Kinachoibeba ccm ni mfumo wa uchaguzi na sheria zake kiujumla. Tunahitaji tume huru, polis wawe neutral, madaraka ya rais yapunguzwe. Ikiwa hivyo ndo uje ujitape hapa kuwa ccm inajiimarisha lakini kinyume na hapo nawe unajua jinsi ccm inavyobebwa na tume yake, polis, vyombo vya habari vya serikali na pia mahakama. Kumbuka kilichotokea zanzibar na hata huku bara jinsi kura za ubunge na urais zilivyochakachuliwa kupitia mabavu ya polis na tume ya uchaguzi. Nikiona mtu wa ccm akijisifu eti upinzani hauna nguvu namuona kama mtoto wa miaka miwili kujifanya hajui kilichopo hapa nchini.