Naomba kujua faida za kusoma nje ya Nchi (Bachelor of Science In Agricultural Engineering).
Habari ndugu zangu,
Mimi ni kijana, nimezaliwa na kukulia katika kijiji kimoja kilichopo Mkoani Shinyanga. Nilihitimu stashahada ya uhandisi Kilimo miaka kadhaa iliyopita kutoka chuo cha Wizara ya Kilimo hapa nchini. Nilifanikiwa kuwa mwanafunzi bora wa mwaka.
Baada ya kuhitimu, nimeweza kufanya kazi za mikataba katika taasisi binafsi mbili na taasisi ya Umma moja. Katika kuendelea kutafuta fursa mbalimbali niliweza kufanya maombi ya ufadhili wa masomo ya Elimu ya juu nje ya Nchi Kwa ngazi ya Shahada. Mungu amenisaidia nimepata ufadhili kwenda kusoma Shahada ya Kwanza ya uhandisi wa Kilimo katika Bara la Ulaya.
Naandika Uzi huu kuomba kujua faida za kusoma nje ya Nchi Kwa kozi ya Bachelor of Science in Agricultural Engineering, Fursa katika kujiajiri, pia naomba kujua ni organizations zipi za kimataifa naweza kufanya kazi kama nikihitimu Shahada hii.
Natanguliza shukrani.