Umeona ehhh! Ukichambua soka ktk upande wa kushabikia mar zote utashindwa kuleta maana.Tukubali tu katae , mpira utabaki kuwa mpira tu
Mpira wa sasa sio historia ya miaka hiyo ulifanya nini ..
Mpira ni strategic planning (mpango mkakati) wa muda mrefu kwanzia maandalizi ya wachezaji, uongozi , mazingira , saikolojia mpka uwanjani.
kaka hatuwezi kujipa moyo kwa kusema kwa maneno tu kuwa simba ni klabu yenye uzoefu , kwamba inauwezo mkubwa na itashinda league, wakati hatuoni mipango thabiti ya kulithibitisha hilo ukilinganisha na wenzetu upande wa pili ...
Mpira sio swala la kusema tu inshalah Mungu atajalia
Mpira ni mipango kiongozi
Na kama club haitakua tayari kukubaliana na huu ukweli mchungu alioutoa mleta uzi basi tukubali tu kuwa "NEXT YEAR IS OUR YEAR SC"
Sasa bahati mbaya hilo wenzetu wengi hawataki kukubaliana na uhalisia, ukisema ukweli unaonekana mamluki kitu ambacho sii kweliUmeona ehhh! Ukichambua soka ktk upande wa kushabikia mar zote utashindwa kuleta maana.
Zimebaki wiki chache tu kabla ya Ligi kuanza.. Tutaona Tofauti kubwa sana kipindi hiki.
Jamaa wataanza ligi wakiwa fresh_cold, sisi mpaka wachezaji waweze kuclick na formation ila take time, na uvumilivu wa fans sote tuna ujua.
Ni kweli aisee. Inaonekana sisi Mashabiki wa SSC tumeridhika kuizomea Yanga pale inaposhiriki michuano yao, na wala hatujiulizi ni vipi na sisi tutashabikia cha kwetu.Sasa bahati mbaya hilo wenzetu wengi hawataki kukubaliana na uhalisia, ukisema ukweli unaonekana mamluki kitu ambacho sii kweli
Labda niseme hivi,
Mimi naamini falsafa inayosema adui muombee njaa
Siwezi support yanga KAMWE kutoka moyoni.
Hata siku ya match na TP pale taifa walivyo pigwa nilishangilia sana tu.
Lakini mimi kutoipenda yanga, wala kutoishabikia hakuipunguzii yanga uwezo wake
Hata nikiisuport team yangu wekundu , kama club haijajipanga support yangu haitaongeza any efficiency.
Ifike mahali tukubali kubadilika,
Mpira ni zaidi ya ushabiki nazi na zomeazomea..
Binafsi ni shabiki damu wa Klabu ya Simba.
Ila napenda kuzungumzia swala fulani kwa jicho la kipekee kabisa ambalo mwana Simba wa kawaida hawezi kuliona.
Hii leo tumeshuhudia Yanga SC ikiumana na Medeama ya ghana. Kuna kitu numejifunza mimi kama shabiki wa Simba.
Licha ya Yanga SC kufanya ovyo katika hatua hii ya Kombe la Shirikisho wanaonekana sio wa level yetu (Simba) kwa sasa.
1. Kama kuna Klabu ambayo Mungu amepanga ije kubeba Ndoo ya Michuano mikubwa ktk miaka ya usoni basi itakuwa ni Yanga na wala sio Simba. Hii ni kutokana na Uzoefu wanao endelea kuupata Yanga kwenye hii michuano.
Ni rahisi sana kwa wao kufanyia kazi mapungufu na makosa ya timu kutokana na kuwa kwenye ushiriki wa muda mrefu. Tofauti na sisi Simba ambao hata ikitokea tunashiriki ktk hii michuano sidhani kama tutaweza kuleta mafanikio ya ghafla. Itatuchukua misimu zaidi ili tuweze kugaina ile momentum ya michuano. Ikifika hatua hii basi hawa wenzetu watakuwa kwenye hatua ya juu zaidi.
2. Suala la pili ni jinsi Yanga wanavyo sajili. Sisi Simba tumekuwa tukisajili aina ya wachezaji ambao tunalenga watusaidie kwenye ligi tu. Tofauti na Yanga ambayo wananunua mchezaji ambaye wanaona kama ataweza kuwasaidia kwenye michuano ya Kimataifa au la. Usajili huu wa Yanga unawafanya wachezaji waweze kufanya vyema kwenye Ligi zaidi, hii ni kutoka ubora wa players wao ni wa hali ya juu.
Klabu yangu ya Simba Sioni ikija kutoa ushindani mkubwa pindi Ligi itapo anza, hii ni kutokana kusajiliwa kwa wachezaji ambao hawakulikani kama wata_click kwenye kikosi au la. (Ingawa si mshabiki wa Yanga, niseme kuwa bado hatma ya ubingwa wa msimu 2016/17 upo mikononi mwa Yanga SC na kidogo sana kwa azama).
Wapenzi wenzangu wa Simba kaeni mkijua kuwa Klabu yetu inahitaji Msimu ujao kujitathmini kama iko imara au la, asije akakuambia mtu kuwa Simba ina nafasi kubwa ya kubeba ndoo msimu ujao.
Hawa Yanga tunaweza kuwacheka na kuwakejeli kwa kufanya vibaya mechi zao za Shirikisho, ila wakiridu kwenye Ligi hawato kamatika kabisa.
Leo hii wakitolewa kwenye hii michuano hawana la kupoteza kwa kuwa akilini mwao bado wana uhakika kuwa Msimu ujao ni lazima watashiriki michuano hiyo.... Msimu huu wa Ligi watautumia kama kuwania tiketi ya kushiriki michuano ya Kimataifa ya msimu Keshokutwa.
KWA HIVYO KOCHA WA MEDEAMA AKISEMA KWAMBA ANAITAMBUA SIMBA SC & GOR MAHIA TU...Ulimsikia lakini kocha wa madema na timu captain. Au unahorojoka tu. Wamesema kwenye huu ukanda wa africa mashariki na kati wanazijua timu mbili tu. Nayo ni Simba na Gormahia ya kenya. Nenda huko wewe huwezi kuwa wa msimbazi wewe ni wajamgwani tu unataka kujifariji.
Dah! Uwezo wa Kufikiri umegota ukuta?Simba itachukuaje ubingwa wakati Tff na Marefa woote wanataka Yanga ishinde tu,,
Kila mechi lazima ipewe penati au timu pinzani ichapwe red Card,,
Huku kwenye makundi ujinga huu hakuna,, kwa kuionea sn Simba ndiyp maana ikienda huko inapasua sn.
Kuwalazimisha Simba wasizomee Yanga ni kupoteza muda. Ajenda hapa ni kufanya vibaya kwa Yanga kwenye mashindano haya tofauti na matarijio ya Watanzania. Tatizo nini? Nini kifanyike?
Huu ni mwaka wa 18 tangu Yanga ilipocheza hatua za makundi ya klabu bingwa Afrika.
Sijasema kuwa Mashabiki wa Simba tusiwazomee Yanga. Ila wewe Kipofu usiyeona kupitia macho yote 2 utamchekaje yule Kipofu asiyeona kupitia jicho 1?
Ninachomaanisha ni kwamba sawa tuendelee kumcheka Yanga kwa nguvu zote ila tusisahau na sisi kujicheka.
Kwani Ubora wetu Simba unafanana na Yanga kqa sasa! Jibu ni hapana. Hata ikiletwa mechi kesho tu... Nina imani kuwa kampuni za kubashiri zitampa point nyingi Simba na kidogo kwa Yanga. (Kama utakuwa umenielewa)
Nilichozungumza awali ni kuwa wenzetu wamesajili vyema zaidi ya sisi ndio maana wapo hapo walipo na sisi tupo kule tulipo (licha ya wao kufanya vibaya), bado wana nafasi ya kufanya vyema zaidi msimu ujao kwa kuwa wamejifunza kutikana na kushindwa kwao leo. [/b][/B]
Unapo sema hilo pia usisahau kuwa hata sisi tuna Miaka 13 tangu mara ya mwisho tucheze hatua ya makundi CAF
Na tuna Miaka 8 pia tangu tushiriki michuano yoyote ile inayo ratibiwa na CAF.
Tuna Tofauti gani na wao wa miaka 18? Au ndi hiyo miaka 5.