Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,184
- 5,102
Hakuna ambaye hapendi kuona mtoto au kijana wake akipata maarifa bora na elimu ambayo mwisho wa siku itamsaidia katika maisha yake. Elimu ambayo inakwenda kumuinua zaidi mtoto na kumfanya awe msaada kwa familia, jamii na taifa kwa ujumla. Ni jambo zuri sana ukimuona mtoto wako akitumia maarifa yake kutatua matatizo ya kijamii, na hili sio jambo la ghafla au ajali tu, bali ni jambo ambalo tunapaswa kulianza kulifanyia kazi kuanzia msingi.
Elimu ni ufunguo thabiti katika kufungua milango migumu ndani ya jamii, Tanzania itakuwepo mpaka vizazi kumi mbele nina uhakika huo kuwa uendelevu wa vizazi vijavyo vinategemea sana kizazi hiki kinaishi namna gani. Kama watanzania tuna kila sababu ya kutengeneza mazingira bora na nchi jirani katika kutengeneza mahusiano mazuri kwa sisi pamoja na majirani.
Tutengeneze mahusiano mazuri ya kimkakati na mabalozi wa nchi rafiki pamoja na taasisi za kimataifa. Kwa mujibu wa tovuti kuu ya serikali, Tanzania ina jumla ya mabalozi 90 wanaowakilisha nchi zao, huku mabalozi wadogo wakiwa ni nane, pia tuna mashirika ya kimataifa zaidi ya 22. Takwimu hizi ukizitazama unaweza kuona hazina maana ila kuna thamani kuwa sana ya uwepo wa mabalozi hawa na uwepo wa wawakilishi wa taasisi za kimataifa ndani ya Tanzania.
Wazo langu ni kwamba kama Tanzania kupitia wataalamu waliopo Wizara ya Elimu watengeneze mifumo ambayo itaruhusu kutengeneza mahusiano mazuri na hawa mabalozi ambapo tuutapeleka watoto wetu nje ya nchi ili kupata maarifa.
Mfano, wanafunzi bora wa kidato cha nne, kidato cha sita pamoja na wale wa vyuo vikuu, tunaweza kuwaongezea uwezo kwa kuwapatia ufadhili wa kwenda kusoma nje ya nchi, kama vile Korea ya Kusini, au Japan huku tukiwa na lengo la kutengeneza kizazi bora cha watanzania ambao miaka ya mbele waje kusaidia kuleta maendeleo. Lengo kuu ni kuja kuwatumia katika kulisaidia taifa katika utatuzi wa matatizo.
Kutengeneza mifumo ya kuendeleza wanafunzi kwa kuzingatia mahitaji muhimu.
Ni suala la msingi kuwapatia elimu watoto na vijana huku tukiwa tunafahamu kuwa zao hili litakuja kutumika vizuri sio kuhitimu na kurejea nyumbani. Uwepo wa NACTVET umekuwa ni msingi bora sana sambamba na ule ambao uliwekwa na VETA ila je baada ya kuhitimu mafunzo hawa vijana tunawatumia wapi? Kuna vijana wengi sana wapo wanasoma kozi mbalimbali kwenye vituo vya ufundi VETA ila ukiwauliza kuhusu maisha baada ya kumaliza mafunzo, kinachofuata ni kigugumizi kikali sana, tuna imani kuwa tunahitaji elimu ambao watoto na vijana wetu watafahamu kuwa watafanya nini punde tu baada ya kuhitimu.
Tanzania imekuwa ikipata nafasi ya kupeleka watu kwenda kusoma kupitia fadhili mbalimbali kama KOICA, JICA, NDC, UKAID, na wengine ila ajabu huwa wanakwenda watu ambo wanaishia kutalii pekee na wakirudi hawaleti mabadiliko yoyote ya kiutendaji, mtu kapelekwa na JICA kusoma elimu ya uzamivu katika Disaster Management Policy lakini mafuriko yakipiga Dar es Salaam, Arusha na sehemu zingine hawa watu wala hana msaada wa kitalaamu, kumbe mwamba aliishia kwenda kutalii Fushimi Inari Taisha, Bustani ya Shinjuku Gyoen pamoja na kula Sushi, Yakitori, kunywa masupu ya Miso pamoja na Tempura.
Kuwajengea uwezo vijana kujitolea kimataifa haswa katika balozi za Tanzania katika nchi rafiki.
Wengi wanaifahamu kwa jina la Internships ila sio jambo jipya kusikia kazi ambayo TAESA wanaifanya katika kuwajengea mazingira mazuri vijana waliohitimu na wenye uhitaji wakupata uzoefu. Sisi kama Tanzania tunaweza kuwajengea uwezo wahitimu kupata uzoefu huku wakiendelea kuwa wazalendo, moja ya njia ambayo ni nzuri ni kuwaruhusu kuzunguza na kupata msukumo mpya wa maisha nje ya Tanzania.
Mhitimu akifanya kazi kwa mwaka mmoja kwenye Ubalozi wa Tanzania pale Brazil na kupata uzoefu wa kutazama kazi za ujenzi kutoka makampuni ya ujenzi kama vile Cemex Ventures, Oderbrecht, Camargo Correa na kadhalika, hii fursa itampatia ujasiri wa kuja kufanya kazi kwa wepesi kwenye makampuni ya hapa nyumbani.
Wale vijana wanaomaliza Aquatic Sciences pale UDSM ukiwapatia fursa ya kwenda kupiga kambi Canada kwa mwaka mmoja tu na kujifunza kazi zinazofanywa na Canfisco, Labrador pamoja na Cooke Aquaculture, wakirudi watakuwa ni msaada tosha kwendye kuendeleza shughuli za uvuvi katika maziwa yetu.
Kuna nukuu moja maarufu sana kuwa “Internships are a fantastic way for students to gain real-world experience.” vijana waliosoma PSPA wapewe nafasi ya kuwa na uzoefu wa kimataifa, hata akirudi nyumbani basi asiwe na uoga wa kuomba kazi kwenye ofisi na taasisi za kitaifa, kama umefanya kazi Ubalozi wa Tanzania pale Urusi, akiwa chini ya Usimamizi wa Mheshimiwa Fredrick Ibrahim Kibuta, ebu chukua picha kwenye wasifu wako unaonesha kuwa ulifanya kazi kwenye ubalozi wa Tanzania ambao ulikuwa unafanya kazi sio tu na Urusi bali na Belarus pamoja na Georgia.
Kuimarisha misingi ya Alumni Networks.
Binafsi shule nimesoma ngazi za Sekondari pamoja na High School mpaka leo tuna umoja wetu ambao tuna kundi la mtandao wa Whatsapp na tunawasiliana kwa zaidi ya miaka sita sasa, kupitia kundi letu tunabadilisha fursa nyingi sana, kazi za muda mfupi, kazi za muda mrefu pamoja na kukutana mara kadhaa kujadili kuhusu harakati za maisha. Uwepo wa Alumni Networks kwa wengine wanaweza kuona kama hazina kazi za msingi ila ukweli ni kwamba endapo watu wakitumia hizi nafasi ya kuwa ndani ya Alumni Networks basi unaweza kujikuta unapata uzoefu wa jambo fulani kwa wepesi sana. Kumaliza na kuhitimu ni jambo moja ila kufahamu kinachoendelea kwenye kozi uliyosoma ni jambo jingine.
Kuna fursa nyingi sana zipo kwenye hizi Alumni Networks za vyuo kama UDOM, Mzumbe, UDSM, SAUT, Mwenge, City College, ZION pamoja na vyuo vingine ambavyo baadhi ya fursa na taarrifa hazitoki nje kirahisi.
Wapeni nafasi vijana kwenye mabaraza pamoja na majukwaa ya ushirikiano wa kimataifa.
Kama ambavyo serikali inatangaza na kutoa maagizo kuwa wanafunzi wavae sare na kubeba bendera kwenda kusikiliza wateule wao kwenye mikutano ya hadhara basi tusiogope kuwakusanya vijana wetu kwenda na kuongozana nao kwenye mabaraza na majukwaa ya kitaifa ili wapate uzoefu wa kukutana na watu mashuhuri na wenye maamuzi.
Kama kuna kongamano la OPEC basi Waziri Prof. Makame Mbarawa ongozana na wanafunzi bora watatu kutoka kozi ya Petroleum Engineering kutoka UDSM ungana nao katika msafara, kama kuna mkutano wa Mazingira chini ya UNEP basi Daktari Ashatu Kachwamba Kijaji ongozana na wanafunzi wawili watatu kutoka kozi ya Environmental kutoka chuo cha Ardhi.
Kama kuna Tamasha la Muziki, Sauti za Busara basi Dakatari Damas Ndumbaro ishauri serikali iwe inawasafirisha wanafunzi kadhaa kutoka Idara ya Muziki UDSM, Bagamoyo au Chuo cha Tumaini wapate kujifunza kuhusu sanaa.
Hizi Gladiators Summit pamoja na Expo zitumike kuwajengea uwezo vijana ambao wamekwisha kuhitimu masomo ya Uhandisi ili waone namna bora za kutumia ujuzi wao katika kuijenga nchi. Viongozi mkienda Dubai World Trade Centre, Daktari Seleman Jafo pamoja na Mheshimiwa Exaud Kigahe msisahau kwenda na wanafunzi ambao ndo watakuja kushika hizo nafasi miaka kumi ijayo katika sekta ya viwanda na biashara.
Nina imani kuwa tuna jukumu kubwa sana la kuitengeneza Tanzania endelevu, Tanzania ambayo wajukuu wa vitukuu vyako wakiona picha yako basi watajivunia sana wewe, watajivunia kuwa ulikuwa sehemu ya kipekee sana katika uendelevu wa maisha ya vizazi na vizazi. Hatuna budi kutumia uwepo wa mabalozi na ushirikiano wa kimataifa katika kuiendeleza nchi yetu, sio lazma tuwapeleke vijana MIT, Princeton au McGill ila vijana kupata mazingira mapya kunaweza kuwaongezea uwezo wao wa kufikiria njia mbadala za utatuzi wa matatizo ndani ya jamii.

SIO KWA UBAYA!