Namibia yatangaza kuwauza tembo kwa mnada

Namibia yatangaza kuwauza tembo kwa mnada

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Wizara ya mazingira ya Namibia imesema kwamba serikali ya nchi hiyo inapanga kuuza ndovu 170 kutokana na hali mbaya ya kiangazi na idadi kubwa ya ndovu katika nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika.

Tangazo la kuuzwa kwa ndovu hao limetolewa na shirika la habari la serikali la New Era ambalo limeripoti kuongezeka kwa visa vya ndovu kushambulia binadamu na ndovu hao kuwa katika hatari ya kutoweka kutokana na uwindaji haramu pamoja na sababu za kimazingira.

Wizara ya mazingira, misitu na utalii imesema kwamba itauza ndovu hao kwa mnada kwa mtu yeyote ndani ya Namibia au nje ya nchi chini ya mpangilio maalum utakaowekwa kuhusu mahali ndovu hao watawekwa iwapo wananunuliwa na mtu ndani ya nchi.

Raia wa nchi nyingine wanaotaka kununua ndovu hao, wanatakiwa kuonyesha idhini ya maafisa nchini mwao kwamba wanaruhusiwa kuingiza ndovu hao nchini mwao.

Idadi ya ndovu imeongezeka kwa kasi nchini Namibia, kutoka 7,500 mwaka 1995 hadi 24,000 mwaka 2019.
 
Kwani meno yao siku hizi hayaongezi mambo ya mkongo Dust mbona wanawaacha sana wanafeli wapi hao jamaa.
 
Si rahisi kusafirisha mnyama kutoka nchi moja kwenda nyingine. Vibali vyake ni vingi sana, kwa mfano, wizara husika iwe na uhakika unampeleka wapi mnyama huyo, vipimo vya mardahi ya mnyama ili asijekuwa na maradhi, namna utakavyomsafirisha bila kuleta madhara yo yote kwa watu wengine. Vile vile kama una zoo, ina usalama kiasi gani kwamba hatatoroka kwenda sehemu tofauti.

Kama mnakumbuka Rais Magufuli alishasema watu waombe vibali wafungue vibali lakini nadhani mahsrti yake ni magumu na lazima uwe na mtaji wa kutosh kuhakikisha ulinzi wa wanyama hao ili asije kudhuru watu. Mfano, Tembo mmoja akitoroka kwenye hifadhi inabidi wale whausika wamsake kabla ya kuleta madhara kwa jamii inayozunguka hifadhi au zoo.
 
Back
Top Bottom