Namna ya kuandaa kachumbari mchanganyiko hatua kwa hatua

Pilipilihoho

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
202
145
Mahitaji muhimu

Nyanya kubwa 2
Vitunguu maji 3
Karoti 3
Pilipili hoho ya kijani 1
Pilipili hoho nyekundu 1
Tango 1
Kotmiri 1/2 fungu (1/2 kicha) au 1/2 bunch
Majani ya iliki (parsley) 1/2 fungu (1/2 kichana au 1/2)
Cerely vijiti 4
Chumvi kiasi
Ndimu kiasi

Jinsi ya kuandaa/ kutayarisha

1. Osha mbogamboga kwa kutumia maji safi ya uvuguvugu (pendelea kuosha saladi kwa kutumia maji ya namna hii ili kuua vijidudu)

2. Katakata vitu vyote isipokuwa ndimu, kisha uweke katika mashine ya kusagia chakula ( yaani food processor)

3. Weka namna mbili kwenye mashine yako kisha saga mchanganyiko wako kwa kusita kila baada ya sekunde 1 mpaka kachumbari yako ichanganyike vizuri.

4. Ikishachanganyika vizuri, weka maji ya ndimu kisha changanya na kijiko, tia ndani ya bakuli tayari kwa kuliwa.

Vilevile waweza kutumia brenda kwa ajili ya kusagia, hakikisha usisage kwa muda mrefu ili isiwe majimaji sana. Hivyo nio namna ya kuandaa kachumbari mchanganyiko.
 
Majani ya iliki ndo yakoje, celery ni nini?
Nimegoogle cerely ni vile vitunguu vichanga (majani yake) ila majani ya iliki sijaelewa naona tu yanafanana na bangi nisijekata kachumbali ya bangi......
 
Majani ya iliki ndo yakoje, celery ni nini?
Nimegoogle cerely ni vile vitunguu vichanga (majani yake) ila majani ya iliki sijaelewa naona tu yanafanana na bangi nisijekata kachumbali ya bangi......

Hahahaha
Eti kachumbali ya bangi
 
Majani ya iliki ndo yakoje, celery ni nini?
Nimegoogle cerely ni vile vitunguu vichanga (majani yake) ila majani ya iliki sijaelewa naona tu yanafanana na bangi nisijekata kachumbali ya bangi......

wife, huyo hawezi kukujibu manna kaikopi kwenye blog ya wenyewe.
 
Wapendwa wana Jf,

Naomba mnisaidie jinsi ya kuandaa kachumbari.

Nimeandaa pilau moja matata sana ila natakiwa kuandaa na kachumbari pembeni. Nime-google lakini kuna lugha inatumika kwenye blogs za wapishi ni ngumu kwa sisi wapishi wachanga kuzielewa.

Natanguliza shukrani.
 
Upo nchi gani?!

Walau wewe umeuliza.

Hatahivyo, wewe nisaidie tu na procedure za kuandaa kachumbari nzuri itakayoendana na pilau la kuku.

*kwa lugha rahisi tafadhali...

Natanguliza shukrani.
 
Nyanya...kitunguu....ndimu...pilipili....hoho...chumvi

Anza kukata kimoja baada ya kingine kwny bakuli moja kisha kamulia ndimu na kuweka chumvi vichanganye vzr kwa kukoroga na kijiko
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…