Nani mkali: Msaga Sumu vs Manfongo

wewe KINANDA a.k.a gita mwananyamala enzi hizo miaka 93 94 kama sikosei basi 95
na kina MUDDY KADOGO na kundi zima la HISANI MUSICAL CLUB lilikuwa maskani yake pale MWANANYAMA Kwa manjunju na album yao ya GARI KUBWA TISHIO ikiambatana na nyimbo kali zenye vionjo vikari kama
nalialia ooh mamaoo uko wapi mama ooh
shemeji kaulamba mkopo wa sukari
nataka kubebwa ooh nataka kunyonya eeh
na vingne vingi
kabla baadae kuja 7suvival then ikaja JAGWA MUSIC watoto wa jolijo wanaosumbua sasa hivi ingawaje jagwa ya kitamba miaka ya 2000 ndo ilikuwa chikopa zaidi
hatari sanaa
Kuna ile singo ya hereni pia ya mjini je wazikumbuka hzo, unajua watu wasichanganye mnanda, mchiriku, kigodoro, then kisingeli ingawa ni revolution ya ingine. Na pia naiona clouds fm kabisa wakitaka kuiua hicho kisingeli.
 
Msaga sumu andio ID ya mchiriku/ singeli na hio mnanda, Man Fongo wa kupita!
Msaga Sumu ndo habari ya mjini, mfalme wao!
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Habari wanajamvi?
Kwanza naomba niseme mie nimezaliwa na kukulia uswazi mpka nilipoanza maisha ndio nikahamia walau nusu uswazi...

Uswahilini kwetu kwa wale wa maeneo ya tandika,maguruwe,yombo,temeke kwa maganga na sehemu nyinginezo mnakumbuka mziki wa MNANDA ambao ni kinanda kidogo lakini kinapigwa kwa umahiri mpaka mziki ukaitwa "MNANDA".
Kwakua mziki huu ulihusisha vibaka wengi polisi walidhibiti na taratibu mziki huu ukapotea... Achama na mnanda wa marehemu Omary Omary ulikua wa kisasa ingawa nae alikua muanzilishi enzi hizo maemeo ya temeke TP.

Sasa miaka ya 2010 kama sijakosea,akaibuka Msaga Sumu yeye alitumia vionjo kwa nyimbo za watu na hatimae uswahilini wakaita "VIGODORO" kwakua likianza ni mpaka asubuhi.

Lakini kwa sasa kuna kitu "zamu ya nani leo zamu ya man fongo sijui ninininiiiii........" huyu amekuja na style inaitwa KISINGELI ni balaa...
Nliangalia tamasha la chips mayai msaga sumu alipopanda stage wanambagala walipagawa lakibi manfongo nae alipopanda akaleta balaa zaidi..

Nkajiuliza hivi nani zaidi?
Majibu sina


!
!
msaga sumu stand up....
 
NYIMBO YAKE KALI KULIKO NI ILE YA TUNAMPENDA LOWASA
Sema ya NAIPENDA SIMBA SHABIKI WA DAMU, hiyo ya lowassa alipachika tu jina la lowassa kupiga hela za nnyumbbu maana aliwasoma walivyo wepesi ikitaja jina la lowassa wako tayari kulipa!
 
Sema ya NAIPENDA SIMBA SHABIKI WA DAMU, hiyo ya lowassa alipachika tu jina la lowassa kupiga hela za nnyumbbu maana aliwasoma walivyo wepesi ikitaja jina la lowassa wako tayari kulipa!
LOWASA KIBOKO YENU LUMUMBA kuhusu aliyeimba naipenda SIMBA MSHABIKI WA DAMU NI MC SOUDY yule aliyeimba rafik wa kwel babu wa loliondo ila MSAGA aliimba naipenda Vyura mtoto wa jangwani
 
LOWASA KIBOKO YENU LUMUMBA kuhusu aliyeimba naipenda SIMBA MSHABIKI WA DAMU NI MC SOUDY yule aliyeimba rafik wa kwel babu wa loliondo ila MSAGA aliimba naipenda Vyura mtoto wa jangwani
Kaweke rekodi zakp sahihi!
 
Back
Top Bottom