Naomba Kujua Kuhusu Mikopo ya Riba nafuu kutoka Hazina.

clinician

JF-Expert Member
Mar 5, 2014
2,020
4,757
Heshima kwenu!
Nimesikia kuna mikopo inatolewa na serikali kupitia hazina kwa watumishi wa uma. Nimetafuta nyuzi humu JF kuihusu lakini nimeona michango ni kidogo sana haitoi usaidizi mzuri.
Ninaomba kwa yeyote mwenye taarifa sahihi kuhusu mkopo huu,vigezo na masharti vya kupata ,utaratibu wa kupata na utaratibu wa marejesho
 
Mikopo hiyo huwa inatoka mara 2 kwa mwaka. Yaani kwa mara ya kwanza ni kati ya mwezi wa 3 na wa 4 na kwa mara ya pili ni kati ya mwezi wa 11 na 12.

Mara ya kwanza mikopo hiyo ilikuwa ikitolewa kwa wafanyakazi wa Serikali kuu tu lakini kuanzia mwaka huu mkopo huo umetolewa pia kwa Halmashauri za Wilaya.

Kwa sababu uko katika Halmashauri ya Wilaya maelekezo ni kama ifuatavyo:-

1. Mkopo huwa ni kidogo kulinganisha na hitaji la watumishi wa Halmashauri. Mfano zinaweza toka milioni 200 kwa kila Halmashauri wakati kila mtumishi wa Halmashauri anataka mkopo huo hivyo huwa kuna kupata au kukosa.

2. Mkopo huo hauna riba kabisa ingawa kuna asilimia fulani ndogo sana ambayo kimsingi siyo riba bali ni bima ya mkopo huo.

3. Sharti kuu la mkopo huo ni kwamba unapaswa usiwe na mkopo mwingine ili ubaki na 1 ya 3 ya mshahara wako.

4. Kuna fomu za kujaza ambazo Mkurugenzi wa Halmashauri na timu yake aliyoichagua inapitia maombi yote na kuamua nani apate na nani akose. Katika fomu hizo utabandika picha zako pamoja na salary slip yako.

5. Marejesho yake ni kukatwa katika mshahara wako kila mwezi.
 
Kwa hiyo niende mwezi wa ngapi pale Halmashauri kufuatilia mkopo huu?
 
Shida ya huo mkopo huwa wanagawana kwanza hapo Halmashauri HQ na mabaki ndio wanapata wachache watakaobahatika. Kuna jamaa namfahamu aliomba milioni 12 lakini akaingiziwa milioni 5 tu, unaweza kutofanikisha malengo yako.
 
Heshima kwenu!
Nimesikia kuna mikopo inatolewa na serikali kupitia hazina kwa watumishi wa uma. Nimetafuta nyuzi humu JF kuihusu lakini nimeona michango ni kidogo sana haitoi usaidizi mzuri.
Ninaomba kwa yeyote mwenye taarifa sahihi kuhusu mkopo huu,vigezo na masharti vya kupata ,utaratibu wa kupata na utaratibu wa marejesho
Umegugo haigugiki?
 
Wewe ni MWALIMU wa shule ya msingi au sekondari?
Mkuu una ugomvi gani na walimu? Mimi sio mwalimu wa sekondari wala msingi.
Mikopo hiyo huwa inatoka mara 2 kwa mwaka. Yaani kwa mara ya kwanza ni kati ya mwezi wa 3 na wa 4 na kwa mara ya pili ni kati ya mwezi wa 11 na 12.

Mara ya kwanza mikopo hiyo ilikuwa ikitolewa kwa wafanyakazi wa Serikali kuu tu lakini kuanzia mwaka huu mkopo huo umetolewa pia kwa Halmashauri za Wilaya.

Kwa sababu uko katika Halmashauri ya Wilaya maelekezo ni kama ifuatavyo:-

1. Mkopo huwa ni kidogo kulinganisha na hitaji la watumishi wa Halmashauri. Mfano zinaweza toka milioni 200 kwa kila Halmashauri wakati kila mtumishi wa Halmashauri anataka mkopo huo hivyo huwa kuna kupata au kukosa.

2. Mkopo huo hauna riba kabisa ingawa kuna asilimia fulani ndogo sana ambayo kimsingi siyo riba bali ni bima ya mkopo huo.

3. Sharti kuu la mkopo huo ni kwamba unapaswa usiwe na mkopo mwingine ili ubaki na 1 ya 3 ya mshahara wako.

4. Kuna fomu za kujaza ambazo Mkurugenzi wa Halmashauri na timu yake aliyoichagua inapitia maombi yote na kuamua nani apate na nani akose. Katika fomu hizo utabandika picha zako pamoja na salary slip yako.

5. Marejesho yake ni kukatwa katika mshahara wako kila mwezi.
Mkuu Asante sana kwa maelezo mazuri,kwahiyo halmashauri ndio wanaamua upate kiasi gani? au muombaji unaomba unachohitaji? Loan ceiling(ukomo wa mkopo) upoje? yaani kima cha juu na cha chini cha kukopa. Mengineyo nadhani naweza kuuliza Halmashauri. Ubarikiwe sana.
 
Nenda hazina iliyopo mkoani Kwa kwako Kwa maelezo zaidi, mwanzo ilikua kujiunga laki 2 then unakatwa kidogo kulingana na salary slip Yako baada ya muda unaruhusiwa kukopa riba ni 2% nadhani
Hiki unachozungumza wewe ni HAZINA SACCOS.

Ila HAZINA wao Kama wao Wana mikopo huwa wanatoa kila Halmashauri huwa Kuna mgawo unatoka. Ninavyosikia huwa haina riba. Na nasikia huwa Kuna sharti ili ukope inatakiwa usiwe na mkopo mwingine.

Ila tatizo kwa Halmashauri Kuna watu Wana njaa na tamaa kinoma, kwahiyo Kama Halmashauri imepewa milioni 300 ni ngumu kwa mtumishi wa chini kupata. Wanakopeshana wakuu wa idara pesa yote.
 
Sasa mkuu watajikopesha kila mwaka hizo pesa?
 
Back
Top Bottom