Naibu waziri wa ulinzi, IGP na Mkuu wa Jeshi Mwamunyange wafika palipotokea mauaji Amboni

Kinachoniuma mimi kesi kama hizi kuchukua hd mwaka bila kumalizika wakati inatakiwa iwe. ndani ya wiki moja wawe wamehukumiwa kunyongwa,
 
Hata hao wauwaji wakikamatwa vyombo vya dola hawajawahi kurud kutuambia adhabu iliyotolewa dhid ya wauwaji ila kila siku watu wanachinjwa na askari wanatangaza msako ila ndo story itaishia hapo
 
Shida ya hawa watu they don't fight conventional war.

Vita yao wanatumia wananchi kama kinga yao kujificha. Hawana uniform za kijeshi huwezi tofautisha kati ya adui na mwananchi wa kawaida.

The only way ya kuwashinda hawa watu ni kupitia vita ya kijasisusi na ulinzi shirikishi.

Kutuma undercover agents wafanye hata infiltration ndani ya hivi vikundi wajiunge nao na wakusanye taarifa za kutosha juu ya orgchat yao na nani anawa'sponsor.

Pia wananchi wanaotoa taarifa zisipuuzwe zifanyiwe kazi na wanaotoa taarifa wafichwe identify zao. Ulinzi shirikishi pia utasaidia kuwazima hawa watu. Vijana wawe trained katika mbinu za kutoa taarifa na mafunzo ya ukakamavu.
 
Nadhani wangeweka kambi ya jeshi hapo badala ya kusambaratisha eneo hilo la kihistoria
Amboni kambi ya jeshi ipo na tangu mambo haya yaanze eneo zima la mapangoni kuna ulinzi mzito toka kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, haileweki ni kwa namna gani jamaa bado wapo na wanapora vyakula na kurudi humo kuendeleza mapambano
 
Hali ya umakini mkubwa inatakiwa sasa,
Kwa situation kama hii Serikali na Wananchi kwa ujumla wake inapaswa kuwa makini mno,
Hao jamaa wanakuwa na mipango ya muda mrefu sana, kama pale Kenya walilisoma jengo la Westgate kwa muda mrefu kiasi kwamba waliweza kuingiza silaha zao na kulimiliki jengo huku vyombo cya ulinzi vya Kenya bikishindwa kuingia kwa wakati, kwa sababu hawakuwa wakilijua Jengo vizuri

Sasa hofu kubwa ni kuwa jamaa wanaweza kuwa wanapanga shambulizi kubwa ila wanatumia kuwazunga Wananchi na vyombo vya Usalama kuwa wako Amboni na Mwanza so focus yote iamie huko, inapaswa tuwe kwenye Taadhari nchi nzima
Hakika mkuu, hawa hawakai mahali bure
 
Kwahiyo utalii umeisha hapo!kumbukeni hayo mapango ni makubwa ht maumau wa kenya walijificha humo.ni pakubwa sana humo ndani
 
Nafikiri bado tunafanya mchezo na maisha ya raia wema.Tunajaribu kugeuza mada('trending issues').
Hili suala la mauaji linachanganywa na siasa. Kwa nini wataalamu hawaachwi wafanye kazi yao?
Wanasiasa ndiyo wanashawishi nani aende kwenye mapambano kati ya Polisi na Jeshi ili kulikuza sana.
Tuna Polisi wetu maalum wa kupambana na Ugaidi na Majanga makubwa ya kijinai.. waachwe wachunguze na kutatua ikiwezekana na wakishindwa wataomba usaidizi JWTZ lakini bado naamini hii ni kazi ya Polisi..
 
Amboni kambi ya jeshi ipo na tangu mambo haya yaanze eneo zima la mapangoni kuna ulinzi mzito toka kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, haileweki ni kwa namna gani jamaa bado wapo na wanapora vyakula na kurudi humo kuendeleza mapambano
Asante Mkuu nilikua sijui hili ,hiyo kambi ya jeshi inaitwaje ??

Tatizo hawa police Wa dogo wanatoa siri za wananchi wanaofichuwa majambani, I don't trust them at all, ukiwa na taarifa nyeti bora ubishe hodi kwa RPC, information is money na ukizitoa sehemu isiotakiwa itakugharim, ndio kinachotokea Kule Tanga. Myself I don't trust these police called "CONSTABLES" they normally don't keep secrecy of their informers. IGP Mangu lazima alijue hilo.Jana tu yule boss Wa wale wahamiaji haramu waliokamatwa kwenye fuso kule TMK u can't imagine inasemekana amewapa CONSTABLE dollar wakamuachia kasepa zake. If you have valuable information regarding majambazi, men,You better go to RPC.
 
Asante Mkuu nilikua sijui hili ,hiyo kambi ya jeshi inaitwaje ??
Huku zinaitwa kulingana na mahali zilipo mfano kambi ya Kange, Raskazone, Jkt maramba nk.

Hiyo ya Amboni ni ya Jwtz na ipo kitambo sana na kuna wanangu wanafanya kazi hapo.
 
Tatizo hawa police Wa dogo wanatoa siri za wananchi wanaofichuwa majambani, I don't trust them at all, ukiwa na taarifa nyeti bora ubishe hodi kwa RPC, information is money na ukizitoa sehemu isiotakiwa itakugharim, ndio kinachotokea Kule Tanga. Myself I don't trust these police called "CONSTABLES" they normally don't keep secrecy of their informers. IGP Mangu lazima alijue hilo.Jana tu yule boss Wa wale wahamiaji haramu waliokamatwa kwenye fuso kule TMK u can't imagine inasemekana amewapa CONSTABLE dollar wakamuachia kasepa zake. If you have valuable information regarding majambazi, men,You better go to RPC.
Hili ni tatizo
 
Ilivyo toka ile video wakihamasisha watu kujiunga nao na wakitoa angalizo kuwa kuna ndugu zao wame kamatwa mwanza na wengine wanalawitiwa.. Tukasema serikali isichukulie mzaha sababu panapofuka moshi kuna moto., ikaja kauli ya mkuu wa mkoa kukanusha ikafatiwa na mahojiano ya wananchi kukiri kuwa kuna watu wanavamia maduka na kupora mali na kujeruhi wananchi pia wakasema wameambiwa mwisho kuwa mashambani saa 10 hapo serikali haikushtuka.. Nadhani Vifo vya wananchi vimetokana na kuonekana ktk tv wakati wakiohojiwa
Ndugu yangu nchi yetu tunaongea sana,tena tunaongea mpaka ambapo hapastahili maelezo mengi ila bado tunaongea.Ndilo tatizo pia la viongozi wetu hapa wanaongea tu kwa kuwa wanajua wao hawahusiki.Ndio maana watu wakikamata mwizi wanaua wenyewe kwa sababu kama hizi.Mambo yalianikwa humu na kule lakini wakaongea kama vile wananchi hawajui kinachowasibu sasa waendelee kuongea ziaidi.Tutaona tunakoelekea,tupunguze kuongea ongea saana.Si kila pahala pa kuongea ongea na kushangilia tutapoteza wengi sana.INAUMA SAANA.
 
Yani nikaamua kabisa kujiita "Mapango ya Amboni" ili kuutangaza utalii hasa wa ndani, leo hii mapango ya Amboni yamekua ni sehemu ya magaidi kujificha!? Jamani vyombo vya ulinzi na usalama fanyeni kila muwezalo kuirudisha Tanga yetu katika hadhi yake ya utulivu na amani. Hatujozea kabisa kusikia watu wengi hivyo wanauawa Tanga na eidha majambazi au magaidi. Nashauri pia kuwe na program maalum ya kuhuisha ziara za mara kwa mara "Mapango ya Amboni". Zianze na viongozi wa serikali, na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kama ilivyokua zamani. Lakini baada ya kuhakikisha pamesafishwa na serikali ina control kamili, msije mkatuulia watoto huko.
 
Back
Top Bottom