Mjanja M1
JF-Expert Member
- Oct 7, 2018
- 4,023
- 14,177
Mimi Mjanja M1 sikuwahi kuwaza kama kuna siku nitaandika uzi kwaajili ya wanyama hususani wanyama wa majumbani eg. Paka, Mbwa na wengine ambao tunawafuga.
Kwenye pilika zangu nimekutana na Vitoto vya Paka vikiwa vimetupwa jalalani na muhusika (Mfugaji) hajulikani. NILIUMIA SANA š¢
Ukiachana na suala la kutupa wanyama wanapozaa eg. Paka na Mbwa bado kuna suala la kuwatesa wanyama kwa kuwapiga pindi watu wanapowaona mitaani, kama wewe ni mmoja wa watu waliowahi kuona Mbwa au paka akiwa na shida kwenye mwili wake basi tambua kuwa kuna katili amemnyanyasa mnyama kwa kumrushia mawe au kumpiga na silaha nyengine.
Ninaumia sana ninapoona wanyama wa majumbani wananyanyasika bila ya kuwa na mtetezi wao, Mimi Mjanja M1 kwa kutumia Platform hii ya Jamiiforums naamini ombi langu litafanyiwa kazi na serikali yetu ili wanyama wawe salama zaidi.
Ningependa pia kuiomba Serikali yetu iwe inatoa ruhusa kwa wenye uwezo pekee kuishi na wanyama na sio kila mtu yoyote, Mateso wanayoyapitia wanyama wa majumbani ni makubwa maana wakiumwa wamiliki wanashindwa hata kuwapeleka hospital kwaajili ya matibabu.
NAAMINI OMBI LANGU LITAFANYIWA KAZI, NA PIA WEWE UNAESOMA HAPA NAKUOMBA SANA UUSAMBAZE UJUMBE HUU ILI TUWALINDE WANYAMA WA MJUMBANI NA MATESO.
ASANTENI SANA! š