Nakusudia kufungua kesi ya madai

Kufungua madai kwa maoni yko umefkilia TORT (Malicious p) ili kufungua tort muda ni 3 years je jiulize kwan ameweka alitendewa lini????? Ili kujua LIMITATION OF ACTION muda hajaonesha halaf unakurupuka maelezezo yanajitosheleza.

Je anadai kiasi gan????? Pecuniary Jursdiction. Mwache mkurupuke akaktane na P.O halaf alipe gharama!!!
Kesi ilianza Novemba 24/11/2016 na kuisha tarehe 22/3/2017.
 
Mkuu Ndomaana Nikasema Atoe Mazingira Na Scenario Nzima Iwe Disclosed. Labda Hatuamini Au Anaona Uvivu Kuandika. Maelezo Yake Yako Too Vague,Na Hayakupi Mtu Mwanga Wa Nini Unafanya. Btw Niliposema Sanasana Sikumaanisha Solerly Ni M-P. Afterall Hawa Ndo Wateja Na Apo Ana Hasira Anataka Kukomoa Au Alikua Hajui Kaambiwa Anaweza Kulipwa Akachangamkia Fursa Kisa Kuna Fedha Ndo Kaja Apa Aone Uwezekano Upo Wa Kupiga Iyo Ela.
Pamoja Katika Sheria!!
Walifika polisi wawili wakiwa na wazazi wa mtoto husika,pamoja na mwalimu wa shule anayosoma huyo mtoto.Mtoto mwenyewe aliyeelezwa kuwa kabakwa ana umri wa miaka 7 mpaka 8.
Walifika nyumbani kwangu na kumkuta mtoto wangu wa kike na kuulizwa na askari ambaye alivaa kiraia kama kuna mvulana mwanafunzi wa shule fulani.Alipowajibu kuwa yupo waliomba picha yake na yule mtoto wangu akaingia ndani akawapa.
Waliichukua na kumuonyesha yule mtoto ambaye alikuwa analia kwa kipigo toka kwa polisi,na kumuuliza ni yupi aliyembaka ni yupi ambapo kulikuwa na watu wawili akamwonyesha mtoto wangu ambaye alikuwa amevaa sare ya shule.
Wakaondoka mpaka shuleni na kuomba wafanye gwaride la utambuzi(Identification Parade).Walifanya na mtoto hakuweza kumtambua japo askari aliyekuwa anaendesha gwaride alipofika alipokuwa amesimama huyo kijana alisimamishwa na askari na kuonyeshwa kwa kidole kama hamtambui.Mtoto wa kike alikataa kumfahamu muhusika.Ila mwisho yule alimtaja kijana mwingine.Polisi walimchukua yule kijana wakamuhoji kwenye ofisi ya mwalimu kisha wakamuacha.
Baada ya hapo polisi walimwambia mwalimu kuwa tunaomba kuondoka na mwanafunzi ambaye tunayo picha yake,japo kwenye gwaride hakutajwa.Mwalimu aliwahoji kivipi wakasema tunakwenda kujiridhisha.Aliombwa na mwalimu kuandika alichofanya pale shuleni kwenye Logbook ya shule.Alikubali kuandika, ila kabla ya kuondoka pale shuleni yule polisi aliwaweka pamoja mtoto wangu na yule mtoto aliyesemwa amebakwa na kuwakutanisha na kumuuliza hata kama anamfahamu tu mtoto alikana kumfahamu wala kumuona.
Cha ajabu bado polisi waliondoka na mtoto wangu mpaka kituo cha polisi,ambapo alihojiwa na askari wa upelelezi na wote wakakubaliana kuwa yule kijana hahusiki na tukio lile.
Kwa pamoja waliafikiana kumuachia ila wakamwambia aje baada ya wiki moja.
Siku ya pili katika hali isiyoeleweka aliitwa tena kituo cha polisi na kufanywa gwaride kwa mara ya pili yule mtoto ndio akamtaja mtoto wangu kuwa ndiye aliyembaka.
Baada ya hapo akawekwa ndani na kunyimwa dhamana mpaka siku ya tatu akapelekwa mahakani na kushitakiwa kwa kosa la kubaka.Tukamtoa kwa dhamana mahakamani.
Kesi ikaanza kusomwa, PH tu ilichukua wiki tatu mwendesha mashtaka kila ikisomwa anasema upelelezi haujakamilika.Mpaka hakimu alipoanza kuwafokea.
Maelezo ya awali(PH) yaliposomwa mashahidi ikawa kazi kuja waliitwa mara nne bila kufika mara ya tano wakaja mashahidi baadhi.Kesi ilianza lakini huyu mtuhumiwa alisimama imara sana kuuliza maswali mashahidi mpaka wengine kuchanganyikiwa na wengine kuhamaki mahakamani.
Huyu kijana alifanyakazi nzuri sana maana mpaka askari wenyewe walikwama katika maswali aliyokuwa anauliza.
Kifupi aliwashinda mashahidi wote na hawakuwa na hoja aliyemaliza kazi ni mtoto mwenyewe aliiambia mahakama kuwa hakubakwa ila walikuwa wanamlazimisha aseme kisichokuwepo.
Shahidi wa mwisho daktari aligoma kabisa kuja mahakamani pamoja na kuitwa mara 4 hakutokea mahakamani.
Ikamlazimu hakimu kufunga ushahidi na kutoa hukumu kwa kuzingatia mashahidi waliopo na kufuta kesi.
HITIMISHO
Kinachonipa uchungu ni muda niliopoteza,mtoto kapoteza mwelekeo katika masomo ukizingatia alikuwa na uwezo mkubwa sana darasani,na huu ni mwaka wake wa mwisho.Zaidi ya yote familia imepata athari kubwa kiuchumi na kijamii.Nimepoteza kazi ambayo ilikuwa nilipwe zaidi ya laki 6 kwa mwezi kutokana na kesi hii.
 
Sanasana Ni Malicious Prosecution.. Ila Kama Kulikuwa Na Probable Cause Kesi Inaweza Kufeli. Kwa Mfano Huyo Kijana Alionekana Na Mbakwaji Muda Mchache Kabla Ya Tukio Kufanyika.
Ila Ungetoa Mazingira Yalivyokua Na Mwenendo Mzima Itasaidia Hata Kukuambia Kama Itawezekana Au Lah!!
Ni baada ya siku 7 ndio alikamatwa
 
Kuna uthibitisho kwamba mbakwaji alibakwa? Kesi ilitupiliwa mbali kwa sababu ya uzembe wa prosecutor? Alikuwa aquitted au ni nole prosequie? Angalia usije sababisha kijana akajikuta ana hatia.
Hakubakwa hilo lilithibitishwa katika ushahidi wa mama wa mtoto kwani yy ndio alimchunguza kabla kwa kusema alimkuta mwanawe ana michubuko na uvimbe hakukuwa na mbegu.Pia hospitali alipimwa siku ya pili.
 
Achana na hayo mambo. Maadam kesi imeshakwisha usipiende kujiingiza kwenye matatizo yasiyo na tija... Unaweza kufungua kesi ya madai alafu fidia utayopata utaambiwa tu jeshi likuombe radhi na kukusafishia familia yako... Hapo utakuwa umeshatumia pesa nyingi sana na hussles za kutosha...
Hasa nilichotaka hasa ndio hicho kwani familia yangu imevunjiwa heshima sana.Na kuonyesha jinsi askari wetu walivyokosa weledi ktk upelelezi.Wamenikosea sana.
 
Kufungua madai kwa maoni yko umefkilia TORT (Malicious p) ili kufungua tort muda ni 3 years je jiulize kwan ameweka alitendewa lini????? Ili kujua LIMITATION OF ACTION muda hajaonesha halaf unakurupuka maelezezo yanajitosheleza.

Je anadai kiasi gan????? Pecuniary Jursdiction. Mwache mkurupuke akaktane na P.O halaf alipe gharama!!![/QUOTE

Kama we ni wakili mzuri hukutakiwa at first umuulize nini anadai kwa sababu amekupa scenario ili wewe uone available remedies katika situation yake. unachotakiwa ni kumuuliza zaidi na kwa undani haswa ili uone maelezo yake yana-fit katika wapi na sio kumuuliza anachodai. Yeye anaona mwanae kaonewa lakini hafahamu haswa ni namna gani ya kupata kile anachodhani anastahili kama haki.

Hivyo, kama wataka kumsaidia nenda inbobo uchukue maelezo zaidi utengeneze kesi yako ila usimuulize
"uwe mwazi (open) unachotaka udai" yawezekana hajui kabisa.
 
Mtoto wangu ambaye yupo kidato cha nne sasa mwaka jana alizushiwa kesi ya KUBAKA ktk mazingira ya ajabu sana.
Tulienda na kesi mpaka mwisho ilitupiliwa mbali baada ya polisi ambao ndio mashahidi wa Jamhuri kushindwa vibaya kuthibitisha chochote.
Nakusudia kufungua kesi ya madai.Wapi nitapata msaada wa kisheria?
Ulichoomba ni kuelekezwa mahali pa kupata msaada wa kisheria..
Nenda kwa wakili au mwanasheria aliyepo karibu na eneo lako, usiende na story tu bali uende na nakala ya hukumu pamoja na vielelezo vilivyotumika wakati wa kusikiliza shauri la ubakaji (kama vipo)..
Pia unaweza kuweka nakala ya hukumu hiyo hata hapa ili watu wanapokushauri watoe ushauri huku wakijua uhalisia wa tukio hilo..na maswali yatayofuata yatakuwa ni machache maana story inakuwa ipo kwa ufupi kwenye hukumu..
 
Si unaenda kwa mmkuu wa mkoa kuna wanasheria wa kusaidia raia.
Hapana, kwa mkuu wa mkoa wanasheria waliopo ni kwa ajili ya kumshauri RAS na kusimamia masuala yote yahusuyo sheria kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa.
Wanaweza kumsaidia kwa makubaliano (kwenye ofisi zao nje ya serikali) maana shida hiyo ni ya binafsi (sio ya ofisi ya mkuu wa mkoa wala ya kiserikali)..hivyo aende huko akijua kuwa sio haki yake kusaidiwa na hao wanasheria
Lakini pia wanasheria wa serikali hawaruhusiwi kuendesha kwa namna yoyote ile kesi yoyote dhidi ya serikali.
 
Hapana, kwa mkuu wa mkoa wanasheria waliopo ni kwa ajili ya kumshauri RAS na kusimamia masuala yote yahusuyo sheria kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa.
Wanaweza kumsaidia kwa makubaliano (kwenye ofisi zao nje ya serikali) maana shida hiyo ni ya binafsi (sio ya ofisi ya mkuu wa mkoa wala ya kiserikali)..hivyo aende huko akijua kuwa sio haki yake kusaidiwa na hao wanasheria
Lakini pia wanasheria wa serikali hawaruhusiwi kuendesha kwa namna yoyote ile kesi yoyote dhidi ya serikali.


Upo nyuma sana kwenye maalumati ya yanayoendelea nchini.

Upo mkoa upi? Labda huko ulipo bado halijafika hilo. Dar tayari. Fatilia.
 
Upo nyuma sana kwenye maalumati ya yanayoendelea nchini.

Upo mkoa upi? Labda huko ulipo bado halijafika hilo. Dar tayari. Fatilia.
Hao wa Dar ni wanasheria binafsi wa mkuu wa mkoa (yaani anawalipa yeye kwa fedha yake binafsi)..sasa hata huko Dar wameanza juzi tu na kwa maana hiyo mikoa mingine hawapo kwa sababu sio lazima wawepo..na hao wa Dar uwepo wao ni pamoja na uwepo wa Makonda..ikitokea ameacha kuwa mkuu wa mkoa kwa sababu yoyote ile inawezekana wasiendelee kuwepo hapo
Ila nitashukuru ukitueleza vizuri kama unazungumzia wanasheria wa Makonda au wanasheria wa ofisi ya mkuu wa mkoa
 
Lawyers should not decide on behalf of clients what do they think, Lawyers should remain advice on SUBSTATIVE & PROCEDURAL on what clients decide (e.g to wave) clients should express TO LAWYERS what service do they seek for assistance.

Huu uanasheria Njaaaa ili mteja atake wewe unavyotaka ili upate hela hata ya ku-draft PLEADINGS ili uishi mjini na upate KODI ya ofsi HAIFAI kamwe.

Nenda LST kwanza upate ethics za fani!!!!
Hahahahahahahahaha,,noted msomi
 
Back
Top Bottom