tenda ya kujenga shule fulani, tulifuata tofali za kuchoma wilaya kibondo mkoa wa kigoma, na tofali moja lilisimamia sh 70 wakati ule huku la simenti likiwa kama 400 hivi!!
 
Point yako ya msingi ni ipi hasa, me nasema tofari za kuchoma ni Imara, tht why nikakutolea na mfano wake wa kuwa Imara
hana point huyo jamaa,
kwanza inawezekana anpoishi tofari za kuchoma ni adimu
pili hana uzoefu katika mambo ya ujenzi
tatu hajui kama hata tofari za kuchoma kuna maeneo maalumu ya kuzifyatua, anadhani wanafyatua popote tu!
 
Tofari za kuchoma ni bora kwa sababu zenyewe kadri muda unavyo ungezeka zinazidi kuwa ngumu. Zile za cement hufika muda zinakosa nguvu coz cement inaexpire

Ila pia udongo unatofautiana. Kuna udongo wenye chumvu haufai kabsa kutengnezea tofal
 
ni hela yako tu,
mwaka 2003 wakati mkapa ametoa hela za kujenga shule za msingi, ndani ya mkoa shinyanga nilipata yenda ya kujenga shule fulani, tulifuata tofali za kuchoma wilaya kibondo mkoa wa kigoma, na tofali moja lilisimamia sh 70 wakati ule huku la simenti likiwa kama 400 hivi!!
Hayatofautiani ukubwa?
 
Matofali ya kuchoma ni imara sana kwani hayaozi ili ya cement muda unafika yanaoza na kuanza kumomonyoka
 
sasa mbona za cement zina bei sana tofauti naza kuchoma. na watu wengi siku hizi wanakimbilia kwenye matofari ya cement ni kwann?
kwanini kiatu cha spesho kina bei kubwa kliko mtumba Lakini hakidumu ? ukifahim hiki fmbo, the same applied to above argument

Sent from my itel it1507 using JamiiForums mobile app
 
N swali ambalo linahtaji kujibiwa kimapana zaidi, lkn mm na hivi vichache tu.
Haijalishi tofali n la material gan, uimara wake unategemea matengenezo yake tngu maandalizi ya material mpaka product.(fabrication process)..
Tofali la cement (block), choma (brick), mawe na material mengine yanatumika ktk ujenzi kwa sababu zifuatazo.
1• upatikanaji wa hayo material, mf. Moshi mchanga na cement kwa ajili ya matofauli ya block n gari zaidi kuliko ukiandaa tofali la choma.
2• utendaji kazi, ufanisi wa kazi kulingana na eneo.
Mf. Moshi ktk material yanayo tumia cement, vitu kama admixture vinahitajika kuongezwa ktk cement ili viweze kutoa product nzr zaid, hivyo garama kukua pia size ya tofali la choma jepesi lkn n ngumu unjenzi wa ukuta kwa Sababu linchukua nafasi ndogo zaidi. utendaji kazi kua mgumu na ufanisi wa kazi unahitaji umakini zaidi.
mfano 2, kwa dar
Ni gumu kutumia tofali la choma kwa Sabab
1• material hayapatikani kirahisi ukilinganisha na cement.
2. Nishat ya joto kwa ajili ya kuchomea matofali ni gari sana ukilinganisha na Joshi.
3• watalam na wazoefu wa kazi sio wengi sana.
Mfano wa tatu.
Mwanza.
Mawe ndio material yanayo tumika kujenga misingi, retaining structure na hata kuta za nyumba kwa sehemu kubwa sana. Mfano mitalo krb yte mwanza imejegwa kwa mawe, kwa sababu ya upatikanaji wa mterial ya mawe ni rahisi zaid ukilinganisha moshi na dar japokua utendaj kazi wake n mgumu sana.
3• kudumu kwa material na ukarabati wake.
Hitimisho, kama yote yataandaliwa ktk standard stahiki (accordingly to engineering code of practise) kulingana na eneo yanayo tumika.

[HASHTAG]#Mawe[/HASHTAG] ni imara zaidi kuliko choma na block
Choma ni imara kuliko tofali la cement.
 
Niliwahi shuhudia lori likimwaga matofali ya kuchoma kama linavyo mwaga mawe au mchanga!na hayakupasuka/kuvunjika....tafakari unaweza fanya hivyo ya sementi?lipi bora kati ya hayo?
La kuchoma halina expire....udongo hauna expire date tofauti na sementi ambayo with time inaexpire
 
Kumbe we ndo uliyokua unapita unakagua kagua nyumba za watu sio?
Siku nyingine anzia kwa mjumbe maana tutakuja kukuona we kibaka unasoma sheet
 
tatizo la tofali la kuchoma ikiaribika kwenye ukuta lazima uondoe ukuta wote japo ni nzuri kwenye moto kuliko tofali za cement, pia ubora wa tofali izi mbili inategemea na hali ya hewa sehemu husika, aina ya udongo au mchanga uliotumia, uchomaji au mixing ratio, tofali ya cement ikiwekwa ratio nzuri inayoitajika ni bora sana, pia kuta za nyumba zinategeea zaidi msingi ilo tusisahau ukiweka msingi mbovu hata kama uweke tofali za mawe zitashuka tu
 
Hili la kuungua tusidanganyane mkuu. Moto uliotumika kuivishia tofari ama kigae unaweza kukuta unatofautiana kwa kiwango cha joto la moto wa ajali husika.
Nimewahi kushuhudia nyumba ya vigae na tofari choma ilivyoungua na kuteketea kabisa na vigae vikawa kama uonavyo "wind screen" ya gari inavyokuwa itokeapo ajali.
Nilistaajabu kwa kuwa nami mwanzo nilidhania vitu vya udongo vilivyokamilishwa utengenezwaji wake kwa kuchomwa moto huwa haviungui.
Tukija kwenye gharama za ujenzi, tofari za saruji ni bora katika ujenzi kuliko tofari za kuchoma. Tofari choma zinakula saruji sana wakati wa kujenga kuliko tofari za saruji.
Ubora wa tofari la saruji hutokana na resho utakayoitumia wakati wa uchanganyaji wa mchanga wa kufyatulia matofari.
Pia ubora wa tofari choma ni aina ya udongo ulioandalia matofari yako, pia uivishaji katika kuyachoma.
Kutumia tofari la saruji katika ujenzi kwa nyumba za kisasa ni kilakitu. Fanya utafiti utaelewa ukweli.
Si kweli mkuu,, tofali ya kuchoma ina ubora zaid ya kuliko ya cement zipo sababu za kisayansi zikiwepo chemical reaction na validity of matrials found in cement powder. Na ukiweka tofali la kuchoma na la cement uyahifadhi mahali kwa miaka kumi ukija kufanya quality analysis la cement litakuwa limesha poteza ubora kwa 20% dhid ya tofali la kuchoma na ndio maana hata wenzetu weupe ambao ndio ma pro founders wa hizi technologies wana prefer zaid tofali za kuchoma katika ujenzi wa makazi yao.

Tatizo ni moja tu lililo jengeka miongoni mwa ngozi nyeusi kuwa usasa ni kujenga na tofali za cement wakati ubora wa cement unapungua kadri siku zinavyo songa wakati la kuchoma ubora unaongezeka kadri linavyo zid kuish na likichomwa vyema kabisa linakuwa kama jiwe.wakati cement hata ukiweka ratio kubwa kadri siku zinavyo songa ubora unapungua.

Tatizo lingine upatikana wa tofali ya kuchoma kwa baadhi ya mikoa ni mgumu kutokana na nature ya udongo wa mikoa husika hunyo kulazimika kutumia tofali za cement maana udongo mzuri wa tofali za kuchoma unapatikana sana mikoa ya mbeya,arusha ,kagera,njombe na iringa, tanga hasa lushoto,songea,baadhi ya maeneo,rukwa,kilimanjaro, kwa sehemu kubwa mikoa tajwa hapo ndio unaweza pata tofali imara kabisa la kuchoma maana udongo wa maeneo hayo unafaa sana kwa tofali hizo ,na hata nyyuma nyingi za mikoa hiyo zina tofali za aina hiyo zaid.
 
tatizo la tofali la kuchoma ikiaribika kwenye ukuta lazima uondoe ukuta wote japo ni nzuri kwenye moto kuliko tofali za cement, pia ubora wa tofali izi mbili inategemea na hali ya hewa sehemu husika, aina ya udongo au mchanga uliotumia, uchomaji au mixing ratio, tofali ya cement ikiwekwa ratio nzuri inayoitajika ni bora sana, pia kuta za nyumba zinategeea zaidi msingi ilo tusisahau ukiweka msingi mbovu hata kama uweke tofali za mawe zitashuka tu
umesema tatizo la tofali za kuchoma likiharibika kwenye ukuta lazima ubomoe ukuta wote?

we ni fundi washi?
au unaongea tu! hivi hiyo sentesi hata mtoto anaweza kukubaliana na wewe?
 
Back
Top Bottom