Nani kubeba tuzo ya Msanii bora wa Kiume kwa Bongo kati ya mafahari hawa?

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
2,201
5,585
1724943882448.png

Kamati ya Tanzania Music Award (TMA) leo August 29,2024 imeanza kutangaza Nominees wanaowania tuzo za muziki Nchini kwa kuanza na category tatu ambazo ni Mwanamuziki bora wa kiume wa mwaka, wimbo bora wa taarabu wa mwaka na wimbo bora Afrika Mashariki, Kusini na Magharibi.

Wimbo bora wa taarabu wa mwaka kuna Watu na Viatu ya Malkia Layla Rashid, Hatuachani ya Amina Kidevu, Bila Yeye Sijiwezi ya Mwinyi Mkuu, Sina Wema ya Mwasiti Mbwana na DSM Sweetheart ya Salha.

Wimbo bora Afrika Mashariki, Kusini na Magharibi kuna People ya Libianca, American Love ya Qing Madi, Lonely at the Top ya Asake, Unavailable ya Davido ft Musa Keys na Mnike ya Tyler ICU.

Kwa upande wa Mwanamuziki bora wa mwaka wa kiume kuna Marioo kupitia wimbo wa Shisha , Diamond Platnumz kupitia Shuu, Harmonize kupitia Single Again , Alikiba kupitia Sumu na Jay Melody kupitia wimbo wa Nitasema

Kamati ya Tuzo inayoongozwa na Mwenyekiti wake David Minja na Makamu Mwenyekiti Seven Mosha wamesema category nyingine zitaendelea kutangazwa kila baada ya muda huku zoezi la kupigia kura likifumgulowa rasmi September 3.
 
Mario ana nafasi kubwa ya kuchukua, ametoa hit song tupu toka ameingia kwenye game…
 
Back
Top Bottom