Ubalozi wa nchi gani bado giza tororo, nani amepewa nafasi yake pia ni giza. Sina hakika kama ni uteuzi ambao mhusika alijipanga au ni maamuzi yaliyotokana na kelele za wadau. Mimi sijui, wanajua wenyewe waliohusikaBado sijaona mantiki ya Rais kumwondoa Dr.Possi kwenye Unaibu Waziri na kumpa Ubalozi.
Ndio kumtumbua kiana huko? (Mpaka sasa sijaona makosa yake)
Ndio kupunguza wale wabunge wa kuteuliwa wakiume ili wabaki watano? (Sheria haimpi rais mamlaka ya kumvua Ubunge mtu)
Ndio kumpandisha cheo huko? (Dr.Possi ni msomi wa juu wa sheria, Mkufunzi wa chuo kikuu, ana ulemavu wa ngozi nk. Sote tuliamini alipewa uwaziri awe alama ya uwezo wa mtu mwenye ulemavu au fadhila kwa makundi ya walemavu, kumpa ubalozi ni sawa na kuwasha taa na kuificha chini ya uvungu).
Mtihani uliopo mbele ya Rais ni mteule mpya ya nafasi iliyoachwa wazi na Dr. Possi, watu wanategemea atakayechukua nafasi hiyo atapaswa awe ni mtu mwenye Ulemavu, tofauti na hapo kelele zitaanza...