Getrude Mollel
JF-Expert Member
- Apr 26, 2022
- 259
- 353
Mwaka 2022 sekta ya utalii nchi iliimarika zaidi baada ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kucheza na kuzindua filamu ya Tanzania: Royal Tour.
Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa katika historia ya Taifa letu, ambapo Rais anacheza filamu nzima, tena kama muhusika mkuu katika harakati za kuendeleza sekta ya utalii.
Katika ya utalii ni sekta ni muhimu sana kwenye uchumi wa Taifa letu, ni sekta ya kuvalia njuga hasa kwani ni sekta ambayo inaliingizia Taifa dola bilioni 2 za kimarekani kwa mwaka, sawa ni Tsh trilioni 4.6 za kitanzania.
Kupitia filamu hii, Tanzania itazamia kupokea watalii milioni tano kwa mwaka ifikapo 2025 kutoka watalii takribani milioni mbili kwa sasa. Pia Tanzania inategemea kuingia USD bilioni 6 kwa mwaka, sawa na Tsh 13.8 za kitanzania kwa mwaka, kutoka trilioni 4.6 kwa sasa.
Idara ya Takwimu ya Taifa (NBS) inaonesha kati ya Jan - Oct 2022 watalii 1,175,697 wameingia nchini, tofauti na watalii 716,741 wa kipindi kama hicho mwaka 2021, ambapo ongezeko hilo ni sawa na 64%.
NBS inasadiki ya kwamba ongezeko la watalii nchini ni matokeo ya filamu ya Royal Tour, mfano kwa mwezi Octoba 2022 tu, walii walioingia nchini walikuwa ni 141,517 tofauti na 92,345 kipindi kama hicho 2021, ambapo ni sawa na 53.2%.
Kutoka Ulaya, Tanzania imepokea watalii wengi zaidi kutoka Ufaransa (12,553), Marekani (9,097), Germany 98,874), UK (6,614) na Italy (4,557).
Watalii hao katika mahojiano mbalimbali wakisadiki ya kwamba wao ni mara ya kwanza kuingia Tanzania, na wamevutiwa zaidi kutembelea Tanzania baada ya kutazama filamu ya Royal Tour.
Filamu ya Royal Tour bado inazidi kuoneshwa katika kumbi za sinema kwenye mataifa mbalimbali, huko mabalozi wetu wanafanya kazi kubwa kuhakikisha hilo. Sept 2022 ilioneshwa Sweden, na inazidi kuoneshwa zaidi kwenye nchi za Scandinavia.
Pia inatarajiwa kuanza kuoneshwa kwenye nchi kama Latvia, Finland, Denmark, Iceland, Lithuania, Estonia na nyingine nyingi za bara la Ulaya.
Filamu ya Royal Tour ni legacy ya Rais Samia Suluhu itakayoishi milele, faida zake hazitoishia kwakwe tu, bali hata kwa viongozi wajao, watakuwa na wepesi katika kuutangaza utalii wetu, kwani barabara imara itakuwa tayari imeshachongwa mtangulizi wao, Mh Rais Samia Suluhu.