Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 27,573
- 66,383
NAMNA YA KUWEZA KUISHI DAR! ISHI KIBEPARI
Anaandika Robert Heriel
Ni ndoto ya Vijana wengi hapa nchini kuja mjini hasa Dar es salaam. Hilo sio ajabu kwani hata katika mataifa mengine hiyo ni kawaida. Kwa Kenya Vijana wengi hutamani Nairobi, Nigeria ni Lagos na Abuja, Misri ni Cairo, na majiji mengine makubwa. Hiyo ni kawaida Kwa sababu kwenye majiji makubwa ndio kuna fursa nyingi ndogondogo na kubwakubwa tofauti na huko mashambani ambapo papo Limited.
Sasa nisiseme MENGI nisijekuwachosha kwani najua wengi wenu maisha yamewapiga Knockout ya landings😀(natania japo labda ni kweli 😊)
Namna ya kuweza kuishi Dar es salaam, au jiji lolote kubwa Duniani!
1. Kuwa Mjanja!
Yaani hii ndio kanuni namba moja! Be smart, ruhusu akili yako ifanye kazi mara elfu. Yaani muda wote uwe macho, usizubae zubae.
Usilete akili zako za Shamba huko Kinyanambo.
Kama hutokuwa mjanja mjanja basi mji huu utakushinda mapema Sana. Alafu utateseka na kuchapika vilivyo.
Ujanja sio kusoma Sana shuleni, ujanja nu kuweza kuona gap Kwa haraka kabla ya wengine. Ujanja ujanja!
Usije ukadhani kuchapa kwako kazi Kwa bidii au kuamka Asubuhi Asubuhi ndio utapata pesa mjini 😂 mjini ni mipango, mifumo na kujenga mitandao itakayokusaidia kudhibiti njia nyeti za uzalishaji Mali.
Weka ndoo kwenye bomba linalotoa maji.
Kila mara ikague connection yako kuwa IPO active😊. Nimeeleweka.
2. Jibrand. Jenga jina
Sio unafika mjini alafu unaishi Kama kibwengo! Yaani umezubaa zubaa! Mwisho wa siku ulale njaa.
Jibrand. Jenga jina lako. Hakikisha watu wanakufahamu.
Kujibrand mara nyingi hakuhitaji pesa mingi. Ni wewe Tu kujikubali na kuonyesha nini unacho.
i. Jitangaze kanisani au misikitini
Kama muimbaji imba, omba kutoa adhana msikitini au kufundisha madrasa au tafuta Jambo lolote la kukufanya utambulike. Sio unaenda kanisani Kwa kunyata Kama Paka shume linalofizia kifaranga.
Ati mtu anaenda kanisani anajificha nyuma huko hataki watu wamuone😀 huko ni kutokujiamini. Labda uwe unajiweza. Toa masomo kanisani, yaani ndani ya miezi mitatu wawe wamekutambua.
Usiwe umezubaa zubaa Kama Mzee anayesubiri kufa😀.
ii. Kuwa mtanashati au Mrembo
Usiwe Kama kinyago cha Bure, mtaani ukiwa mtanashati watu watakujua tuu. Watakuzingatia hata ukipita, lakini ukiwa lichafu lililozubaa zubaa watu watakupuuza. Hata mademu tuu watakuona Kama mkosi. Au hata Masela watakuona binti wa hovyo. Jipe thamani.
iii. Itambulishe kazi yako kwenye jamii
Kama ni mwalimu mtaani wakujue kuwa wewe ni mwalimu Bora, sio tuu mwalimu Bali mwalimu wa kimataifa, Kama ni Mwanasheria au Fani yoyote jaribu kuisaidia jamii. Kaa karibu na jamii yako.
Usizubae zubae.
Jitenge na jamii Kama unajiweza na siku zote wanaojiweza wanamakazi Yao.
3. Kuwa mnafiki
Jiji lolote ili ulimudu lazima uwe King au Queen of Drama, kuwa muigizaji, mnafiki wa kimataifa. Uwe na msimamo Kwa wenye msimamo, lakini pia uwe Kigeugeu Kwa wenye Kigeugeu. Uwe na akili Kwa walio na akili, lakini uwe mjinga Kwa waliowajinga. Usipende kukosoa mfumo utakaoukuta ukiwa jiji lolote lile. Sio kazi yako kubadilisha mambo, kazi yako ni kujibadilisha wewe mwenyewe uwe mtu Bora.
Mfano no 1
Sio unafika Sinza au Kinondoni unakuta Wadada wanaovaa nguo za uchi uchi alafu unaleta mambo yako ya kishamba huko kantalamba, utakosa vitu vizuri shauri yako. Ukiona pisikali imevaa kichupi wewe mkonyeze😉 kisha msalimie alafu mwambie umependeza Sana Sister, ama kweli kuna watoto mmeumbwa, akijichekesha mpe tena na tena za uso, kisha sepa. Yaani utaishi maisha Raha mustarehe. Ukijifanya mjuaji unaweza kujikuta unakufa bila hata kutoka na Vitoto vizuri Kwa upuuzi wako.
Mfano no 2
Unapita Club au Bar au Casino unakuta wenzako wanaenjoi Kwa namna yao labda Kucheza au kupiga gambe alafu wewe unaleta usnitch wako WA kilokole au kisabato. Ooh! Sijui pombe sio nzuri kiafya mara ooh! Kitimoto imekatazwa kwenye Biblia sijui Quran, kwani Nani hajui hayo wewe boya😂😂. Hakuna asiyejua kitimoto Biblia imekataza na hakuna asiyejua pombe sio nzuri. Na wala hakuna asiyejua kuzini ni dhambi au kuvaa nguo za uchi ni kosa. Utakosa Dili Kwa ujinga wako.
Ukiwa mazingira ya kazi fanya kilichombele yako. Sio ulete wimbo wa mazishi kwenye harusi. Mji utakushinda mapema.
Kama unataka kuhubiri wasubiri kanisani au msikitini mbona watakuja na wao ndio watoa Sadaka wazuri, na wao ndio wanaelewa zaidi ya hao wasiofanya hayo😀😀.
4. Jifunze kukaa na Njaa
Kukaa na njaa jijini ni kitu cha kawaida Sana. Usilete mambo yako ya Shamba au kijijini kwenu kuwa ni lazima ule Milo mitatu au minne. Huku mjini kikawaida Milo inayotambulika ni Milo miwili tu. Na Kwa wale hustlers hupiga mlo mmoja tu. Kuna wakati hata huo mmoja ni Kwa mbinde. Jifunze kukaa na njaa, hata ukiwa na pesa ikiwa bado ishu zako hazijatiki yaani Mishe zako za kupata pesa sio za uhakika, jiwekee tuu Ratiba kuwa unakula Milo miwili. Sio kosa.
Usishindane Kula utakwama, sio jirani kanunua nyama na wewe nyama!
Subiri ukiwa na hela ya uhakika. Kula diet Kwa gharama nafuu
5. Usiwe na marafiki wengi hasa wachovu!
Na hii inatokana na jinsi Brand yako ilivyo. Kama jina lako sio kubwa huwezi kuwa na marafiki wa maana. Halikadhalika na Kama sio mjanja. Ndio maana nilitaja hayo hapo juu.
Usipendelee marafiki Wale wa kutembeleana tembeleana mara Kwa mara nyumbani hiyo ni Dalili ya kukosa kazi za kufanya. Kumaanisha hata wewe hutakiwi kutembea katika maghetto ya washikaji mara Kwa mara huo ni utoto na kutojitambua. Kama mnakutana yapo Maeneo ya kukutana Kwa bei ya kununua soda tuu ya Buku. Huku ni mjini usilete mambo ya kijijini ya kutembeleana nyumbani.
6. Tafuta Pisikali/ mshikaji anayejishughulisha
Usilete mambo ya kizamani na kijamaa ukiwa mjini. Ili jiji liitwe jiji lazima ubepari uwe juu Sana. Usikubali kunyonywa. Yaani ukiwa mjini kuwa Opportunist. Usikubali kuwa demu ambaye anaomba ati nauli ya Buku tano sijui vocha huyo Hana maana, piga chini. Huyo asubiri watu kutoka Shamba huko. Au mwanaume asiyejishughulisha, asiye na makazi yake iwe hata ghetto lenye godoro na kitanda. Huyo kimbia usimtake.
Taikon huwaga nawaambia vijana, mji ukikushinda utake mwenyewe.
Unajipa mizigo mwenyewe Kwa ujinga wako.
Unahonga mwanamke asiyekuhonga😂😂 alafu bado u mtafutaji wa pesa yaani bado unajitafuta, wewe ni Fala. Yaani wanawake wanaojishughulisha walivyojaa hapa mjini wanaotafuta wanaume unakosa hata mmoja 😀😀.
Taikon ni bepari tena bepari haswa! Ukiwa mtafutaji usikubali kunyonywa bali nyonyana.
Unakakuta kakijana kawatu kametoka Huko Usukumani ndio kamepata biashara ya Duka au Bodaboda kanaanza kujiumiza Kwa videmu uchwara visivyo na mbele wala nyuma ati kisa anapewa papuchi😀😀 wewe ni boya.
Tumia kanuni ya "Tupeane"
Ukinipa penzi nitakupa penzi
Ukinipa pesa nitakupa pesa
Kama ni pesa Kwa penzi basi zipo pisikali zinazojiuza Kwa bei Sawa na bure huko mitandaoni na viunga vya jiji. Usikubali kulaliwa.
Na Mwanamke usikubali kuwa na Mwanaume Mpumbavu asiyejielewa.
Usijesema ooh! Sijui dini sijui Mila na desturi zinataka mwanaume afanye blah! Blah! Kwenye majiji makubwa hizo kanuni hazitumiki ndugu yangu, huku hakuna cha dini wala hakuna cha Mila na desturi. Huku ni ubepari mwanzo mwisho.
Ukitaka kushindwa huku mjini leta mambo yako ya Dini na Mila sijui desturi. Utakwama mapema. Huku jicho lako lijikite kwenye napata faida gani hasahasa ya kiuchumi maana hiyo ndio itaamua ubaki mjini au uondoke Kwa aibu.
7. Jenga Connection za uhakika
Jifunze kuendesha Gari, kuwa karibu na wenye magari au madalali wa magari, Usiishi mjini hujui kuendesha Gari nyau wewe.
Mjini kuna hitaji mambo makuu matatu.
1. Connection ya watu
2. Simu nzuri Kwa ajili ya mawasiliano na hizo connection
3. Usafiri
Hakikisha ndani ya miaka mitano mpaka Saba uwapo mjini ununue kigari hata cha milioni tatu au nne. Usizubae zubae na kuleta maneno ya washamba au ya watu wa vijijini kuwa ooh! Gari ndogo hiyo, sijui IST au vitz ya wanawake, wengi wanaoongea hayo maneno bado wanaakili za kijijini.
Gari ni Gari, kuliko usiwe nayo ni Bora uwe hata na haki kadogo.
Wenye magari wanaheshimiana wawapo Iwe kanisani, misikitini, Bar, Club, sherehe n.k.i
Usiwaze hela ya Mafuta utapata wapi, waza kununua Gari Kali zaidi inayokula Mafuta zaidi ya hiyo ndogo uliyonunua. Ukishanunua Gari utashangaa hata mifumo yako ya upataji pesa inabadilika automatically.
Wenye magari watakubaliana na Mimi. Hasa Wale wa majiji makubwa.
8. Usiogope Kuzaa
Nilishakuambia Majiji makubwa hayafuati kanuni za Kidini na Mila na desturi. Ukijifanya unafuata hayo Kwa Sana utajikuta unachelewa au hutafanya lolote.
Vijana wengi mjini wamejikuta wanamiaka 30-40 wakiwa hawana hata mtoto mmoja kisa kuleta mambo ya kijijini.
Normal ukiwa jijini angalau kabla hujapiga 30 uwe na mtoto mmoja wa kibepari.
Majiji yanatabia ya kukutoa mchezoni ikiwa utashindwa mambo madogo madogo Kama hayo.
Ilimradi usimzalishe Mwanafunzi ukaanza kukimbizana na serikali au Mke WA Mtu ukaanza kujikuta katika vita visivyo na maana.
Ukiwa na mtoto kabla ya 30 itakupa utulivu wa kuendelea kuwa mtafutaji kwani akili yako itakuambia angalau bado nina mtoto. Lakini usipokuwa naye inaweza kukuwela under pressure yaani utakosa utulivu.
Mara uwaze kuoa/kuolewa mara mapenzi yakusumbue yaani utakuwa Kama katoto kanako Balehe!
Mwishowe utapoteza utulivu wa utafutaji.
9. Ishi kibepari
Usiwe na huruma
Ifanye pesa ndio mungu wako Wapili Baada ya Mungu Mkuu.
Iheshimu na ipende. Izalishe zaidi, hakikisha unai-accumulate zaidi kuliko unavyoitawanya.
Kuwa mchumi Kwa mambo yasiyo na maana.
Usipende sifa za kijinga Kwa watu ambao hutapata au hawatakupa faida yoyote kiuchumi.
Yaani wewe kila kitu kiangalie katika jicho la kiuchumi.
Usiogope maneno ya wanawake wakikuambia wewe bahili au mchumi. Tafuta wanawake wenye uwezo huwezi sikia maneno au Kauli Kama hizo.
Mtakachojadili ni mambo ya pesa na namna mtakavyozizalisha sio mtakavyozitumia.
Taikon yupo Kwa Walamba Asali. Nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam