Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,040
- 43,766
Hii nchi ukiwa na pesa utaendelea kuwa tajiri kwasababu maskini hana mteteziMamlaka zimelala,hizi applications zimekua nyingi sana,ni watakatishaji fedha wa wazi..BOT wamechelewa sana kuchukua hatua,hawa jamaa wana ukwasi wa hatari! Wanatumia umasikini na ujinga wa watanzania kuwaibia..
Mtanzania akiwa na shida we mpe form ya vigezo na masharti wala hatasoma,ataishia kusaini tu,na hapo ndio mnapopigwa! Huwezi kuamini wanasema Tanzania kuna pesa za bure..angalia pia kwenye makampuni ya kamari! Na msitegemee hali kubadilika kwa sababu kuna wakubwa wananufaika na pia wapo kwenye payroll ya hawa mabwana.