Nakumbuka zamani

Ahsante sanaaa!!!! Ila ungemuuliza zamani yake ni lini?? Maana kuna wengine zamani yao ni mwaka 2005 atiii!!!!

Ninachojua mie kwenye saluni zamani ilikuwa ni chini ya miti na kiwembe alafu chenyewe ni kimoja kinaweza kula vichwa 20 kijijini!!!!

na issue za kuambukiza hazikuwepo, enzi hizo ni VD tu, ukimeza rangi mbili issue inaisha mwilini
 
enzi za club mambo leo shooooooooow!! jioni hiyo na huku unakamua pilsner baridi

enzi hizo hakuna mafisadi lakini
 
ahsante sanaaa!!!! Ila ungemuuliza zamani yake ni lini?? maana kuna wengine zamani yao ni mwaka 2005 atiii!!!!

Ninachojua mie kwenye saluni zamani ilikuwa ni chini ya miti na kiwembe alafu chenyewe ni kimoja kinaweza kula vichwa 20 kijijini!!!!

hata jana ni zamani
 
Nakumbuka siku ya mechi ya Simba na Yanga wenye redio zao kubwa na maspika ya muziki huyafungua na kuweka nje ili hata mtu aliyeko mbali kiasi gani na majukumu yake asikie matangazo. Siku hizi aahhh!!! wapi, English Premier Leaguee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


-Halafu tulikuwa tunarekodi matangazo hayo ya mpira, siku ukitaka kujikumbushia jinsi Omary Hussein alivyowatungua SSC au Jumanne Hassan "Masimenti" alivyowatungua Yanga, basi unafungulia redio yako kwa sauti kuuuuuubwaa!

-Ninakumbuka pia tulikuwa na daftari au vitabu tunabandika picha za wachezaji wa timu tunayoipenda, zilizotoka kwenye magazeti (enzi hizo uhuru, mzalendo, daily news, sunday news na sana sana mfanayakazi ukiliwahi jumaooosi), wengine walikuwa wanabandika picha hizo kwenye kuta za vyumba vyao!!

Natamani kulia nikikumbuka zamani zileeeeeee!!
 
zamani zile bana ilikuwa raha sana nakumbuka nil;ivyoanza sec nilikuwa naandika nyimbo za wanamuziki na kubandika picha zao yani naushika wimbo mzima,pia wakati namaliza primary tulikuwa na vijitabu tunaandika fareware kwenye vitabu,vile vitu unavyovipenda na usivyopenda
 
Zamani ukipewa shilingi tano au ukiokota shilingi tano unapata pipi Tanoooooooooooooo!
 
Aaah! Zamani ukiona gari yenye rangi nyekundu au ambulance utatimua mbio kwa kuepusha kunyonywa damu.
Usiombe hayo magari yapite karibia na shule wakati wa vipindi.
Masomo yatasitishwa kwa muda.
Nyonya damu.
 
Zamani nakumbuka disco mbowe,vision,tku disco rungwe ocean,nawakumbuka madj eg jpp,john bure,DAN STAR,PAUL MC GHEE.SWEET Cofee,EDD SALLY,DOUBLE K,ilikuwa raha
 
Kwa sisi wa miaka ya sitini ilikuwa tunakwenda shule tumevaa viatu, ila tukirudi nyumbani viatu vimehifadhiwa mpaka siku ya pili ya kwenda shule. Mitaani kote ni peku peku tu, ukijikata na kigae cha chupa basi ni mafuta ya moto hapo ulipojikata au ulipojichoma mwiba.

Jee kuna wale wanaomkumbuka Leonard Mambo Mbotela na kipindi chake cha radio "jee huu ni uungwana?". Kilikuwa ni kipindi cha visa vinavyotokea Nairobi na kilikuwa kinatangazwa kila Jumapili saa saba na robo (sikumbuki ni station gani), lakini kilikuwa na tangazo la biashara 'Aspro ni dawa kweli, Aspro ni dawa kweli, hutuliza maumivu kwa mara moja'
 
Back
Top Bottom