Ibambasi
JF-Expert Member
- Jul 25, 2007
- 9,284
- 4,688
Msikitikie Mbowe maana Lissu anampita sasa hivi tuKiukweli, namsikitikia Prof. Kitila Mkumbo, Mshauri wa ACT-Wazalendo. Anashiriki siasa, anazipenda lakini siasa hazimpendi. Kuna wakati, alipokuwa CHADEMA, alifanya ziara za kujitangaza Jimboni kwa Mwigulu Nchemba kule Iramba 'akijiandaa' kugombea kupitia CHADEMA. Mambo yakawa siyo. Yakapita.
Juzi tu hapa, aliteuliwa na ACT-Wazalendo kugombea Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki almaarufu kama EALA. Truly, he was the best candidate of them all. Bunge limetoa maelekezo, kupitia Katibu wa Bunge Dr. Thomas Kashililah kuwa ACT-Wazalendo na NCCR hawatapata kiti hata kimoja.
Huo ni ukomo wa mbio za Prof. Kitila katika kuusaka Ubunge wa EALA. Katika mgawanyo uliofanyika kulingana na idadi na asilimia za Wabunge wa vyama vya siasa Bungeni, CCM tumepewa nafasi 6; CHADEMA 2 kama walivyo wagombea wao na CUF 1. Nafasi 9 zimeishia hapo. Prof. Kitila na Wakili Msando wamekwama.
Namsikitikia Prof. Kitila Mkumbo. Afadhali angebaki ndani ya CHADEMA apambane humo. Vivyohivyo kwa Wakili Msando.
Bastola ya nini tena jamani!?
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam