Naomba kujua Blue Band (tunayopaka kwenye Mkate) kwa Kiswahili inaitwaje?

Tangu nikue, hadi nimemaliza chuo, ni neno moja tu ninaloliona na kuliskia, iwe ni dukani, kwenye TV n.k.: Blue Band. Je, kwa kiswahili inaitwaje? maana nime-google sipati jibu, japo nahisi neno 'Blue Band' ni brand ya kampuni flani, lakini naomba kujua jina halisi la hiyo bidhaa.

Asanteni.
Kizungu Margarine, kiswahili jibini au siagi
 
Tangu nikue, hadi nimemaliza chuo, ni neno moja tu ninaloliona na kuliskia, iwe ni dukani, kwenye TV n.k.: Blue Band. Je, kwa kiswahili inaitwaje? maana nime-google sipati jibu, japo nahisi neno 'Blue Band' ni brand ya kampuni flani, lakini naomba kujua jina halisi la hiyo bidhaa.

Asanteni.
Inaitwa siagi mkuu. Ila naomba nikupe ushauri wa bure mkuu.Acha kubugia matakataka hayo,utaishia kuwa overweight na hatimaye kuishia kupata maradhi kama hypertension,kisukari magonjwa ya moyo nk.Jamani doesn't common sense tell you that kubugia mafuta ni hatari kwa afya yako.Funny isn't it.Mkuu makampuni mengi yana agenda za siri,inabidi sisi wenyewe tuwe makini.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Inaitwa '' MADE IN KENYA" maana wafanyabishara wakubwa Bongo wanatengeneza ma juice tuu hakuna anayebuni kutengeneza vitu kama hivyo na mwisho wake tunakuwa soko la Kenya ndio maana hata kiswahili chake hakijulikani
Miaka ya 70 hadi 80 tulikuwa tunatengeneza TAN BOND margarine japo quality yake ilikuwa mmh,sasa inawezekana pengine kiwanda kilfungwa ila sina uhakika.
 
Ni nini tofauti ya Siagi na Jibini?
Jibini ni Cheese,inatengenezwa na cream ya maziwa
Siagi ni kama blue band,tanbond etc hii nadhani inatokana na vegetable oils
Kuna ingine yaitwa margarine ingine butter.,tofauti zake kwa undani hapo sasa wapishi na wa mambo ya lishe watuambie
 
Inaitwa siagi mkuu. Ila naomba nikupe ushauri wa bure mkuu.Acha kubugia matakataka hayo,utaishia kuwa overweight na hatimaye kuishia kupata maradhi kama hypertension,kisukari magonjwa ya moyo nk.Jamani doesn't common sense tell you that kubugia mafuta ni hatari kwa afya yako.Funny isn't it.Mkuu makampuni mengi yana agenda za siri,inabidi sisi wenyewe tuwe makini.
Sio takataka mkuu,cha msingi angalia kiasi unachokula kiwe kidogo
Fats and oils ni sehemu muhimu sana ya lishe katika rika lolote
 
Miaka ya 70 hadi 80 tulikuwa tunatengeneza TAN BOND margarine japo quality yake ilikuwa mmh,sasa inawezekana pengine kiwanda kilfungwa ila sina uhakika.
Ina harufu flani hivii I find choking,labda utumie for baking only
 
Tangu nikue, hadi nimemaliza chuo, ni neno moja tu ninaloliona na kuliskia, iwe ni dukani, kwenye TV n.k.: Blue Band. Je, kwa kiswahili inaitwaje? maana nime-google sipati jibu, japo nahisi neno 'Blue Band' ni brand ya kampuni flani, lakini naomba kujua jina halisi la hiyo bidhaa.

Asanteni.
Blue band ni jina la aina ya siagi itengenezwayo nchini Kenya.
Ikumbukwe hapa Tanzania kwenye miaka ya.. 80 hivi palitengenezwa siagi kama hii ikijulikana kwa jina la "Tan band"
Blue Band kwa tafsiri ya kiswahili kama alivyoitumia mtengenezaji ni "ufito wa buluu" (ona taswira ya ufito huo wa buluu katika kila bidhaa na matangazo ya Blue Band)
 
Back
Top Bottom