bigmind
JF-Expert Member
- Oct 28, 2015
- 12,457
- 12,682
- Thread starter
- #61
Unajua unachekesha sana, dini ya biblia maana yake ni nini..? Naomba unitafutie ni lini na wapi na kwa jinsi gani kanisa Katholiki (Universal church) lilipata kugain power na kuongoza dola ya kirumi. Yaani Papa kuwa kiongozi wa dini na nchi...?Nitaandika kwa uchache hio habari ya WAWALDENSIA WAITETEA IMANI.
Katika kipindi kirefu cha utawala wa papa, walikuwepo mashahidi wa Mungu ambao walikuwa wanaithamini imani kwa Kristo kama mpatanishi pekee kati ya Mungu na wanadamu.
Walikuwa wanaiamini Biblia kama kanuni pekee ya maisha, na kuitakasa sabato ya kweli.
Walikuwa wakiitwa waasi maandishi yao yalipigwa marufuku yakapotoshwa na kukataliwa, lakini walisimama imara.
Haawa hawatajwi sana katika kumbukumbu za wanadam, isipokuwa katika tuhuma kutoka kwa watesi wao. Kanisa la Roma lilikuwa linataka kuangamiza kila ambacho lilikuwa linaona kuwa ni "uasi" kiwe ni watu au maandishi.
Kanisa la Roma pia liliamua kuharibu kumbukumbu zote za ukatili wake dhidi ya wale waliokuwa na maoni tofauti. kabla ya kugunduliwa kwa elimu ya uchapaji, vitabu vilikuwa vichache, kwa hiyo kulikuwa hakuna jambo la kulizuia kanisa kutimiza makusudi yake. Mara baada ya utawala wa papa kupata madaraka lilianza kuwaangamiza wote waliokuwa hawataki kukubaliana na utawala wake.
Roma yakabiliana na Dini ya Biblia.
Kanisa la Roma liliazimu kuiweka Uingereza chini ya utawala wake. Katika karne ya sita wamisionari wa kanisa la Roma walianza kuwang'ia watu wa Saxony waliokuwa wapagani.
Sasa roho ya kweli ya utawala wa papa ilidhihirika, kiongozi wa kirumi akasema " Kama hamtawapokea ndugu watakaowaletea amani, basi mtapokea maadui watakaowaletea vita" vita na udanganyifu vilitumika dhidi ya mashahidi hawa wa imani ya Biblia, hadi makanisa ya Uingereza yalipoharibiwa na kulazimishwa kumtii papa.
Nitaendelea
Nafanya rejea tu ya hiki kitabu tuifikie namba 666 tuone Ellen anasema nini
Sent using Jamii Forums mobile app