Namna ya kupika vijungu

Mrs Kharusy

JF-Expert Member
Sep 23, 2013
1,244
671
Mahitaji-
Samaki jodari/ nguru vipande 6-8
Mayai 12
Chumvi to taste
Pilipili manga kijiko cha chai 1
ndimu 2-3
Pilipili mbuzi 1-2
Pilipili boga 1-2(kata ndogondogo sana)
Kitunguu swaumu kijiko cha chai 1
Tangawizi kijiko cha chai 1
Simbambili kijiko 1-2
Mafuta nusu chupa
Bread crumbs (ukipenda)

Jinsi ya kupika

Mayai

Chemsha mayai 10 yakiiva wacha yapoe then yatoe ganda la juu na uyakate kwa urefu pande mbili, toa kiini cha ndani weka pembeni.

Samaki
Mchemshe samaki wako muweke viungo vyote,isipokua pilipili boga .
Chemsha samaki na viungo vyote hadi aive na kusiwe na maji muache samaki apoe.
Baada ya kupoa mchambue mchanganye na vile viini vya mayai.
Baada ya kuchanganya weka mchanganyiko ndani ya mayai uliokata.
Ukimaliza bandika karai jikoni weka mafuta,piga mayai mawili pembeni chovya kijungu ndani ya mayai na uchome.

Ukipenda weka bread crumb ndo uchome.
Vijungu tayari kwa kuliwa.
1404110490218.jpg
 
shukran, pishi limetulia. hivi naeza kula na juice, baada ya taraweh kabla ya daku. ngoja ntafte malighafi weekend insha'h nkupe feedback
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom