Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,199
NANI ATAKUWA RAIS MUOKOZI WA TANZANIA???
Wakati ndugu zetu wa ZNZ tayari washajua nani atakuwa Rais wao baada ya uchaguzi wa 2010, sisi kutoka Bara bado tunatia mikono yetu gizani kumdhania huyu au yule atafaa kama Kikwete kweli atapumzika mwakani kutokana na matatizo yake ya akili.
Atakaeiokoa nchi hii ni Rais kutoka upinzani na sio kutoka CCM. Kwahivyo, badala ya kupeyana nambari za simu ili tumshawishi mtu fulani wa CCM agombee urais mwakani, ni bora tutumie nguvu zetu kuvishawishi vyama vya upinzani nchini vikubaliane kumuweka mtu mmoja kugombea urais. Wapinzani wakiungana CCM itaanguka na hapo ndipo tutakapopata muokozi wa kweli wa hili Taifa. Kutegemea fulani ni waziri machachari na hodari wa kazi yake kutoka CCM na atakuja kuliokoa Taifa ni sawa na kutokutumia akili zetu vizuri, kwani katika chaguzi zetu za Rais hapa Tanzania tunakichagua chama na sio mtu. Kwahivyo, CCM ikishinda urais na Rais mpya akawa anafanyakazi zake kinyume na system ya kubebana ya CCM ilivyo, definitely watamuweka upande na badala yake fisadi atawekwa kuwa Rais na mambo yataenda kama yalivyo hivi sasa!
Maandishi niliyoweka red, sijapenda kabisa kauli hiyo. Ni kweli inawezekana kwamba tunamchukia Rais wetu lakini tumpe heshima yake jamani. Hivi wewe babako akiambiwa akili yake ina matatizo unajisikiaje? au ungekuwa wewe ndo kiongozi wa nchi ukaambiwa hivyo unajisikiaje? Tuache dharau zinazopita mipaka bwana. Huyu ni kiongozi wa nchi, kwanini tumdhalilishe hivyo? Wakati tunamchagua hatukuona kama akili yake ina matatizo? Iwaje leo tuseme hana akili? Uliyeandika haya lazima na wewe akili yako siyo timamu.
La pili, unasema wapinzani waungane! Ni nani aliyekwambia wapinzani wa tanzania wapo kwa maslahi ya taifa? Ingekuwa hivyo siwangeshaungana siku nyingi? Hawana lolote hawa, na kuamini kwamba wapinzani wataleta ukombozi tanzania ni kujilisha upepo. Upinzani wa kweli utatoka CCM, angalieni mfano wa Kenya, wapinzani wa kweli walitoka KANU na hao ndiyo waliokuja na wazo la muungano, siyo hawa wanaoangalia tu masilahi yao. Mara ngapi wamejaribu kuungana wakashindwa? Ndo maana mwenzao Makamba anawaita mapaka, wanavutana mikia badala ya kumkabili panya. Wala hakuna tumaini lolote kwa hawa wapinzania wa bongo. porojo tu!