Nani anaweza kuthibitisha kuwa binadamu ni udongo?

Ni wewe ndo unapaswa kusepa,unataka kutulea uliyo kalilishwa shuleni?uhalisai unaonekana
Shule unafundishwa jinsi ya kuwa critical thinker kuelewa mazingira yanayokuzunguka, na ufanyeje kukabiliana na changamoto zake. Sasa ukiniambia shuleni umekaririshwa je kwenye dini tusemeje??
 
Shule unafundishwa jinsi ya kuwa critical thinker kuelewa mazingira yanayokuzunguka, na ufanyeje kukabiliana na changamoto zake. Sasa ukiniambia shuleni umekaririshwa je kwenye dini tusemeje??
Usiku mwema aisee
 
Kuna watu wana matatizo yani badala ya kujibu maswali kadri ajuavyo yeye,matokeo yake anaanza kupinga majibu ya wenzake na kuanzisha ubishi ubishi usio na lazima.

Kuna watu wana matatizo yao ya kiimani ila wanayaamishia kwenye sayansi na ndiyo maana unakuta mabishano hata yasiyo na ulazima. Na karibia wote wametoka imani moja na ndiyo maana nasema wana matatizo ya kiimani na wamekurupukia sayansi na kuigeuza kama ndiyo imani yao mpya baada ya baada kutoka huko watokako,na ndiyo wanatuletea shida kwa kila watakapoona jambo la imani lazima walete ubishani.

Hivi ni nani katika dunia hii anapingana na sayansi hadi kuwe na mabishano? na ndiyo maana naita mabishano yasiyo na ulazima yenye kuletwa na watu wenye matatizo ya kiimani.
 
Mwili wa binadamu ni chakula+maji+hewa. Chakula ni mazao + nyama. Jiulize mazao yanaota wapi na wanyama wanakula nini?
 
Naamini umeshapata majibu mazuri tu ya swalinla kwanza.
Kwa ufupi tu. Kila unachokula kinatoka kwenye udongo, Hivyo ni udongo. Yaani hata ukila nyama myama alikula majani au alimla myama ailiyekula majani ambayo yanamea from udongo.
Na unjua bila chakula hata hizo sperm/ova(gamet) zako zisinge tengenezwa so hizo nazo ni udongo.
Hivyo ukitrace back from vizazi na vizazi vyote vimeanzia udongo= mwisho hamna ubishi sisi ni udongo.
Kuhusu nafsi na moyo.
 
Kama wanasayansi wangekuwa na mawazo kama yako hakika tungekuwa tunaishi bado kwenye dark ages

Tunataka prove hatutaki maneno bila ya uthibitisho

Mfano vitabu vya dini viteketezwe vyote halafu miaka 1000 mbele tuambiwe zirudishwe hakika hazitorudishwa lakini sayansi unaweza kuharibu hata ipite miaka 1000 kupitia experiment, nk zitarudishwa tu

Je maneno ya vitabu zina scientific proof
Unataka proof? Tunaongelea dini na dini inahusisha imani ya mwanadamu kwa mamlaka yenye nguvu na Mara nyingi isiyoonekana..done,mimi sikuwepo wakati Yesu anasulubiwa msalabani wala sikuwepo wakati wa uumbaji,ila naamini,.Mimi naamini binadamu na vyote vilivyomo vimeumbwa.Kila siku naposoma mwili wa binadamu ndivyo navyozidi kuamini kuwa viumbe vyote vimeumbwa na sihitaji proof yoyote.Mark Zuckerberg,mmiliki wa Facebook alikuwa Ni atheist(haamini uwepo wa Mungu) ila juzijuzi tu kaamua kuamini..hulazimishwi,kumwamini Mungu Ni maamuzi yako.Na kuwa mwanasayansi haimaanishi humwamini Mungu.
Ukitaka scientific proof, Muamini Darwin.

"Mwenyezi Mungu huumba anavyopenda. Anapohukumu jambo, huliambia 'kuwa' (basi) likawa".3:47
Aina nyingine za uumbaji ni ile ya usanii wa ufinyazi na kupitia wazazi wawili:
"Amemuumba mtu kwa udongo wa ufinyanzi(utoao sauti) kama vyombo vya udongo(55:4)
Na katika ishara zake (za kuonyesha uwezo wake) ni huku kukuumbeni kwa udongo, kisha mumekuwa watu mnaoenea (30:20).
"...... amekuumbeni katika nafsi moja. Na akamuumba mkewe katika nafsi ile ile. Na akaeneza wanaume wengi na wanawake kutoka katika wawili hao(4:1).
 
Kwa swali la nafsi na moyo. Ningeweza kukueleza vizuri kama unaamini uwepo wa roho pia.
Anyway. Nafsi (self) na moyo(heart) kila kimoja kina nafasi yake na kila kimoja kina uwezo wa kuathiri kingine.
Labda kwanza tuongelee moyo ni nini maana kwenye moyo wengi tunachanganya maana kila mmoja anasema kwa kumaanisha entities tofauti.
Kwanza kwa maelezo yangu ya hapo juu kabisa moyo nilimaanisha ni kiungo chenye kusukuma damu mwilini. Kwa sababu niliassume ulimaanisha moyo huo.
Wakati mwingine watu husema moyo wakimaanisha ni sehemu ya akili inayohusika na hisia za mwanadamu . hisia za kimihemko yaani mfano kupenda / kuchukia/ huzuni/huruma nk.
Hadi hapa kwa namna zote mbili za maana za moyo, bado nafsi na moyo ni entities mbili tofauti.
Tukianza na moyo kama kiungo. Moyo na nafsi zinamuingilianao katika utendaji. Yaani kimoja kinaweza kuathiri kingine . na kimoja kina uwezo wa kuendesha kingine. Mfano kwa nafsi yako unaweza ukaamua kujiwazisha ( imagine) hatari na mapigo ya moyo yakaenda mbio. Zaidi ya hayo nafsi yako inaweza kufanya hata ikaletea shida za kweli za moyo ambazo zinaweza zikawa ugonjwa hatari kabisa.
Pia Moyo unaweza ukasababisha nasfi inyong'onyee endapo, say, una tazizo la moyo la kiafya. Linaweza likafanya ukatetamaa au kuathir namna yako yote ya maisha, fikra nk.
Ila Hata hivyo Nafsi siku zote ndio ilipaswa iongoze moyo.
Na ndio ambayo ipo superior kwa Moyo.
Hata ukiuchukulia Moyo kama sehemu ua akili inayo husika na hisia za kimihemko bado Hisia hizi"Moyo" utabaki kuachini ya nafsi. Japo ukiacha ukuongoze"ukucontrol" utakucontrol kweli. Na binadamu wengi tunashindwa hapa kwasababu hatu maintain ile order ambayo ndio inapaswa iwe. Nafsi kwanza .then Moyo. Tungejizoesha au kujilea hivyo tungekua very rational beings. Tofauti na sasa sehemu kubwa ya binadamu tunaongozwa sana na mihemko kuanzia kufanya maamuzi madogo ya shuguli zetu za kila siku hadi maamuzi makubwa ya kimaisha.
 
Hapa mkuu kitabu kitakatifu ndo mambo yote hakuna haja ya kujadili sana, Mwanasayansi atasema yake lakini kumbuka majadiliano yote hayo bado anatumia kitabu kitakatifu kutoa suluhisho Tuliumbwa kwa udongo na tutarudi kuwa udongo
 
Hiyo issue ya kusema watu walitokana na udongo, hata baadhi ya machapisho ya sayansi yanakubali.

Ni kwa sababu elements zote [H, O, N, S, C, +MADINI] Yaliyopo kwenye miili ya watu inapatikana pia kwenye udongo.
Hata vyakula tunavyokula navyo ni udongo, ndio maana kuna mtu anazaliwa na 3.5Kg lakini anazikwa na 100Kg.
Photosynthesis ndio mchakato unaowasaidia watu kujiongezea kiwango cha 'udongo' kwenye miili yao kwa kula vyakula vilivyotokana na udongo.

Hilo swali la pili bado ni debate iliyopo mezani.

Nikisema udongo umetokana na kuoza kwa mwili wa binadamu ambao una madini mbalimbali na kufanya udongo uwe na madini hayo kutoka mwilini mwa binadamu nitakuwa nakosea????
 
Kua na some elements ambazo zinapatikana kwenye ardhi doesn't make us udongo.
Udongo ni nini? Kuna udongo wenye composition tofauti, binadamu anatokana hasa na upi?
Tukisema binadamu ni udongo kutokana na kua na elements kama Iron, Calcium e.t.c tunakosea, in that case tutaclassify kila kitu kama udongo when in reality sio. Hata hizo elements kabla ya kuingia ardhini zime-originate from something entirely different, from stars formation, nuclear fusion ikasababisha bombardments ya Hydrogen, ikawa Helium, ikapanda hadi kufika kwenye Iron, mengine yakaja kutokana na kucool down na milipuko mingine within the planet. Sasa origin ni udongo au ni nyota? Basi tuseme binadamu ni nyota kama tunaenda na this kind of thinking.

Watu wa dini wanahisi science ipo ili kupingana nao when the reality says otherwise, tupo ili kuprove kama ni kweli au tunapigwa fix tu. Bila scientific discoveries leo hii tungekua tunaishi mistuni, au tungekua kwenye slavery, au hata extinct kutokana na event flani abayo tungeshindwa kuizuia. Science is a necessity, I can't say the same for religion, imeua watu kibao utadhani Malaria.
 
Madini yote yaliopo kwwnye udongo tunayo mwilini,na yakipunguwa kiwango kinachotakiwa na mwili, ndani ya miili yetu,tayari tunakuwa na matatizo ya magonjwa mbali mbali.
Na hata vyakula vyote tunavyokula na kunywa,vinatoka kwenye udongo,kwa hiyo tunsjenga miili yetu,kupitia udongo.
 
Wa kulithibitisha hili ni Muumbaji mwenyewe.
Binafsi siwezi kuthibitisha pasipo na shaka(zaidi ya kusimuliwa na kuamini) kama nisivyoweza kuthibitisha kwamba babu yake na babu yangu ndiye aliyemzaa babu.
 
Back
Top Bottom