Nandy haiba yako inaendana vema na mavazi ya heshima. Usivae nusu uchi

Muite

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
2,838
6,319
Tofauti na mwanzoni alivyokuwa anavaa nguo nzuri sana na zinazomsitiri vema, hakika alikuwa anapendeza sana na nina uhakika ndicho kilichomuongezea umaarufu na kupendwa.

Ila kwa sasa naona Nandy naye anavaa vinguo kuonyesha tumbo, mapaja na matiti. Ukiangalia sura ya Nandy haijakaa KIMCHARUKO bali imebeba sura ya STAHA NA MAADILI.

Kama upo humu nakushauri urudie u uniqueness wako uliokuwa nao mwanzo. Zuchu yeye kipindi kile alipopanda stejini nakuonyesha VITAKO live hakuna mtu aliyeshangaa maana yeye ndivyo alivyo.

Kwahiyo Nandy jaribu kujifunza kwa wasanii wakubwa kama Ali kiba ambaye hana mambo mengi ya ajabu kama kutoboa pua kama Harmonize.

Don't behave like Kajala or Zuchu. Stay natural and decent
 
Back
Top Bottom