Nakosoa: Si sahihi kufuta kila posho na mafunzo kwa watumishi wa umma

Mimi ni mtumishi wa umma,sijawahi lipwa posho yeyote.Posho hutolewa kibaguzi na kujuana.Semina zinatolewa kwa wale wateule wa mabosi.Hivyo kama kuishi kama mashetani tumezoea,wazitoe tu ili na wengine waonje maisha yetu ya kimapepo.
 
Tatizo letu lingine sisi watanzani tumejengeka kwa kutofuata sheria na taratubu za kazi. Tunaleta sana kujuana makazini. Tuwabinafsi sana. UBINAFSI NDIO SUMU YA MAENDELEO.Htupendani hatufikiriani.viongozi wanajifikuria wao wenyewe na watu wao wakaribu..
 
Mstari unaotenganisha watumishi wanaostahili posho na huduma mbalimbali unapita wapi? Wakuu wa wilaya, mikoa na mawaziri ni watumishi wa uma au la? Wanastahili posho na huduma au na kwao zimefutwa?
Mambo mengine hayahitaji matangazo na matamko, yanahitaji marekebisho ya ndani kwa ndani kulingana na hali halisi ili kuongeza ufanisi.
Ni muhimu viongozi wakajua kuwa vyeo ni dhamana tu na siyo hati miliki za nafasi wanazotumikia kwa wakati huo.
Na wanaofurahia kuwa heri tukose wote hawaangalii upande wa pili kuwa mtaani hela inazidi kuadimika. Riziki ya mtu ipo kwa mtu. Angalia wenye biashara na wajasiriamali mfb wamilikiwa mahoteli wanalalamikia ugumu wa biashara kwa kuwa safari zimebanwa..posho hakuna vikao hakuna. Mwenye busara hawezi kufurahia kuondolewa kwa posho ambayo ilipitishwa kisheria. ( naongelea posho halali sio wizi)
 
Ila mm nlimuelewa sana aliposema mapato yanakusanywa na wafanyakazi wengi lakini bajeti ya chai na vitafunwa ni kwa wachache wanaojiita wakubwa hili kweli ni tatizo kumekuwa na matabaka yaan wale wanaofanya kazi nzito mshahara kidogo na hakuna posho ila kwa hao wakubwa wenye mishahara mikubwa ndo kwenye chai na vitafunwa...
Kwani wao wakubwa waliofuta posho hawapati au kutafuna posho kuliko walio chini yao? matabaka hayaepukiki, bali kinachofanyika maskini au wanyonge watafikiri kwa faida yao bali ukweli ni kwa faida za kisiasa za wanaofuta posho.Period!
 
Chadema mtaacha lini kutetea ujinga?hizo posho wanalipana maafisa wachache ndani ya halmashauri ,watumishi wanaofanya kazi kama walimu,madaktari,manesi nk.hizo posho hawazipati posho ya Chai na vitafunwa inatafunwa kwenye majengo ya halmashauri tu hao watumishi wengine ambao ndiyo wengi hawazipati.
Ni bora wazitoe zikajenge madarasa,zahanati na Barabara.
Ukijua maana ya privileges haitakusumbua, ndio maana wakuu wa idara wana magari ya ofisi na wasio wakuu wa idara hawana
 
Kwa nchini kwetu Tanzania, kuwa mtumishi wa umma ni kuonesha uzalendo mkubwa. Hii ni kwakuwa, watumishi wa umma Tanzania wanalipwa mishahara kidogo kulinganisha na watumishi wa sekta binafsi.

Watumishi wa umma ni wazalendo kwelikweli. Hawarudishwi nyuma na mishahara na marupurupu yao kiduchu. Wanaendelea kujenga Taifa lao kupitia utumishi wao. Siyo siri, watumishi wa umma huishi kwa posho na mafunzo.

Watumishi wa umma huwa na amani moyoni wanapokuwa na 'viposho' vya hapa na pale. Hii ni kwakuwa, mishahara yao humezwa na mikopo,kodi za Serikali, michango katika mifuko ya hifadhi ya jamii,michango ya afya, michango ya vyama vya wafanyakazi na kadhalika.

Mtumishi anapopata 'kasafari' ka mafunzo ndani au nje ya Tanzania, huyasahau maumivu yake na kusonga mbele kuelekea kwenye kilele cha mafanikio yake. Kufutafuta kila posho au mafunzo kwa mtumishi wa umma ni kumuumiza maumivu yasiyoweza kupozwa.

Posho na mafunzo (visafarisafari) humpa chachu ya utendaji mtumishi wa umma. Mtumishi wa umma hastahili kuishi kama 'shetani'!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Natumikia taifa hili kwa miaka mingi kwa ofisi tofauti. Kwa nadhalia, ni sahihi hayo uliyoandika lakini kiuhalisia, hayo ni matumizi mabaya ya pesa za serikali. Mafunzo kazini iligeuka kuwa ni sehemu kubwa ya matumizi ya pesa za serikali, kuliko hata uwekezaji. Unawezaje kupata digrii ya chuo kikuu na baadaye ukiajiliwa unaonekana hujui kazi na kila siku unakuwa mafunzoni kwa miaka nenda rudi? Hata mtu mzoefu akiteuliwa kuwa mkuu wa wilaya, anaambiwa aanze na mafunzo, semina, kongamano, n.k. rubbish!

Tukubaliane kwamba, sisi watumishi au waajiliwa, tulistahili kuomba mishahara bora na siyo kuvizia safari na semina ambazo ni wateule wachache tu waliofaidi kwa miaka nenda rudi. Angalia mfano wa safari za nje. M-TZ gani anayeweza kutumia dola 450 kwa siku akiwa kenya, sawa na Burundi, sawa na London! Wizi tu! Wakati huo huo mashirika ya UN wanalipa dola 200!

Tusiwe wachoyo kutaka kuchota kila kitu. Haki yetu ni mshahara. Tudai mshahara na kwa kujisahau kwa sababu ya semina na safari, waajiliwa wa serikali tulishindwa kudai mishahara bora. Sasa tuisome namba na tudai mishahara.
 
Hivi ni kweli rais na waziri mkuu wamefuta posho zao zote na kubaki na mshahara tu maana eti mshahara ndio haki yao? Ngoja tusubirie nawabunge ile sitting posho ,accommodation etc nazo zifutwe maana nao wana mshahara wanaolipwa kwa kazi yao
 
Unapotangaza kufuta posho za wenzako ilhali wewe unaendelea kuvuta za kwako huo ni zaidi ya ukoloni wa kijerumani. Asee mtawala mweusi hatari.
 
Natumikia taifa hili kwa miaka mingi kwa ofisi tofauti. Kwa nadhalia, ni sahihi hayo uliyoandika lakini kiuhalisia, hayo ni matumizi mabaya ya pesa za serikali. Mafunzo kazini iligeuka kuwa ni sehemu kubwa ya matumizi ya pesa za serikali, kuliko hata uwekezaji. Unawezaje kupata digrii ya chuo kikuu na baadaye ukiajiliwa unaonekana hujui kazi na kila siku unakuwa mafunzoni kwa miaka nenda rudi? Hata mtu mzoefu akiteuliwa kuwa mkuu wa wilaya, anaambiwa aanze na mafunzo, semina, kongamano, n.k. rubbish!

Tukubaliane kwamba, sisi watumishi au waajiliwa, tulistahili kuomba mishahara bora na siyo kuvizia safari na semina ambazo ni wateule wachache tu waliofaidi kwa miaka nenda rudi. Angalia mfano wa safari za nje. M-TZ gani anayeweza kutumia dola 450 kwa siku akiwa kenya, sawa na Burundi, sawa na London! Wizi tu! Wakati huo huo mashirika ya UN wanalipa dola 200!

Tusiwe wachoyo kutaka kuchota kila kitu. Haki yetu ni mshahara. Tudai mshahara na kwa kujisahau kwa sababu ya semina na safari, waajiliwa wa serikali tulishindwa kudai mishahara bora. Sasa tuisome namba na tudai mishahara.
Umemaliza mkuu,ilifika mahali huku ofisini pesa yeyote inayoingia lazima mafungu ya posho yatengwe kwanza ndio za maendeleo zifuate.
Isitoshe hizo posho zinagusa kundi Dogo sana la watumishi ambao tayari wana privileges nyingi.
Japo siipendi CCM ila kuna mambo nayaunga mkono na ndio tulitegemea UKAWA wakayafanye tukiwachagua.
Posho zinashusha sana utendaji wa kazi serekalini.
 
Chadema mtaacha lini kutetea ujinga?hizo posho wanalipana maafisa wachache ndani ya halmashauri ,watumishi wanaofanya kazi kama walimu,madaktari,manesi nk.hizo posho hawazipati posho ya Chai na vitafunwa inatafunwa kwenye majengo ya halmashauri tu hao watumishi wengine ambao ndiyo wengi hawazipati.
Ni bora wazitoe zikajenge madarasa,zahanati na Barabara.
Maelezo yako yameeleweka vizuri saaana mkuu.
Posho za viongozi zinarudisha saana maendeleo ya halmashauri husika Waziri mkuu ameliona mapema wananchi tusubiri tu maendeleo katika hamashauri zetu.
 
Ndiyo!
Hata baada ya miaka 100, Posho nitazilaani. Mkutano Posho, Kupanga bajeti posho, safari za nje ikawa ni sehemu kubwa sana ya kazi za wakuu wa idara na wizara.
Nasikia siku hizi wanakaa semina za ndani ya nchi kwa siku hata 5 bila kukosa.
 
Unapotangaza kufuta posho za wenzako ilhali wewe unaendelea kuvuta za kwako huo ni zaidi ya ukoloni wa kijerumani. Asee mtawala mweusi hatari.
Kwa hiyo unataka uruhusiwe kuchota posho kama yeye?
Uliposikia ukurugenzi ulifurahia ukiamini sasa posho zitakoma! Sasa tunasubiri taarifa ya CAG ili ifanyiwe kazi.
 
Kwa hiyo unataka uruhusiwe kuchota posho kama yeye?
Uliposikia ukurugenzi ulifurahia ukiamini sasa posho zitakoma! Sasa tunasubiri taarifa ya CAG ili ifanyiwe kazi.
Sasa nani asiyependi mafedha. Sheria iwe msumeno sio shoka.
 
Back
Top Bottom